SIKU YA KIMONDO YAINGIWA NA MAUZA MAUZA FIDIA KWA WANANCHI ZADAIWA KUWAKIMBIA NGORONGORO KUFANYA MAANDALIZI MKOA JIRANI
MAADHIMISHO ya siku ya kimondo duniani yaliyokuwa yafanyike kesho (leo) katika Mkoa wa Songwe yameingia dosari baada ya Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro (NCAA) kuhamishia mkoani Mbeya shughuli za utangulizi wa maadhimisho hayo ambazo awali zilipangwa kufanyika Mkoani Songwe. Maadhimisho ya siku ya kimondo yalianza kuadimishwa mwaka 2017 Mkoani hapa, ambapo huambatana na maonesho ya biashara ya siku tatu na kuhitimishwa na kongamano la la kisayansi kuhusu elimu ya utalii wa anga na uhifadhi wa mali kale. Hata hivyo, katika hali ya kushangaza kongamano hilo la kisayansi kuhusu elimu ya utalii wa anga na uhifadhi wa mali kale lililopangwa kufanyika jana Juni 29, 2023 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe ghafla lilihamishiwa Mkoani Mbeya. Taarifa za uhakika kutoka ndani ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe zimeeleza kuwa hali hiyo ya kuhamishwa kwa kongamano hilo na kwenda kufanyikia Mkoa jirani wa Mbeya kumetokana na kile kilichoelezwa kuwa huenda Mamlaka hiyo inakwepa agizo