SAKATA LA VOCHA KUPANDA SONGWE TCRA WAPEWA MAAGIZO NA WAZIRI
Bei ya vocha za simu za kukwangua zimepanda nchini kutoka Sh1,000 hadi Sh1,200 huku Serikali ikiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhakikisha watoa huduma hawapandishi bei kiholela. Akiuliza swali la nyongeza bungeni leo Mei 29, 2024, Mbunge wa Viti Maalumu, Tunza Malapo amehoji ni nini kauli ya Serikali kuhusu kupanda kwa bei ya vocha za kukwangua kwa kuwa zimepanda kutoka Sh1,000 hadi Sh1200. “Vocha iliyokuwa inauzwa Sh500 sasa ni Sh600. Nataka kauli ya Serikali kwa sababu wananchi hawaelewi,”amehoji. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Maryprisca Mahundi amesema jambo hilo limejitokeza katika maeneo mbalimbali ikiwemo Tunduma, Mbozi na Songwe. “Waheshimiwa wabunge wamekuwa wakilifuatilia na sisi tumefuatilia na kuagiza TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania), wahakikishe watoa huduma hawapandishi bei kiholela lazima wafuate utaratibu,”amesema. Katika swali la msingi, Malapo amehoji ni lini tatizo la mawasiliano ya simu kwa baa