MRADI WA ELIMU VIJANA CHANGAMANI (IPOSA) WAZINDULIWA ILEJE
Mradi wa Elimu ya Vijana Changamani(IPOSA) wenye thamani ya Zaidi ya Shilingi milioni 85 umezinduliwa rasmi wilayani Ileje mkoani Songwe huku matarajio ya kuwainua vijana kiuchumi ukiwa ni moja ya malengo makubwa. Akizungumza na baadhi ya wakuu wa idara na vitengo na baadhi ya madiwani waliohudhuria uzinduzi wa mradi huo Mei 29,2023 uliofadhiliwa na UNCEF mkuu wa wilaya ya Ileje Mhe. Farida Mgomi amesema mradi huo umekuja kwa mda mwafaka wakati dhamira ni kuhakikisha vijana wananufaika kiuchumi. Mhe. Mgomi amesema mradi huo unatarajia kuwasaidia vijana walioshindwa kumaliza masomo au kuendelea na masomo ya sekondari na msingi kwa kuwasidia kupata elimu ya ufundi katika shule maalumu ambayo itanzishwa katka kata ya Chitete wilayani humo. Mhe.Mgomi amesema lengo la mradi ni kuwasidia vijana kutoka mtaani,waliopata mimba za utotoni,ndoa za utotoni kupata ujuzi wa ufundi na hatimaye kuanzisha vikundi na viwanda vidogovidogo kupitia mradi huu Kwa lengo la kupunguza vijana tegemezi. Hi