Machapisho

SILINDE AWAPA SIKU 30 WAMILIKI VIWANDA VYA CHAI KULIPA MADENI WAKULIMA

Picha
  SERIKALI imetoa mwezi mmoja kwa wamiliki wa viwanda vya chai nchini kulipa madeni wanayodaiwa na wakulima wadogo wa zao hilo. Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde, alitoa agizo hilo juzi jijini hapa alipokuwa akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Chai Duniani. "Hadi kufikia Juni 20 mwaka huu wamiliki wote wa viwanda wanaodaiwa na wakulima wadogo wa zao la chai wahakikishe wanalipa madeni hayo ili wakulima wetu wanufaike na kazi waliyofanya katika kipindi chote cha msimu,"alisema. Aidha, Silinde alisema serikali imeweka mikakati ya kuongeza uzalishaji wa zao ilo kwa kufufua mashamba yaliyotelekezwa na kujenga viwanda saba vya kuchakata zao hilo vitakavyomilikiwa na wakulima wadogo. Alisema mkakati mwingine wa serikali ni kuhakikisha inaweka miundombinu ya umwagiliaji katika mashamba ya chai ili wakulima walime misimu yote.  Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Chai Tanzania, Rukia Mwango alisema serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha zao la chai linasimama...

WATU 18 WAJERUHIWA BASI LA TAKBIIR LAPINDUKA SINGIDA

Picha
  WATU 18 wamejeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Takbiir lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Katoro mkoani Geita kupinduka. Basi hilo lenye namba za usajili T 278 DTZ limepinduka saa 1: 00 asubuhi leo Mei 23, 2024 katika eneo la Manga nje kidogo na Manispaa ya Singida. Majeruhi wa ajali hiyo wakizungumza na Nipashe Digital ambayo ilifika muda mfupi baada ya ajali kutokea wamesema basi hilo lilipunduka baada ya kutaka kulipita gari dogo na kugonga daraja dogo na kupinduka. 1 Nipashe Digital ambayo imefika eneo la tukio muda mfupi baada ya ajali kutokea imeshuhudia majeruhi wakichukuliwa  na magari ya wagonjwa (ambulance) wakipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mandewa mkoani Singida.

BREAKING NEWS: WATU 11 WAFARIKI DUNIA BAADA YA KIWANDA CHA MTU WA KULIPUKA

Picha
  Watu 11 wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya mfumo wa joto wa kiwanda cha kuzalisha sukari cha Mtibwa kulipuka wakati wakijiandaa kuanza uzalishaji wa sukari kwenye kiwanda hicho kilichopo Turiani mkoani Morogoro. Akizungumza na Mwananchi Digital leo Alhamisi Mei 23, 2024, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Shaban Marugujo amesema mlipuko huo ulitokea saa 7 usiku na umeua watu 11 na wengine wawili kujeruhiwa. "Ni kweli watu 11 wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya mlipuko wa mpira wa joto wakati wanajiandaa na uzalishaji wa sukari pale kiwandani. Ifahamike ili sukari ichakatwe kuna kiwango cha joto ambacho kinatakiwa kifikie, sasa wakati maandalizi ya uzalishaji yakifanyika na kile kiwango cha joto kikingojewa ndipo ukatokea mlipuko huo na kuwakuta watu hao 11 ambao kwa kiwango kile cha joto wakafariki papo hapo," amesema Marugujo. Amesema:"Chanzo halisi cha mlipuko huo bado hatujakipata ila bado tunaendelea na ...

TANI 500,000 ZA MAHINDI MEUPE KUUZWA JAMHURI YA DEMOKRASIA YA CONGO (DRC)

Picha
Serikali imeendelea kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya uhakika ya mazao ili wakulima wazidi kunufaika na bei nzuri ya mazao ma uhakika wa usalama wa chakula nchini na katika nchi za jirani. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mauziano ya mahindi meupe baina ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi Chakula (NFRA) na Kampuni ya Quincy kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) tarehe 21 Mei 2024, jijini Dodoma. Mkataba huo umesainiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA, Dkt. Andrew Komba pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Quincy, Bw. Yuma Jesse huku ukishuhudiwa na Gavana wa Jimbo la Katanga, Bw Jacques Kyabula Katwe pamoja na Katibu Mkuu Mweli. Mkataba huo unahusisha awamu mbili za mauziano ya mahindi ambapo kwa awamu ya kwanza nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) itakabidhiwa tani 200,000 za mahindi meupe huku tani 300,000 za mahindi hayo zikitarajiwa kukabidhiwa katika awamu ya pili ili kukabiliana na changamoto ya uko...

RPC SONGWE " KAZI YA POLISI NI TAKATIFU"

Picha
Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Songwe wametakiwa kutambua kuwa kazi ya Polisi ni kazi takatifu ambayo majukumu yake yanahusiana na makatazo na amri za Mungu. Kauli hiyo imetolewa Mei 22, 2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga alipofanya baraza na Maafisa, Wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali. “Makatazo yaliyoandikwa kwenye vitabu vitakatifu yana mahusiano makubwa na kazi ya Polisi hasa katika amri za Mungu ambazo katika nyumba za ibada wanaziita dhambi huku kwetu ni uhalifu inatupasa kuzuia vitendo hivyo ili jamii iwe salama” Kamanda Senga alisema hayo Kamanda Senga alisema watendaji wa Jeshi la Polisi ni kioo kwa jamii hivyo basi wanapaswa kuendelea kulinda taswira nzuri ya Jeshi la Polisi kwa Jamii kwa kutenda haki katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili jamii iendelee kukimbilia na kushirikiana nalo katika kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu. Naye, Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Pol...

KASI YA UTEKELEZAJI MAAGIZO YA CHONGOLO MBOZI YAMKOSHA DC MAHAWE

Picha
  Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Ester Mahawe amempongeza kasi ya ukarabati wa miundo mbinu ya stendi ya Mlowo unaendelea kufuatia agizo la  Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo la kutaka stendi hiyo ianze kutumika hivyo aliwataka Halmashauri ya Mbozi kuhakikisha stendi hiyo inaanza kufanya kazi sambamba na kufanya marekebisho ya miundombinu. Akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbozi Abdalah Nandonde sambamba na Katibu Tawala wa Mbozi Mahawe alikagua ukarabati unaondelea na kujiridhisha huku akisisitiza Mkurugenzi kuhakikisha mara baada ya kuanza kutumika ahakikishe ukusanyaji wa mapato unafanyika kwa kuweza kuongezea Halmashauri mapato lakini pia waweze kukara

ABURUZWA MAHAKAMANI KWA KUFANYA MAPENZI NA MWANAYE

Picha
Mkazi wa Nyakato mkoani Mwanza, Bashiri Mohamed (35), amefikishwa mahakamani leo Mei 21,2024, na kusomewa shtaka moja la kuzini na maharimu. Mshtakiwa huyo amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza na kusomewa shtaka hilo lenye kosa analodaiwa kulitenda kati ya Septemba hadi Februari 15, 2024. Akisoma shtaka hilo, mwendesha mashtaka wa serikali Mwanahawa Changale amesema; "Mshtakiwa kwa tarehe tofauti kuanzia Septemba 2023 hadi Februari 15, 2024, eneo la Nyakato-Mecco, wilaya ya Ilemela anadaiwa kuzini na maharimu (16) huku akitambua ni mtoto wake wa kumzaa." Amesema mshtakiwa ametenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 158 (1) (a) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022. Hata hivyo, baada ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa amekana shtaka na kuomba apatiwe dhamana. Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkazi Mwandamizi, wa mahakama hiyo Juma Opudo amemtaka mshtakiwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na wadhamini wawi...

MBOZI WATEKELEZA AGIZO LA CHONGOLO KWA HARAKA STENDI YA MLOWO

Picha
  Halmashauri ya Mbozi imetekeleza kwa vitendo na haraka agizo la Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo alilowataka kuhakikisha stendi hiyo inaanza kufanya kazi na kurekebisha miundo mbinu ya stendi hiyo ili wasafiri na wafanyabiashara waweze kurejea ndani na marekebisho hayo yanaendelea kwa kasi kama ambavyo picha zinavyoonyesha

MAFUTA YA KUPIKIA YAONDOLEWA KODI

Picha
  HABARI: Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema Serikali imeondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika mafuta yaliyosafishwa yanayozalishwa na viwanda vya ndani kwa lengo la kupunguza bei ya mafuta ya kula ili yaweze kushindana na mafuta yanayotoka nje ya nchi. Dkt. Kijaji ameyasema hayo leo Mei 21,2024 Bungeni Jijini Dodoma na wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25. Vile vile, katika mwaka 2022 Serikali ilifanya Mabadiliko ya Sheria ya Ushuru wa Forodha na kupunguza ushuru wa uagizaji wa mafuta ghafi ya chikichi (Crude Palm Oil) kutoka 25% hadi 0% ambapo lengo la mapendekezo hayo lilikuwa ni kusaidia viwanda vya ndani vinavyochakata mafuta ya chikichi (Crude Palm Oil) vipate malighafi na kusaidia upatikanaji wa bidhaa hiyo kwa bei nafuu”,amesema. Aidha, ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuweka mazingira mazuri kwa uwekezaji na hilo kupelekea kuongezeka kwa Mikoa inayolima mbegu za mafuta ya kula nchini ...

SILINDE; AIAGIZA ASA KUJENGA GHALA NA KIWANDA NZEGA

Picha
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Dkt. Sophia Kashenge kuharakisha mchakato wa ujenzi wa ghala la kuhifadhia mbegu zinazovunwa kwenye shamba la mbegu la Kilimi lililopo wilaya ya Nzega, mkoani Tabora. Amesema hayo wakati wa ziara yake tarehe 18-19 Mei 2024 Wilaya ya Nzega ambapo amekagua maendeleo ya uzalishaji wa mbegu kwenye shamba hilo ambalo limeshawekewa miundombinu ya umwagiliaji ili liweze kuzalisha mbegu bila kutegemea mvua. Naibu Waziri Silinde amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alikuwa na maono ya kuiwezesha nchi kuzalisha mbegu za mazao na ili kuhakikisha malengo ya Mhe. Rais yanatimia lazima lijengwe ghala madhubuti la kuhifadhia mbegu na kukamilika ifikapo mwezi Oktoba 2024 ambapo litahakikishia wakulima uhakika wa mbegu kama alivyokusudia Mhe. Rais. Aidha, Mhe. Silinde ameagiza kuanza kwa mchakato wa upatikanaji wa kiwanda cha kusindika mbegu ndani ya sha...

MIAKA 30 JELA KWA WIZI WA SIMU

Picha
Mahakama ya Hakimu mkazi mfawidhi mkoa wa Lindi imemuhukumu Naimu Ally M'baruku @ Soggy, mwenye miaka 20, mkazi wa mtaa wa Ndoro manispaa ya Lindi kwenda Jela kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kunyang'anya simu aina ya TECNO SPARK 8 kwa kutumia silaha (Panga). Aidha Mahakama hiyo imewahukumu Zuberi Saidi Mnape mwenye miaka 47, mkazi wa Kiangala, Liwale - Lindi, Jemedari Hemedi Mpulumila mwenye miaka 67, mkazi wa Mbagala - Dar es salaam na Mohamedi Juma Mbacho mwenye miaka 49, mkazi wa Nachingwea - Lindi kwenda Jela kifungo cha miaka Ishirini kila mmoja au kulipa faini ya shilingi milioni mia sita tisini na sita (Tsh.696,000,000/=) kwa makosa ya Kupatikana na Nyara za Serikali (Meno na Pua ya Tembo), Kumiliki Silaha (Bunduki) kinyume na sheria, Kumiliki milipuko/vilipushi (Risasi) kinyume na sheria na Kuua wanyamapori (Tembo) kinyume na sheria. Katika hatua nyingine Mahakama ya wilaya ya Kilwa imemuhukumu Kamugisha Filbert Lugemalila mwenye miaka 47 na Jamilu Swaibu Kichwabuti mw...

BREAKING NEWS: RAIS WA IRAN AFARIKI KWA AJALI,MAMLAKA ZATHIBITISHA

Picha
  Rais wa Iran, Ebrahim Raisi pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo IHossein Amir-Abdollahian wamethibitika kufariki dunia baada ya helkopta waliyokuwa wakisafiria kuanguka wakati wakielekea katika mji wa Tabriz uliopo Kaskazini Magharibi mwa Iran. Chanzo cha ajali hiyo kinaelezwa kuwa ni hali mbaya ya hewa ukiwepo ukungu katika eneo ilipotokea ajali hiyo, hali iliyoifanya helikopta hiyo kupata wakati mgumu kutua. Helikopta hiyo ni miongoni mwa helikopta tatu zilizokuwa katika msafara huo, ambapo mbili zilitua salama. Kabla ya ajali hiyo kutokea, Rais huyo wa Iran alishiriki katika ufunguzi wa mabwawa mawili karibu na mpaka wa Iran na Azerbaijan. Raisi alichaguliwa kuwa Rais wa Iran mwaka 2021

RAIS WA IRAN AMEPOTEA NA HELIKOPTA ILIOMBEBA

Picha
  Helikopta iliyombeba Rais wa Iran, Ebrahim Raisi na wasaidizi wake imepata ajali katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo, huku chanzo kikitajwa kuwa ni hali mbaya ya hewa katika eneo hilo. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran, Ahmad Vahidi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo lakini hajaeleza zaidi. Amesema itachukua muda kupata eneo helikopta hiyo ilipopata ajali kutokana na hali hiyo mbaya ya hewa ikiwa ni pamoja na ukungu mwingi, na kwamba timu mbalimbali za uokoaji kwa sasa zinaitafuta helikopta hiyo. Rais wa Azerbaijan, Ilham Aliyev ameeleza kushtushwa na ajali ya helikopta hiyo iliyombeba Rais Ebrahim Raisi. Kabla ya ajali hiyo Aliyev alikuwa na Rais huyo wa Iran katika ufunguzi wa mabwawa mawili karibu na mpaka wa Iran na Azerbaijan. Amesema Azerbaijan iko tayari kutoa msaada wowote unaohitajika ili kuweza kubaini ilipo helikopta hiyo. Rais Raisi alikuwa akisafiri na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika msafara wa helikopta tatu ambapo helikopta mbili kati ya hizo zimeripotiwa...

MKURUGENZI JIJI MATATANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

Picha
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha kuanza uchunguzi dhidi ya Mkurugenzi wa jiji la Arusha Mhandisi Juma Hamsini na baadhi ya wasaidizi wake wanaokabiliwa na tuhuma za rushwa na ubadhirifu wa fedha za walipa kodi. Akizungumza na wadau wa utalii mkoani Arusha, Makonda amemuagiza Katibu Tawala wa mkoa huo Missaile Mussa kuwasimamisha kazi watumishi wote waliotajwa kuhusika na tuhuma hizo ili kupisha uchunguzi. Makonda amechukua hatua hizo baada ya Mwenyekiti wa waongoza watalii Mkoa wa Arusha Wilbard Chambulo kudai kuwa baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha wamekuwa wakitengeneza nyaraka bandia pamoja na kuchepusha baadhi ya makusanyo ya kodi yanayotokana na sekta ya Utalii. Chambulo amedai kuwa watumishi hao wamekuwa na kampuni hewa za utalii pamoja na kuwa na namba tofauti za ulipaji kodi na usajili hewa wa kampuni zenye kufanana na kampuni halisi za utalii zilizopo ndani ya Jiji la Arush...

ASKOFU AJINYONGA KISA MADENI

Picha
  ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Methodist Tanzania, Joseph Bundala (55), amekutwa amejinyonga kwa kamba ndani ya ofisi yake iliyoko kwenye kanisani hilo, Mtaa wa Meriwa, jijini hapa. Kiongozi huyo wa kiroho, ameacha waraka mrefu ukieleza sababu za kuchukua uamuzi huo kuwa ni madeni na mgogoro ulioko katika uendeshaji wa shule binafsi. Bundala ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kanisa hilo kwa Afrika, mwili wake uligundulika juzi saa 1:00 usiku ukiwa unaning’inia ofisini kwake. Akizungumzia tukio hilo jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Alchelaus Mutalemwa, alisema Jeshi la Polisi linachunguza tukio la askofu huyo, ambaye ni Mkazi wa Ihumwa jijini hapa kuchukua uamuzi huo. “Tukio hilo liligundulika Mei 16, 2024 majira ya saa 1:00 usiku katika mtaa wa Meriwa, Dodoma, ndani ya ofisi yake iliyoko katika kanisa hilo. Uchunguzi katika eneo la tukio umekutwa ujumbe unaeleza sababu za kujinyonga ni madeni na mgogoro uliopo katika uendeshaji wa shule binafsi,” alisema. Alisema taarifa ...

"WAFANYABIASHARA TUMIENI FURSA YA STENDI YA MLOWO KUJIONGEZEA KIPATO" RC CHONGOLO

Picha
 Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo amekagua zoezi la maboresho ya miundombinu na  uunganishwaji wa vyumba vya biashara na pia kuagiza  wajasiriamali wote kuanza biashara zao ndani ya stendi ya mabasi Mlowo Hatua hiyo imekuja baada ya vibanda hivyo vilivyojengwa hapo awali kuwa ni vidogo ambapo Mhe. Chongolo aliagiza vibanda hivyo kurekebishwa kwa kuunganisha vyumba viwili kuwa kimoja. Mkuu wa Mkoa huyo ametoa wito kwa wafanyabiashara kutumia fursa hiyo kuuza biashara zao kuongeza kipato ‘’Kituo chetu hiki kiwe senta ya mauzo au biashara cha mkoa kwahiyo wananchi watumie hii fursa kama hatupo tayari watakuja walio tayari’’ amesema  Ameahidi kuwa atarudi tena katika stendi hiyo ili kuona mchakato unaendeleaje na kuangalia mpangilio wa mabasi na wajasiliamali unaendaje.

RC -CHONGOLO ATANGAZA KIBANO KULINDA USALAMA WA NCHI KWA WATAKAOJIINGIZA KUVUSHA RAI WA KIGENI KINYEMELA

Picha
Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo ametangaza vita kwa wananchi ana mwananchi atakayejii ngiza katika shughuri za uvushaji na usafirishaji wa binadamu ili kulinda usalama wa nchi hasa mkoa wa Songwe uliopo mpakani. Chongolo aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wananchi kupitia mikutano alipokuwa akihitimi sha ziara yake ya kikazi wilayani Momba,pamoja na kuzungumzia hali ya miradi ya maendeleo,alizizitiza hilo ili nchi na mkoa ubaki salama. Amesema zipo nchi nyingi za afrika hali ya usalama sio mzuri,mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yapo ,hivyo wanasongwe wanakila sababu ya kulinda usalama uliopo nchini kwa kutowakaribisha wageni kuingia nchini kinyemela kwa ni hatari. ‘’Raia hao wa kigeni mnapowakaribisha nchini hamjui wamebeba nini wanaweza kuleta hatari kubwa na madhara kwa nchi,hivyo kila mmoja awe mlinzi wa mwenzie,umuonapo mtu usiyemfahamu toeni taarifa kwenye oungozi uliopo karipo nanyi ikiwemo polisi kata.’’amesema Chongolo. Amesema wilaya ya Momba imepakana na nchi za ...

WANAKIJIJI MOMBA WACHANGISHANA MIL,18 KUJENGA SHULE KUHEPUSHA WATOTO KUTEMBEA KILOMETA 10 KWENYE SHULE MAMA

Picha
Na Ibrahim Yassin,Songwe Wananchi wa vitongoji vilivyopo kata ya Ikana wilayani Momba mkoani Songwe wamechangishana fedha Milioni 18 kuanzisha shule ya sekondari Ikana kuokoa adha kwa Watoto wao waliokuwa wakitembea umbali wa kilometa 10 kwenda kwenye shule mama ya Chikandamulilo hali iliyofifisha ufauru kwa Watoto. Akizungumza leo Mei 16/2024 mwenyekiti wa Kijiji cha Ikana Bahati Sikapize amesema baada ya wanafunzi ambao ni Watoto zao kuona wakiteseka kwa muda mrefu wakitembea kilometa 10 kwenda shule ya Chikandamulilo,waliitisha mikutano ya hadhara kuelezana namna ya kujenga shule eneo hilo. Amesema baada ya kuelezana changamoto hiyo,wananchi wakaridhia kuchangashana fedha na kupatikana Milioni 18 na kuanzisha ujenzi wa shule mpya ya Ikana huku wakitoa maombi serikalini kuongezewa nguvu ya fedha ili malengo yao yatimia na yakatimia. Kaimu afisa elimu sekondari wilayani humo,Mwl,Hamis Nywange amesema baada ya wananchi kuanzisha mchakato huo,ujenzi ulianza mwaka 2021/2022 na kukamilika...

DC MAHAWE ATEMBELEA HOSPITALI YA VWAWA KUONA HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA MADAKTARI BINGWA, AWATAKA WANAUME KWENDA KUPATA HUDUMA

Picha
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe. Esther Mahawe ametembelea Hospital ya Vwawa kuangalia mwenendo wa matibabu yanayotolewa na madaktari bingwa kambi ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. Mkuu huyo wa Wilaya ametembelea Hospitali hiyo leo  Alhamisi Mei 16, 2024. Akizungumza na baadhi ya wananchi walifika kupata huduma za kibingwa katika hospitali hiyo, Mhe. Mahawe  amesema kuwa usipokuwa na afya imara huwezi kufanya kazi hata ikiwa na mikakati kiasi gani. "Ni nichukue fursa hii kumshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia  kwa kuwaleta madaktari hawa, tangu Mheshimiwa Rais ameingia madarakani amefanya mambo makubwa sana hasa katika sekta ya afya kwa kuleta vifaa tiba ikiwemo mashine za kisasa" "Lakini kama mmemsikiliza waziri wa afya bungeni akiwasilisha bajeti ya afya kuna ongezeko kubwa baada ya Mhe. Rais kuingia madarakani kulinganisha na ile kabla hajaingia madarakani" "Alitambua sio watanzania wote wanaweza kwenda katika hospitali kubwa za rufaa akaona awalete mad...

UKATILI WA KUTISHA RC NA RPC SONGWE WASHANGAZWA MTOTO WA MIAKA 2 KUBAKWA HADI KUFA KWENYE SHAMBA LA MAHINDI

Picha
  Na Ibrahim Yassin,Songwe MKUU wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo,kwa kushirikiana na kamati ya usalama ya mkoa,ametangaza vita kwa watu wan aoendekeza vitendo vya ukatili kwa Watoto ikiwa ni Pamoja na mauaji yanayotokana na wivu wa kimapenzi na Imani za kishirikina wanazoshauriwa na baadhi ya waganga wa kienyeji. Chongolo ameyasema hayo,leo Mei/16/2024 alipokuwa akizungumza na wananchi wilayani Momba katika ziara yake ya kuji tambulisha baada a Rais Dkt,Samia kumteua kuwa mkuu wa mkoa iliyoenda sambamba na kukagua miradi ya maendeleo. Amesema kitendo cha baadhi ya wananchi wanaoshindwa kupanga mikakati ya kubuni njia sahihi za kutafuta fedha wana enda kwa waganga wa kienyeji ambao wanawaeleza kuwa ili wapate mahali abake mtoto wake kitu ambacho ni uongo wa hali ya juu. ''hivi hao wanganga wanaotoa maelezo hayo kwa wateja zao,wenyewe hali zao zipoje?,ninyi wananchi achene kudanga nywa,eti unaambiwa ili upate mavuno mengi au dhahabu nyingi basi umbake mtoto tena wa kumzaa na wew...

WATOTO ZAIDI YA 194 WAPEWA MIMBA NDANI YA MWEZI MMOJA MOMBA

Picha
  Zaidi ya watoto 190 Wilayani Momba wamepewa ujazito na  kupelekea kuacha masomo  Kauli hiyo imetolewa leo Mei /2024 na mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo alipokuwa aki zungumza na wananchi Kijiji cha Naming"ong"o Wilayani Momba. Amesema kitendo cha wanaume kuwapa ujau zito wanafunzi hakiku baliki,hivyo ame liagiza jeshi la Polisi kuhaki kisha linawaka mata watuhumiwa wote na kufikishwa Mbele ya sheria. "Wakati mkoa wa Kilimanjaro wana watoto 2 pekee waliopewa mimba hapa Momba mwezi uliopita tu watoto zaidi ya 190 wamepewa mimba" amesema Cho ngolo. Hata hivyo Chongolo amewaagiza Viongozi wa vijiji na Kata kuhakik isha watoto wanakuwa salama na kutoa taarifa kwa mkuu wa Wilaya kunusuru sakata hilo.

WATENDAJI SONGWE WAPIGWA MARUFUKU KUTOA VIBALII KWA WAFUGAJI KIHOLELA

Picha
  Chongolo ameagiza watendaji wa vijiji na kata kuacha mara moja kuingiza kiholela wafungaji pamoja na mifugo yao katika vijiji vyote  mkoani Songwe na kutaka ofisi za wakuu wa wilaya ndio ziwe zinatoa vibari hivyo kwa kushirikiana na ofisi  wa wakurugenzi wa halmashauri za mkoani Songwe. Chongolo ameyasema hayo katika ziara yake ya kukagua miradi na kujitambulisha kwa wananchi wa wilaya Momba ambapo amedai kumekuwepo na migogoro inayoweza kuepukika lakini kutokana na utoaji holela wa vibari hivyo ndio sababu ya  migogoro mingi ya wakulima na wafugaji kutoa. "Kijiji kinaruhusu uingiaji wa mifugo kiholela na hakuna eneo la malisho unategea nini kama sio kuleta migogoro ya wakulima na wafugaji? Kuanzia sasa ni marufuku kwa watendaji au kiongozi yoyote wa Kijiji kutoa kibari cha mifugo natoa agizo ofisi za wakuu wa Wilaya ndio zitatoa vibari hivi kwa kushirikiana na Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri" alisema Chongolo Aidha Chongolo amesema kuna kila dalili za rushwa k...

CHONGOLO AANZA ZIARA MOMBA ATOA MAAGIZO BWAWA LA CHIWANDA

Picha
  Mkuu wa Mkoa wa Danieli Chongolo ameagiza bwawa la Chiwanda lililopa Wilayani Momba  kuhakikisha ifikapo tarehe 30/08/2024 Ujenzi wake uwe umekamilika na ikibidi Mwenye wa uhuru uzindue ameyasema hayo kiongea katika yake siku ya kujitambulisha na kukagua Miradi Wilayani Momba. " Niwaombe sana watu wa Mamlaka ya bonde muhakikishe hili bwawa linakamilika tarehe Mwezi wa nane na ikibidi Mwenge uzindue bwawa hili naomba mkuu wa Wilaya simamia hili" aliagiza Chongolo Katika hatua nyingine Chongolo amewataka Watendaji kuhakikisha miti inapandwa eneo hilo na kuhakikisha wanasimamia mpaka inakuwa.Chongolo ameanza ziara ya siku mbili Wilayani Momba

RPC SENGA AMEMTEMBELEA MSTAAFU WA POLISI NYUMBANI KWAKE MBOZI

Picha
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Agustino Senga akiwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Mkisi, ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Shule ya Polisi Moshi (CCP) kwa sasa amestaafu utumishi kwa mujibu wa sheria. Kamanda Senga alifika nyumbani kwa Mstaafu huyo Mei 14, 2024 Kata ya Igamba wilayani Mbozi kwa lengo la kumjulia hali ikiwa ni pamoja na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo usalama.

RC CHONGOLO ATOA MAAGIZO YA KUANZA KUTUMIKA STENDI YA MLOWO

Picha
 RC CHONGOLO: HALMASHAURI BORESHENI  MIUNDOMBINU NA VIBANDA STENDI YA MLOWO Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo amefanya ziara katika Halmashauri ya wilaya ya Mbozi ambapo ametembelea na kukagua Ujenzi wa stendi ya Mlowo na ameuagiza uongozi wa Halmashauri  ya Mbozi kufanya maboresho ya miundombinu pamoja na vibanda vya biashara katika stendi ya Mji Mdogo wa Mlowo Mhe. Chongolo ametoa maagizo hayo  Jummanne Mei 14, 2024 wakati wa mkutano na wamiliki wa vyumba vya biashara katika stendi hiyo. Katika Mkutano huo makubaliano na wafanyabiashara hao yaliofikiwa ni pamoja na wafanyabiashara kurudi ndani ya stendi ya mabasi pamoja na mabasi kuingia ndani ya stendi. Pia vyumba vya biashara vyote vya mbele kuunganishwa kutokana na udogo wa vyumba hivyo ambapo vyumba viwili vitatoa chumba kimoja. Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa Siku ya Ijumaa atashiriki kikao kitakachohusu uunganishaji wa vyumba hivyo. Aidha, RC Chongolo amepiga marufuku ujenzi holela ambao haufuati ta...