MKURUGENZI TUNDUMA ATANGAZA MIKAKATI ZAIDI KUINUA MAPATO YA NDANI.
HALMASHAURI ya Mji Tunduma, Wilaya ya Momba, Mkoani Songwe ipo kwenye mchakato wa kufanya upanuzi wa Maegesho (Truck’s Parking) ya magari makubwa yanayovuka mpaka wa Tanzania na Zambia, kutoka magari 120 hadi malori 300 kwa lengo la kusisimua na kuiongezea Halmashauri hiyo mapato yake ya ndani. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Philemon Magesa, katika mahojiano maalum na gazeti hili yaliyolenga kupata taarifa zinazohusiana na utekelezaji wa mikakati ya ukusanyaji wa mapato ya ndani na kusababisha mapato hayo kuongezeka mara dufu. Moja ya Malori ya Mizigo likiingia kupaki katika maegesho ya Halmashauri ya Tunduma. Halmashauri ya Mji Tunduma imeongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali, ikiwemo miradi ya kimkakati na kufikia kiasi cha shilingi bilioni 13.7 kwa mwaka. Akifafanua zaidi kuhusu utekelezaji wa mradi huo wa upanuzi wa maegesho ya magari makubwa yanayovuka Mpaka wa Tanzania na Zambia (Truck’s Parking), Mkur