MABILIONI YA RAIS SAMIA ILEJE KUFUNGUA FURSA ZA KIUCHUMI,KUJENGEWA BARABARA ZA KISASA TOKA UHURU
WANANCHI wilayani Ileje mkoani Songwe,wameiharakisha wizara ya ujenzi kupitia wakala wa barabara nchini (Tanroads) mkoani Songwe kuongeza jitihada za kuhakikisha barabara zinakamilika kabla ya msimu wa mvua kuanza ili kukwepa kutopitika kwa barabara hizo kutokana na uwepo wa tope na mashimo. Wilaya ya Ileje ni moja ya wilaya kongwe nchini ikikabiriwa na changamoto nyingi ikiwemo ubovu wa barabara ambazo nyingi ni za vumbi zinazoharibika na kutopitika wakati wa mvua za masika hali inayopelekea kutumia njia za uchochoroni kupita kwenda kupata huduma upande wa pili ikiwemo makao makuu ya wilaya. Kwa muda mrefu wilaya hiyo imekuwa ikikabiriwa na changamoto hiyo,na kusababisha baadhi ya watumishi miaka ya nyuma wanapopangiwa kazi Ileje wakiacha kazi wakiona kama kufanya kazi wilayani humo ni kama adhabu lakini kwa sasa kumekuwa na mabadiriko makubwa. Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti jana wakazi wa wilaya hiyo,walisema kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia barabara zisizokuwa na hadhi kut