Posts

KUMBUKUMBU YA MAISHA YA MH. ESTER ALEXANDER MAHAWE

Image
Tarehe ya Kuzaliwa: 05 Novemba, 1973 Mahali: Kijiji cha Isale, Wilaya ya Mbulu, Mkoa wa Manyara ELIMU Mh. Ester Alexander Mahawe alianza safari yake ya elimu katika Shule ya Msingi Upper Kitete, Wilaya ya Karatu mnamo 1982-1983 na baadaye kuhamia Shule ya Msingi Isale, ambako alihitimu mwaka 1988. Alipata elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Imboru, Wilaya ya Mbulu kati ya mwaka 1989-1992. Mnamo 1994-1996, alihitimu mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti kutoka Chuo cha Ualimu Monduli, Mkoa wa Arusha. Mwaka 2012-2013, alihitimu stashahada ya Uongozi na Utawala kutoka Chuo cha ESAMI, Mkoa wa Arusha. NDOA NA FAMILIA Mnamo tarehe 17 Septemba 2005, Ester Alexander Mahawe alifunga ndoa na Alexander Samson. Ndoa yao ilijaliwa watoto watatu wa kuwazaa: wavulana wawili na msichana mmoja. Aidha, aliwalea watoto wengine sita na hivyo kuacha jumla ya watoto tisa pamoja na wajukuu tisa. KAZI NA UZOEFU Huduma ya Ualimu: 1996-1997: Mh. Ester alikuwa mwalimu katika St. Constantine International Sch...

*KUNDO AGOMA KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI VWAWA-MLOWO

Image
  Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, amegoma kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Vwawa-Mlowo uliopo Mkoani Songwe, unaotekelezwa na Mkandarasi Mzawa wa kampuni ya Current Construction Ltd ya Jijini Dar es salaam  mpaka changamoto zilizopo zitakapo tatuliwa. Mhandisi Kundo amesema kuwa, changamoto hizo ni pamoja na  kazii kufanyika chini ya kiwango kilichokubaliwa.  Kufuatia hali hiyo, Mhandisi Kundo ameiagiza bodi ya Vwmwassa na RUWASA kuhakikisha kwamba wanamsimamia mkandarasi huyo,  ili aweze kufanya marekebisho kwa kasoro zote zilizobainika. Mhandisi Kundo amechukua uamuzi huo leo Januari 14, 2025 katika siku ya pili ya ziara yake ya siku mbili Mkoani Songwe, baada ya kusomewa taarifa ya maendeleo ya utekeleza kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vwawa-Mlowo (Vwamwassa), Mhandisi Clavery Casmir. "Niko tayari kupewa majina mabaya, lakini kwa mradi huu siwezi kuweka jiwe la msingi mameneja wa Wilaya, hata ...

NAIBU WAZIRI WA MAJI AZINDUA VISIMA VILIVYOJENGWA NA MBUNGE MWENISONGOLE MILIONI 65

Image
Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, amezindua mradi wa visima viwili vilivyojengwa kwa juhudi za Mbunge wa Jimbo la Mbozi, Mheshimiwa George Mwenisongole, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. Visima hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 65 vimejengwa katika vijiji vya Ileya na Sambewe vilivyopo Kata ya Itumpi, na vinatarajiwa kuhudumia zaidi ya wananchi 4,068. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mbunge Mwenisongole alimshukuru Naibu Waziri kwa kukubali mwaliko wake na kuwa kiongozi wa kwanza wa ngazi hiyo kutembelea vijiji hivyo tangu uhuru. Alisema visima hivyo ni sehemu ya juhudi za kuunga mkono kampeni ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani. "Niliona mateso ya wananchi wangu, hususan kina mama waliokuwa wakitegemea maji ya mvua kwa msimu mzima. Leo hii tumewapa suluhisho la kudumu kwa visima hivi, ambavyo ni historia kwao. Natoa shukrani kwa wadau wote waliosaidia kufanikisha mradi huu," alisema Mwenisongole. Kwa upande wake, ...

TABIA ZINAZOWEZA KUKUFANYA USIKUBALIKE KWA JAMII

Image
  karibu nawe, maana ni moja ya viashiria vya dharau na majivuno. Mtu anayeringa hana rafiki na taratibu atajikuta akigombana na kila mtu na baadaye atajikuta anaishi kwenye dunia ya peke yake. MASENGENYO Kusengenya wengine ni tabia isiyokubalika na jamii. Kwa bahati mbaya sana ni kwamba, msengenyeji huwa hajui kama ana tabia hiyo. Ilivyo ni kwamba, mtu anayesengenya wengine hujisahau. Leo akiwa mahali anamsema fulani, kesho atakwenda kuzungumza na yule aliyemsengenya jana, akimsengenya mwingine. Taarifa za usengenyaji zikisambaa, mwishowe anajikuta akiwa hakubaliki tena na watu wanaomzunguka. Anashangaa ghafla anaishi kwenye dunia ya peke yake. Hakuna anayemkubali. Akitokea mahali, wenzake wanainuka na kumuacha peke yake. Alama hii ikuzindue usingizini na ukae mbali na usengenyaji ili usijitengenezee mazingira ya kutokubalika kwenye jamii unayoishi. KUTOJITOA Kuna watu wana tabia za ajabu sana… yanapotokea mambo kwenye jamii hana muda wa kushiriki. Hili ni tatizo kubwa na husababi...

MWILI WA BINTI ALIEBAKWA Rucu WAZIKWA KWAO ILEJE

Image
 Mwili wa Rachael Mkumbwa wazikwa Ileje Baba mzazi wa marehemu aliangukia jeshi la polisi Denis Sinkonde.,Mwananchi Denissinkonde@mwananchi.co.tz Ileje. Wakati mwili wa Rachael Mkumbwa ukizikwa leo katika kjiji cha Isongole kata ya Isongole wilayani Ileje Mkoani Songwe baba mzazi wa binti huyo Dickinson Mkumbwa ameliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina kuwakamata waliohusika kuhusika na mauaji hayo. Dickinson Mkubwa amesema licha ya mwanangu kuzikwa Leo naiomba serikali kupitia jeshi la polisi lifanye uchunguzi kuwabaini na kuwakamata wahusika wote ili Sheria ifuate mkondo wake na kukomesha vitendo vya ubakaji. Amesema unyama aliofanyiwa mwanae ni kitendo ambacho hakivumiliki kwani mwanae alikuwa akiishi kwa kumtumikia Mungu lakini amefariki katika mazingira ambayo hayastahikili mioyo yetu. Mkumbwa amesema kama familia wanategemea jeshi la polisi na serikali katika upelelezi ambao utasaidia kuwakamata waliohusika kutenda unyama huo kwani familia ya Racho imeumizwa na taar...

AJALI YA GARI WILAYANI SONGWE YAUA WATATU, YAJERUHI 15

Image
 AJALI YA GARI SONGWE YAUA WATATU, YAJERUHI 15 Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limetoa taarifa kuhusu ajali mbaya ya barabarani iliyotokea Desemba 13, 2024, majira ya saa 12:30 jioni. Ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Mitsubishi Fuso Basi lenye namba za usajili T.701 DEN, mali ya Kampuni ya Mwalumengese. Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi, gari hilo lilipata hitilafu baada ya kupasuka kwa tairi la nyuma, hali iliyosababisha gari hilo kuacha njia, kupinduka, na kupelekea vifo vya watu watatu na majeruhi 15. Mahali na Chanzo cha Ajali Ajali ilitokea katika Barabara ya Mkwajuni-Mbalizi wilayani Songwe. Dereva wa gari, Omary Ally Mdachi (45), ambaye ni mkazi wa Mkwajuni, alifariki dunia papo hapo. Watu Waliopoteza Maisha Jeshi la Polisi limewataja waliopoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni: 1. Omary Ally Mdachi (45) – Dereva wa gari, mkazi wa Mkwajuni. 2. Lugano Mwakasole Asangalwisye (25) – Mkulima, mkazi wa Saza, Wilaya ya Songwe. 3. Mwanamume mmoja ambaye bado hajafahamika, ...

KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA "MAMA SAMIA" KUZINDULIWA MKOANI SONGWE KESHO

Image
  Songwe, Desemba 12, 2024 – Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe inatarajia kuzindua rasmi Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya "Mama Samia Legal Aid Campaign" (MSLAC). Uzinduzi huu umefanyika katika viwanja vya CCM Vwawa na unatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika kutoa haki na msaada wa kisheria kwa wakazi wa mkoa huu. Akizungumza kwa Niamba ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mkuu wa Wilaya ya Ileje Farida Mgomi katika Kikao na Waandishi wa habari aliwahimiza wananchi wa Songwe kuchangamkia fursa hii adimu ya kupata msaada wa kisheria bure. "Haki za msingi za binadamu hazipaswi kupuuzwa. Kampeni hii inalenga kutoa msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa ukatili wa kijinsia, unyanyasaji, na wale waliokosa fursa ya kutetea haki zao," alibainisha. Kampeni ya "Mama Samia Legal Aid Campaign" inalenga kuongeza ufahamu wa sheria kama chombo muhimu cha kulinda haki za binadamu.Kutoa msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa vitendo vya u...

BONANZA LA MICHEZO MOROGORO LAHAMASISHA KUPINGA UKATILI KWA WAFANYAKAZI WA NDANI

Image
Mtaa wa Shule, Kata ya Chamwino, Manispaa ya Morogoro, uligeuka kitovu cha mshikamano na hamasa, wakati Bonanza la Michezo lenye lengo la kuendeleza juhudi za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wafanyakazi wa ndani lilipofanyika leo. Tukio hili la kipekee liliandaliwa na Taasisi ya The Light for Domestic Workers na kuhudhuriwa na mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwanamke na Mafanikio, Bi. Maria Mapunda. Katika hotuba yake, Bi. Mapunda aligusia masuala muhimu kuhusu haki na ustawi wa wafanyakazi wa ndani. Alisisitiza umuhimu wa mikataba ya maandishi, malipo sahihi na kwa wakati, pamoja na kuwajengea mazingira ya kazi yenye upendo, heshima, na thamani. Aidha, alieleza kuwa mafunzo ya awali kwa wafanyakazi wa ndani yanapaswa kuwa kipaumbele ili kupunguza makosa ya mara kwa mara kazini. "Ni wajibu wetu kama jamii kuhakikisha tunawalinda na kuwaendeleza wafanyakazi wa ndani. Wanapaswa kulipwa stahili zao kwa haki, kuelekezwa majukumu yao, na kupendwa kama binadamu wengine. Ukatili wa...

AGIZO LA WAZIRI WA UJENZI LATEKELEZWA KWA VITENDO SONGWE

Image
  Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imetekeleza kwa mafanikio maagizo ya Wizara ya Ujenzi yanayolenga kupunguza changamoto ya msongamano katika barabara ya TANZAM, hususan eneo la Tunduma, maagizo ambayo yalitolewa Novemba 18, 2024 na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Innocent  Meneja wa TANROADS Mkoa wa Songwe, Mhandisi Suleiman Bishanga, amesema juhudi hizo ni matokeo ya mwongozo uliotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Innocent Bashungwa. "Waziri alitoa maagizo ya kutafuta suluhisho la haraka, na kwa kushirikiana na TANROADS Mkoa wa Mbeya, tumefanikisha kupunguza msongamano mkubwa uliokuwa ukisababisha usumbufu kwa madereva," alisema Mhandisi Bishanga.                Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuweka mizani ya ziada inayohamishika (mobile weighbridge) kwa ajili ya kupima magari yanayotoka Tunduma kwenda Dar es Salaam, uimarishaji wa usi...

IDADI YA VIFO VYA KINA MAMA NA WATOTO WAKATI WA KUJIFUNGUA VYAPUNGUA MKOANI SONGWE

Image
  Songwe - Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe amefungua rasmi kikao kazi maalum kinachofanyika Tunduma, kilicholenga kujadili vifo vya akina mama na watoto wachanga vitokanavyo na matatizo ya uzazi. Katika kikao hicho, Seneda aliwapongeza watumishi wa sekta ya afya kwa kazi kubwa wanayoifanya, ambayo imeleta matokeo chanya kwa kupunguza idadi ya vifo hivyo mkoani Songwe. “Haya ni maendeleo makubwa sana kwani hata idadi ya wagonjwa wanaopewa rufaa kwenda hospitali ya kanda imepungua kwa kiasi kikubwa,” alisema Katibu Tawala huyo. Alieleza kuwa jitihada za serikali na utendaji mzuri wa wahudumu wa afya umeanza kuonyesha matokeo chanya katika kupunguza vifo vya mama na mtoto mkoani humo. Kwa mujibu wa takwimu zilizowasilishwa kwenye kikao hicho, mwaka 2022 kulikuwa na vifo 38 vya akinamama vilivyotokana na matatizo ya uzazi, huku vifo vya watoto wachanga vikiwa 320. Hata hivyo, mwaka 2023 idadi hiyo ilishuka hadi vifo 33 vya uzazi na vifo 196 vya watoto wachanga. Hii ni sawa na uwiano wa...

BARAZA LA MADIWANI LAWAPONGEZA WALIMU UFAULU WA DARASA LA SABA

Image
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi limewapongeza wanafunzi wa darasa la saba kwa kufanya vizuri na kuazimia kianzisha programu za mitihani ya wiki ikiwa ni mkakati wa kupandisha kupandisha ufaulu. Akizungumza katika kikao hicho cha Baraza la kupokea taarifa za Kata Mwanyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Mhe. George Musyani amesema kuwa jitihada zilizofanywa na wataalamu kupandisha ufaulu zinatakiwa kutiliwa mkazo ili kuongeza kiwango cha ufaulu.   "Tutengeneze mkakati ambao tutakwenda nao mpaka mwakani ili watoto wetu wafaulu zaidi. Nawashukuru walimu kwa jitihada zao zilizowafanya wanafunzi hao kuongeza ufaulu kutoka asilimia 74 mpaka asilimia 81" amesema na kuongeza; "Twendeni kianzisha programu za mitihani ya kila mwisho wa wiki ambayo inaweza kufanyika kwa kushindanisha shule kwa shule ambayo itawafanya wasome kwa bidii. Tujitahidi kwenda kutoa elimu kwa wananchi wetu kuhusiana na suala hili ili wote tuwe na uelewa wa pamoja ili kusitokee manung...

FAINI MILIONI 20 UKIPEKUWA SIMU YA MWENZA WAKO

Image
 Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ludewa Awataka Wanandoa Kuacha Kupekua Simu za Wenza Wao Katika juhudi za kuimarisha amani na utulivu ndani ya familia, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe, Selestin Luhende, amewashauri wanandoa kuacha tabia ya kupekua simu za wenza wao. Akizungumza na waandishi wa habari, OCD Luhende amesisitiza kuwa kitendo hicho kimekuwa chanzo cha migogoro mingi katika ndoa, migogoro inayoweza kusababisha kuvunjika kwa ndoa na madhara mengine yanayoathiri familia na jamii kwa ujumla. Luhende ameonya kuwa kitendo cha kupekua simu ya mwenza ni kinyume cha sheria, na endapo mwanandoa atapatikana na hatia ya kufanya hivyo, anaweza kukabiliwa na adhabu kali. Sheria inatoa adhabu ya faini ya kati ya Shilingi milioni 5 hadi Shilingi milioni 20, kifungo cha miaka mitano jela, au adhabu zote kwa pamoja. "Kila mtu anapaswa kuheshimu faragha ya mwenza wake na kuepuka vitendo vinavyoweza kusababisha migogoro isiyo ya lazima katika ndoa," amesema Luhende. Ameo...

MKURUGENZI DAR 24 MEDIA AKANA KUTEKWA ADAI NI WEZI WALITAKA KUMUIBIA FEDHA NA WALIMLEVYA

Image
 Mkurugenzi Mtendaji wa Television inayotoa habari mitandaoni ya Dar 24 Media ambaye pia ni Mtendaji wa Data Vision aitwaye MacLean Godfrey Mwaijonga ambaye alipotea tangu October 31,2024 alipotoka ofisini saa 11 jioni, amepatikana jioni ya leo November 02,2024 eneo la Buyuni Wilayani Kigamboni Jijini Dar es salaam ambapo amesema hakutekwa bali Wafanyabiashara wenzake walimlevya na wakapanga kuiba pesa zake na vitu vingine. Akiongea na Ayo TV usiku huu mbele ya Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es salaam Jumanne Muliro na Familia yake Central Police Dar es salaam, MacLean amesema hakutekwa maeneo ya ofisini kwake bali alienda mwenyewe Kigamboni kukutana na Wafanyabiashara wenzake anaowafahamu ili wafanye maongezi ya kibiashara lakini wakamuwekea dawa za kulevya kwenye juisi na akapoteza fahamu na alipozinduka wakaanza kumshinikiza awape password za benki na za mitandao ya kampuni anazozisimamia “Walinitoa pale nilipokuwa ambap sipafahamu na wakaniweka kwenye gari na kuanza kunizungush...

UHABA WA KONDOMU WILAYANI MOMBA WAZUA WASIWASI WA MAAMBUKIZI YA VVU

Image
  Diwani wa Kata ya Mpapa, wilayani Momba, George Kansonso, amelalamikia uhaba wa kondomu katika kata yake, akisema kuwa hali hiyo inaongeza hatari ya maambukizi mapya ya VVU na magonjwa mengine yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiana. Kansonso alieleza wasiwasi huo mbele ya Baraza la Madiwani na kusisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za haraka ili kuhakikisha upatikanaji wa kinga hizo. Akijibu malalamiko hayo, Afisa Maendeleo wa Wilaya ya Momba, Haroub Almas, alisema kuwa wilaya hiyo inatarajia kupokea kondomu 54,000 kama hatua ya awali, na idadi hiyo itaongezwa pindi zitakapopatikana zaidi. Almas aliongeza kuwa kondomu hizo zitasambazwa katika maeneo yote muhimu, lengo likiwa ni kuwafikishia wananchi kwa urahisi. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Mathew Chikoti, aliunga mkono juhudi hizo lakini akashauri kuwa usambazaji wa kondomu ufanyike kwa umakini. Alisisitiza kuwa kondomu hazipaswi kuachwa kwenye maeneo ya hospitali pekee, kwani hospitali ni mahali pa kutibiwa na si ...

BARAZA LA MADIWANI MOMBA LATOA SHUKRANI KWA NAIBU WAZIRI SILINDE KWA KUSAIDIA MALIPO YA FEDHA KUTOKA NFRA

Image
Baraza la Madiwani Momba Latoa Shukrani kwa Naibu Waziri Silinde kwa Kusaidia Malipo ya Fedha Kutoka NFRA Baraza la Madiwani wa Wilaya ya Momba limetoa shukrani za dhati kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa David Silinde, kwa jitihada zake zilizowezesha Halmashauri hiyo kulipwa fedha zao kutoka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA). Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani, Mathew Chikoti, Halmashauri ya Momba imelipwa jumla ya shilingi milioni 156.3 ikiwa ni ushuru wa mazao, pamoja na shilingi milioni 65.6 kama kodi ya pango kwa maghala matatu ya kuhifadhi nafaka kwa kipindi cha mwaka mmoja. Fedha hizi zilikuwa zikidaiwa kutoka NFRA na sasa malipo hayo yamekamilika kwa msaada wa jitihada za Naibu Waziri Silinde. Akizungumza wakati wa kufunga kikao cha Baraza hilo, Mwenyekiti Chikoti alieleza kuwa malipo hayo yameleta faraja kubwa kwa Halmashauri, na kuongeza kuwa fedha hizo zitasaidia kuboresha sekta ya kilimo na huduma za jamii katika Wilaya ya Momba. “Tunamshukuru san...

MADIWANI WAPITISHA AZIMIO KUZIITA SHULE MAJINA YA DC NA DED WA SONGWE KUTAMBUA MCHANGO WAO KATIKA KUIMARISHA MAHUSIANO NA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI

Image
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Songwe limepitisha azimio la kuzipa majina ya Solomon Itunda (Mkuu wa Wilaya ya Songwe) na CPA. Cecilia Kavishe (Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe) shule mbili mpya ambazo ujenzi wake umeanza, ikiwa ni kutambua mchango wa viongozi hao wa kuimarisha mahusiano katika wilaya hiyo pamoja na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo. Azimio hilo limepitishwa leo Jumanne Oktoba 22, 2024 wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa Sambila uliopo katika ofisi za Halmashauri. Azimio hilo limepitishwa baada ya madiwani kupata nafasi kila mmoja kujadili sababu za kuzipa shule hizo majina ya viongozi hao, wakieleza kuwa wamekuwa wakiimarisha mahusiano na kusababisha Wilaya kuwa na utulivu pamoja na usimamizi mzuri wa fedha zinazoletwa kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Katika azimio hilo, Shule ya Amali inayojengwa katika kijiji cha Iseche Kata ya Mwa...

DC MBOZI APANDA GUTA KUHAMASISHA WANAMBOZI KUJIANDIKISHSMA DAFTARI LA MPIGA KURA

Image
Oktoba 2024 - Mlowo, Mbozi Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Ester Mahawe, ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Mbozi, hususani wakazi wa Mlowo, kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la orodha ya wapiga kura, ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni. Akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mjini Mlowo, Mkuu wa Wilaya alisisitiza umuhimu wa kila raia aliye na sifa kuhakikisha amejiandikisha ili kupata fursa ya kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi. Alieleza kuwa ushiriki wa wananchi ni msingi muhimu wa maendeleo na demokrasia, huku akiwakumbusha kuwa uamuzi wa viongozi wa mitaa unategemea kura zao. "Nawaomba mujitokeze kwa wingi katika zoezi hili la kujiandikisha, kwani ni haki na wajibu wetu kama wananchi. Kupiga kura ni moja ya njia kuu ya kushiriki katika maendeleo ya wilaya yetu," alisema Bi. Mahawe wakati wa kampeni hiyo ya hamasa. Aidha, Mkuu wa Wilaya alisisitiza kuwa Serikali ya Wilaya ...

RC CHONGOLO AMETEMBELEA MRADI WA MAEGESHO YA MAGARI YA MIZIGO CHIMBUYA,MBOZI

Image
I'm Songwe, Tanzania – Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo, amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha maegesho ya magari ya mizigo (malori) katika eneo la Chimbuya, Wilaya ya Mbozi. Mradi huu ni sehemu ya juhudi za serikali za kuboresha miundombinu ya uchukuzi na kurahisisha usafirishaji wa mizigo katika maeneo yanayopakana na mipaka, hususan mpaka wa Tunduma. Mradi huo unatekelezwa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na unaendelea chini ya usimamizi wa mkandarasi Mehrab Construction Co. Ltd. Kituo hicho kitakapokamilika, kitakuwa na uwezo wa kupokea malori takribani 90 kwa wakati mmoja, hatua ambayo itasaidia kupunguza msongamano wa magari katika barabara za mipakani, ambapo mara nyingi malori yanakuwa yameegeshwa kiholela kando ya barabara. Mhe. Chongolo, akiwa na viongozi wa Mkoa, alisisitiza umuhimu wa kukamilisha mradi huo kwa wakati uliopangwa ili kuanza kutoa huduma haraka kwa manufaa ya wafanyabiashara na wananchi wa Songwe na maeneo ya jiran...