POLISI SONGWE WAOMBA USHIRIKIANO NA WANANCHI KUTOKOMEZA USHOGA NA UKATILI
Tunduma. Wananchi wa Mkoa wa Songwe wametakiwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kutokomeza vitendo vya ukatili, rushwa na ushoga vinavyoibuka katika jamii. Rai hiyo imetolewa leo Jumapili Aprili 30, 2023 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Theopista Mallya wakati wa ziara yake aliyoifanya katika ibada katika makanisa mawili mijini Tunduma. Kamanda Theopista amehudhuria ibada katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) uaharika wa Tunduma na Kanisa House of Prayers lililopo pia mjini humo. Akizungumza katika ibada hiyo, RPC huyo amesema vitendo vya ukatili ikiwemo ukatili dhidi ya watoto, ushoga vimeshamiri katika jamii hivyo viongozi wa dini hawanabudi kukemea vitendo hivyo. "Naomba tushirikiane sisi polisi na ninyi ili tuweze kuutokomeza, jambo la kwanza ni ukatili uliokidhiri katika jamii" amesema Amesema kuwa kuna aina mbalimbali za ukatili unaofanyika katika jamii ikiwemo vipigo, ubakaji, ulawiti na matusi, unyanyasaji na