KAMANDA WA POLISI SONGWE APELEKA SOMO LA UKATILI WA KIJINSIA KANISANI TUNDUMA ATOA WITO
Kamanda wa polisi mkoa wa songwe kamishna msaidizi wa jeshi la polisi Theopista Mallya ametembelea kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo chini ya mchungaji Edwine Sostenes katika mtaa wa Nyerere mjini Tunduma wilaya ya Momba mkoani Songwe Kamanda wa polisi mkoa wa songwe alipata nafasi ya kutoa elimu kwa waumini wa kanisa hilo Katika mambo mbalimbali ambayo yanapelekea matendo maovyo na kupelekea ukatili wa kijinsia na uhalifu, Ikiwa pamoja na Rushwa,Ulawiti,Tamaa ya mali,Kubaka,Wivu wa Mapenzi,Ushoga Migogoro ya ardhi, Ulevi uliokithili,Imani za kishirikina, Huduma za polisi ni bure,Kudhini na ndugu wa damu na pia Wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili kutokomeza vitendo hivyo katika maeneo yao yanayowazunguka. Aidha elimu hiyo imetolewa kwa kutumia vifungu mbalimbali vya maandiko katika Biblia vinavyozungumzia mambo hayo, Sambamba na hayo aliyataja madhara ya vitendo hivyo ikiwa pamoja na Matatizo ya akili, ulemavu, kujitenga na marafi...