Posts

Showing posts from November, 2022

MAMA AFARIKI KWA MOTO NA WANAE

Image
  Watu watatu wamefariki dunia wakiwa ndani ya nyuma baada ya kuungua moto usiku wa kuamkia leo Jumatano, Novemba 30, 2022 wilayani Kahama mkoani Shinyaga wakati wakiwa wamelala nyumbani kwao huku chanzo cha moto huo kikiwa hakijajulikana. Tukio hilo limethibitishwa na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga na kuwataja waliopoteza maisha ni pamoja na Dotto Juma (32) ambaye ni mama mzazi na watoto wake, Samsom Mathew (13) na Joseph Samson (9) Kiswaga amesema tukio hilo limetokea alfajiri wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao, moto huo uliwaka na kuwaunguza hali iliyosababisha kupoteza maisha huku Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likifanikiwa kuuzima moto huo. Amesema waliopoteza maisha ni mama yao mzazi na watoto wake wawili waliokuwa wanasoma shule ya msingi Athony wa Padua, darasa la pili na la sita na kuiomba familia hiyo kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea na uchunguzi. Nao baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo akiwemo mwenyekiti wa Nzengo ya Miemben

IGP AHUKUMIWA MIEZI 3 JELA

Image
  Mahakama kuu nchini Nigeria imemhukumu mkuu wa polisi nchini humo kifungo cha miezi mitatu kwa kutotii amri ya mahakama. Uamuzi huo ulifuatia kesi ya afisa wa polisi ambaye alifutwa kazi mwaka 1992. Afisa huyo alipinga kustaafu kwake kwa kulazimishwa, na kuachishwa kwake kazi baadaye kulikataliwa kortini. Mahakama iligundua kuwa Inspekta Jenerali Usman Alkali Baba anafaa kutumikia kifungo cha miezi mitatu, atamrejesha kazini afisa huyo wa polisi. sasa jeshi la polisi limeshindwa kutekeleza agizo hilo. Katika taarifa, msemaji wa polisi Olumuyiwa Adejobi alielezea huo kuwa “wa kushangaza”.  Alisema jeshi la polisi linasoma hukumu hiyo ili kujua hatua za kuchukua. “Inafundisha kutambua kwamba kesi hiyo inamhusu afisa ambaye alifukuzwa kazi tangu 1992, miaka michache baada ya IGP wa sasa kujiunga na Jeshi la Polisi la Nigeria,” alisema. Aliongeza kuwa “hukumu ya hivi majuzi zaidi juu ya suala lilitolewa mnamo 2011 ambalo linasema kuwa chini ya matumizi hayo ya sasa wa jeshi”.

Daktari ajinyonga akijiandaa kutoa mahari

Image
  Muktasari: Moyo wa mtu kichaka, ndivyo unavyoweza kusema unaposimuliwa tukio la Dk Joseph Ngonyani kudaiwa kujinyonga kwa kutumia shuka akiwa nyumbani kwake kitongoji cha Saghana na kuacha simanzi na vilio kwa ndugu na majirani. Moshi. Moyo wa mtu kichaka, ndivyo unavyoweza kusema unaposimuliwa tukio la Dk Joseph Ngonyani kudaiwa kujinyonga kwa kutumia shuka akiwa nyumbani kwake kitongoji cha Saghana na kuacha simanzi na vilio kwa ndugu na majirani. Ngonyani aliyekuwa mfanyakazi wa zahanati ya Saghana iliyopo nje kidogo ya mji wa Himo Kata ya Makuyuni wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro, anadaiwa kujinyonga Jumamosi Novemba 26, 2022, siku ambayo ilikuwa ni ya kupeleka mahari ukweni na ikiwa umebaki mwezi mmoja kabla ya siku ya harusi yake Desemba 28. Inaelezwa kuwa muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kuelekea ukweni kutoa mahari, aliwaambia aliokuwa aambatane nao, watangulie na yeye angewafuata, lakini kadiri muda ulivyokuwa ukienda na wao kukaribia ukweni, wakaanza kumpigia simu, amb

RAS SENEDA AGEUKA MBOGO KITUO CHA AFYA KUTOKUWA NA MPANGO MATUMIZI YA DAWA.

Image
  RAS SENEDA AGEUKA MBOGO KITUO CHA AFYA KUTOKUWA NA MPANGO MATUMIZI YA DAWA. Na Rahimu Secha,Songwe KATIBU tawala mkoani Songwe,Happines Seneda,amechukizwa na kitendo cha kutokuwepo kwa mpango mzuri wa upokeaji na utoaji wa dawa kwa wagonjwa katika kituo cha afya Ileza kata ya Magamga wilayani Songwe mkoani hapa. Seneda aliyesema hayo juzi alipotembelea kituo hicho kujua hali ya uamilifu wa ujenzi majengo mapya pamoja na huduma za matibabu zilizoanza kutolewa ambapo alishikwa na butwaa kuona baadhi ya madudu hasa katika ukosefu wa taarifa za utoaji wa dawa kwa wagonjwa. Kata ya Magamba iliyopo pembezoni mwa wilaya hiyo,ikiwa na zaidi ya wakazi 17.400 ambapo awali wananchi hao walikuwa wakitembea kulometa 18 kupata huduma za afya makao makuu ya wilaya yaliyopo kata ya Mkwajuni. Sophia Mwashilindi,mkazi wa kijiji cha ileza alisema kituo hicho kimeanza kazi ya kutoa huduma na wao kuondokana na kadhia ya kutembea umbali huo wa zaidi ya kilometa 18 ambapo pia walilazimika kwenda kupata tib

MADARASA YA GHOROFA TUNDUMA YATAJWA KUPUNGUZA MSONGAMANO NA KUONGEZA UFAURU KWA WANAFUNZI

Image
Na Rahimu Secha,Tunduma UPUNGUFU wa madarasa katika halmashauri ya mji Tunduma umetajwa kumalizika baada ya ujio wa madarasa yanayo jengwa kwa mtindo wa Ghorofa hali iliyotajwa kuondoa msongamano uliopelekea wanafunzi kushindwa kusoma vizuri. Halmashauri ya mji Tunduma ipo Wilaya ya Momba ambayo ilimegwa kutoka wilaya ya Mbozi miaka ya hivi karibuni huku ikikabiriwa na changamoto nyingi ikiwemo mlundikano wa wanafunzi darasani ambapo kwa wastani darasa moja limekuwa na Zaidi ya wanafunzi 200. Kutokana na msongamano huo,halmashauri ya mji Tunduma kupitia vikao vyao walipendekeza kuanza kujenga shule kwa mfumo wa Maghorofa ili kuendana na uhaba wa maeneo kutokana na mji huo ambao ni wa kibiashara kuingiwa na watu wengi ambao wamekuwa wakifuata fursa za kibiashara. Zephania Mgola mkuu wa shule ya sekondari Uwanjani,alisema ili kukabiliana na changhamoto hiyo mwezi Disemba 28 2021 walipokea Tsh,470,000,000  kutoka serikali kuu kupitia Program ya SEQUIP kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya

UJENZI WILAYAÑI SONGWE MATUNDU 15 YA VYOO SHULE YA MSINGI MWAMBANI

Image
Na Rahimu Secha,Songwe KUTOKANA na uwepo wa changamoto ya ukosefu wa matundu bora ya vyoo kwenye shule ya msingi Mwambani iliyopo wilayani Songwe mkoani hapa,hatimaye halmashauri ya wilaya hiyo imejenga matundu 15 yenye thamani ya Milioni 26,085.56. kwa ajili ya kunusuru wanafunzi na hadha ya kujisitili. Hayo yalibainika leo wakati wa ziara ya kikazi iliyofanywa na katibu tawala mkoani humo akiwa na timu yake ya wataalam ambapo katika wilaya hiyo,ambapo akiwa katika shule hiyo aliweza kuyakagua matundu hayo ya vyoo na kuridhika na ujenzi. Shule ya msingi Mwambani inawanafunzi 602 wavulana wakiwa 284 kuanzia darasa la awali hadi darasa la saba,ambapo idadi ya matundu ya vyoo yaliyopo ni 12 kati ya hayo matundu 6 ni ya wavulana ambapo shule hiyo imepokea Tsh,Milioni 20,601 kwa ajili ya ujenzi wa matundu 15 ambapo kati ya hayo matundu 7 ni ya wavulana. Akizungumza leo (jana) kwenye ukaguzi huo,afisa elimu msingi wilayani humo,Michael Nzunda,alisema fedha ilipokelewa tarehe 15 Juni 2021 ki

MIL,300 ZA SERIKALI KUU ZIMETUMIKA KUJENGA NYUMBA YA MKURUGENZI WILAYA YA SONGWE

Image
Na Rahim Secha,Songwe ILI kuhakikisha tatizo la nyumba za watumishi lina malizika serikali imetoa Ths,Milioni 300.000.000. kujenga nyumba ya kurugenzi katika halmashauri ya wilaya ya Songwe mkoani hapa hali itakayopunguza tatizo la nyumba za watumishi. Wilaya ya Songwe ni moja ya halmashauri mpya mkoani songwe iliyomegwa kutoka wilayani Chunya mkoani Mbeya miaka kadhaa iliyopita ikiwa na changamoto nyingi kutokana na upya wake hasa uhaba wa nyumba za watumishi. Uhaba huo wa nyumba za watumishi umeanza kufanyiwa kazi baada ya serikali kuu kutoa kiasi hicho cha Tsh,Milioni 300,kujenga nyumba ya mkurugenzi ambapo nyumba zingine za watumishi zikiwa zinaendelea kujengwa hali inayochochea hamasa ya utendaji kazi kwa watumishi wa halmashauri hiyo. Mzee Ayoub Mwashilindi mkazi wa Mkwajuni alisema yeye ni mzaliwa wa wilaya hiyo tangu ikiwa sehemu ya Mbeya,kulikuwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa ofisi na nyumba za watumishi,lakini kwa awamu hii alisema ameona kasi ya ujenzi wa miradi mbalimba

MILIONI 90 ZA SERIKALI YA MAMA RAIS SAMIA ZIMETUMIKA KUJENGA VYUMBA VIWILI VYA MAABARA SHULE YA SEKONDARI SUME -SONGWE

Image
Na Rahimu Secha,Songwe WANANCHI wa vijiji vilivyopo kata ya Mkwajuni wilayani Songwe mkoani hapo wameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suruhu kwa kutoa kiasi cha Milioni 90kujenga nyumba viwili vya maabara Pamoja na thamani zake hali itakayosaidia wanafunzi kujifunza masomo kwa vitendo. Awali shule hiyo ilikuwa haina maabara hali iliyowapa changamoto wananfunzi kujifunza kwa vitendo hasa masomo ya fizikia na sayansi ambapo kwa sasa changamoto hiyo imetimizwa baaada ya serikali kusikia kilio cha wananchi. Mayasa Msafiri mkazi wa Mkwajuni,alisema licha ya wao kuwa na muamko wa kuwapeleka shule Watoto wao lakini walikuwa wakikabiliwa na ukosefu wa maabara ambapo kwa sasa ujenzi wa maabara za kisasa zipo hatua za mwisho huku akiwa na uhakika wanafunzi wataongeza ujuzi mara dufu kwa vitendo. Hayo yalifanyika leo katika ziara ya kikazi ya katibu tawala mkoani Songwe akiwa wilayani humo ambaye alizungumza masuala mbalimbali ya kielimu na kuwataka wazazi kuwapeleka Watoto

JOYCE MWAZEMBE; MLEMAVU ANAYETEMBEA KWA KUTAMBAA , MWENYE NDOTO ZA KUSAIDIA WALEMAVU, YATIMA NA WASIOJIWEZA

Image
Na Baraka Messa "NILIANZA na mtaji wa shilingi 18,000 ambao nilipata baada ya mama angu mzazi kwenda kuniuzia mnadani Vwawa viazi vichache nilivyovivuna  ambavyo nililima nyumban. Mama alipo Rudi na kunikabidhi hela aliyoniuzia viazi nilifurahi sana, nilinunua karanga za maganda debe tatu nikazimenya nikapata debe moja la zilizomenywa nilipoliuza nilipata shilingi 21,000 niliendelea na biashara Hiyo ya karanga baadae mtaji ulivoongezeka nilianza kununua samaki" anasimulia Joyce Alan Mwazembe  (36) ambaye ni Mlemavu wa miguu anayepata mahitaji yake kwa kutambaa . Joyce ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Sumbaluwela Kata ya Ihanda Wilaya ya Mbozi anasema ulemavu alionao hakuzaliwa nao bali aliupata akiwa na umri wa miaka 15 akiwa darasa la tano katika shule ya Msingi Sumbaluwela. Akiongea na mwandishi wa makala haya aliyemtembelea Kijijini hapo,  anasema ulemavu wake aliupata baada kudondoka kwenye mti wakati akijaribu  kuchuma matunda aina ya  parachichi, ambapo anadai kuwa alipo d

IPUNGA BARABARA YA KILOMETA 50 KUUNGANISHA MBOZI NA MOMBA KUPITIA MSANGANO,KAMSAMBA YATAJWA KUONGEZA FURSA ZA KIUCHUMI

Image
  Na Rahim Secha,Mbozi WANANCHI wa vitongoji 21 wa kata ya Ipunga wilayani Mbozi mkoani Songwe wameanza kupata manufaa ya kiuchumi baada ya wafanyabiashara ya mazao yakiwemo mahindi kutoka nchi za Zambia,Malawi na Kenya kufika na magari katika mashamba yao kununua nafaka hizo kutokana na uwepo wa barabara nzuri inayochecheo mnyororo huo. Wakizungumza jana na gazeti hili wakazi wa eneo hilo walisema wao asilimia 80 ni wakulima wa mazao mbalimbali miaka zaidi ya kumi wanunuzi wamekuwa wakinunua mazao yao kwa bei ya kilanguzi kutokana na wafanyabiashara wakubwa kushindwa kufika kutokana na uwepo wa barabara mbovu. Antson Simbeye mkazi wa Ipunga alisema barabara ya kutoka Mlowo kwenda Kamsamba inaumuhimu mkubwa kwani bidhaa nyingi zinazotoka wilaya ya Momba inapita katika njia hiyo kwenda makao makuu ya mkoa na hata mikoa mingine hivyo serikali imefanya kazi nzuri kuijenga licha ya kuwa bado haijawekwa lami. Juhudi Siyame mkazi Vwawa,alisema Serikali kupitia wakala wa barabara mijini (Tanr

JINSI YA KUPIKA BIRIANI YA KUKU

Image
 birian ya kuku. mahitaji. kuku maziwa mala/mtindi pilpil manga nzima bizar nyembamba mdalasin, hoho tangawiz na saum kitunguu kikate ukikaange viaz  menya uviweke rangi kisha vikaange tomato na paste  rangi  ichnganye n maji kidogo. chumvi  mchele uchemshe uumwage maji.  katika blenda weka tangawiz, saum, tomato, paste, mtindi, spices, hoho saga vyote pamoja kisha weka. kwenye sufuria  pamoja na kuku. weka. moton acha vichemke rojo likianza kupungua kias wwka viaz, chimvi na vitunguu acha viive pamoja mpaka liwezito. chukua mchele urudishe sufurian. baad kuuchemsh weka rangi kias upendacho    kisha weka vitunguu sio lazima funika acha kwa mda wa dakika 15 mpk 30 moto mdogo mdogo ili wali uive vizur.. epua koroga uchanganyike vizur kisha serve n enjoy

BREKING NEWS: RADWELL MWAMPASHI ASHINDA UENYEKITI MKOA WA SONGWE

Image
 Uchaguzi wa nafasi ya Uenyekiti Mkoa wa Songwe umefanyika katika Ukumbi wa Kanisa la Morovian na haya ndio matokeo yake Radwell Mwampashi- 415  Kisa Kibona-104 Isabela  Mbaya- 27 Matokeo ya Uchaguzi nafasi ya Ujumbe Halmashauri kuu Taifa Mkoa wa Songwe Aden Mwankyonde-328 Ombeni Nanyalo- 211   Uchaguzi huo ambao ulirudiwa kwa mara ya pili baada ya matokeo ya mwanzo Kushindwa kupatikana mshindi  Na matokeo ya awali yalikuwa ifuatavyo Awamu ya kwanza Aden 274 Nanyalo 154 Nsonjo 122

KATIBU TAWALA SONGWE SENEDA AWAPONGEZA JUMUIYA YA KIISLAMU MKOA WA SONGWE KWA WAZO LA KUANZISHA CHUO CHA MAADILI

Image
(Katibu Tawala Mkoa Songwe Happnes Seneda )  Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Hapness Seneda amehudhulia Sherehe ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (Saw) Maulid iliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanawake wa kiisalamu Mkoani Songwe katika msikiti wa Ijumaa wa Noor uliopo Vwawa Wilayani Mbozi. Sherehe hiyo iliofanana kwa kaswida na usomaji fasaha wa Quruani ilienda sambamba na Nia ya kuanzishwa cha Chuo cha mafundisho ya Dini na maadili (Madrasa) Ili kuweza kutoa mafunzo Kwa Watoto wa kiisalamu pamoja na dini zingine. (Wanawake wa Kiisalamu Songwe akiimba na Kupiga madufu katika Maulid ilifanya Mbozi) Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiisalamu Mkoani Songwe Bi Tatu Ramadhani amesema Jumuiya hiyo imekuja na wazo la kuanzishwa Chuo hicho Ili kuwafunza Watoto maadili ya Dini na kuwaepesha matendo ovyo ya Dunia na kujenga kizazi chenye hofu na Mungu na Maadili mema. Aidha amesema Chuo hicho kitawafundisha Watoto wote bila Kujali Dini wala jinsia hivyo ameiomba Serikali kuwasaidia kwa hali na mali Ili kuwe

HUYU HAPA MWENYEKITI WA UVCC MKOA WA SONGWE

Image
 Matokeo ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Songwe  Fatuma Husein 164 Baraka Thomas 65 Benard Kijalo 59 Mjumbe Mkutano Mkuu CCM Mkoa Noeli Mtafya 165 Modesta Kimisha 99 Ernest Eligius Mwakenja 14 Alphonce Albert Stima 02 UJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA NA MKUTANO MKUU WA CCM TAIFA       1. Shaibath Kapingu   154.           2. Noel Mtafya 80.       3.Modesta kibisha 40  

PICHA MBAMBALI ZA UCHAGUZI JUMUIYA YA WAZAZI MKOA SONGWE

Image
Picha mbalimbali zikionyesha zoezi zima la upigaji wa kura jumuiya ya Wazazi Mkoa nafasi ya Mwenyekiti ambapo ndugu Rabson Mwaipula ameibuka mshindi akimbwaga bila huruma Mwenyekiti wa zamani Ruth Manongi  

AIR TANZANIA YASHINDWA KUTOA BUKOBA KUTOKANA NA HALI YA HEWA

Image
  Dar es Salaam. Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imeshindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera kutokana na hali mbaya ya hewa. Badala yake ndege hiyo imelazimika kutua salama katika uwanja wa Mwanza Alipoulizwa kwa simu leo Alhamisi Novemba 17 kuhusu tukio hilo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari amethibitisha tukio hilo.   “Ni kweli nimepata taarifa ndege ya Air Tanzania imeshindwa kutua kutokana na hali mbaya ya hewa, kulikuwa na ukungu, mvua, radi na giza uwanja ukawa hauonekani, kwa hiyo rubani akafuta safari na kurudi Mwanza na ametua salama,” amesema. Awali taarifa iliyotumwa na Mbunge wa Viti Maalum, Neema Lugangira kwenye mitandao ya kijamii ilieleza tukio hilo. “Still shaken  lakini Mungu ni Mwema. Nimepanda ndege asubuhi ya leo kwenda Bukoba. Safari ilikuwa na changamoto, tumefika lakini ndege ikashindwa kutua. “Nampongeza rubani kwa uamuzi sahihi wa kurudi Mwanza na sasa narudi Dar. Serikali ibebe kwa uzito suala la airp

SAZA-WILAYANI SONGWE WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUWAJENGEA MIUNDOMBINU YA BARABARA NA TAA ZA BARABARANI

Image
Na Rahim Secha,Songwe WANANCHI wilayani Songwe mkoani hapa, wameipongeza Serikali kupitia wakala wa Barabara nchini (TANRODS) Mkoani Songwe kwa kuwajengea barabara sambamba na uwekaji wa taa eneo la Saza Hali iliyochochea kukua kwa uchumi. Uwekaji wa taa hizo katika eneo la mzunguko (Round About) kumewezesha kata ya Sasa inayokuwa Kwa kasi kiuchumi kutokana na kuwa ni eneo la uchinbaji wa madini ya Dhahabu Hali inayovutia wawekezaji na wajasiliamali kuzidi kuwekeza zaidi. Mussa Rashid dereva wa bajaji kutoka Mkwajuni kwenda Saza, alisema uwekaji wa taa hizo kunefungua mnyororo wa thamani kwani Kwa sasa wanalazimika kufanya kazi ya kubeba abiria hadi saa saba usiku ukilinganisha na awali ambapo walikuwa wakiishia saa moja hadi saa mbili usiku. Albert Lusambo mchoma nyama na mkazi wa Sasa alisema anakila sababu ya kuipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suruhu Kwa kuwajali wananchi wake na kwamba wanalazi mika kufanya biashara hadi saa nane usiku wakitumia mwanga wa taa

ADEM KUANDAA MODULI YA MAFUNZO YA MASAFA MAREFU

Image
 Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (Adem), unandaa moduli kwa ajili ya kutoa mafunzo ya masafa marefu, lengo likiwa ni kuwezesha viongozi wa sekta ya elimu wanaopata changamoto ya ruhusa kazini kupata mafunzo. Hayo yamesemwa leo, Jumanne Novemba 15, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa Adem, Dk Siston Mgullah wakati akielezea majukumu ya wakala huu na vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha 2022/23. Dk Mgullah amesema kwa sasa wanamradi na Chuo cha Mzumbe kwa ajili ya kuandaa moduli za kuendeshea mafunzo ya masafa, ambapo wameshafika mahali pazuri “Programu tuliyonayo ni kuanza mafunzo ya masafa kwa namna tofauti, tunaweza tusiende kama Open University (Chuo Kikuu Huria) kinavyofanya ndio maana tunashirikiana pia na Aghakhan University (Chuo Kikuu cha Aghakhan) ambao wako advance (wako juu) katika suala hilo,” amesema. Amesema lengo ni kushirikisha taasisi hizo na kutafuta raslimali zitakazowawezesha kutengeneza mifumo hiyo. Aidha, amesema wana mkakati wa kuanzisha masomo ya jioni katika mikoa

BREAKING NEWS: KOCHA SIMBA AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA NA WENGINEWAPO 11

Image
  Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya miongoni mwao akiwa ni Kocha wa Makipa wa Simba Muharami Mohamed ‘Shilton’.   Hayo yameelezwa leo Novemba 15, 2022 na Kamishna Jenerali wa DCEA, Gerald Kusaya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.   Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mamlaka hiyo imesema iliendesha Operesheni katika maeneo mbali mbali ya nchini na kukamata Jumla ya Kilo 34.89 za dawa za kulevya aina heroin pamoja na kukamata biscut 50 zilizotengenezwa kwa kutumia dawa za kulevya aina ya Bangi kama moja ya Malighafi.   Mtuhumiwa mwingine miongoni mwa hao waliokamatwa ni Kambi Zubeir Seif ambaye ni Mfanyabishara na Mmiliki wa Kituo cha Michezo cha Cambiasso kilichopo Tuangoma, Kigamboni Dar es Salaam.

AMUUA MDOGO WAKE KWA KUMKATAKATA NA MAPANGA

Image
 Jeshi la Polisi mkoa Kilimanjaro, linamshikilia mkazi wa kijiji cha Kilema Chini wilaya ya Moshi mwenye umri wa miaka 47 kwa tuhuma za kumuua ndugu yake Gasper Mbuya (36) kwa kumkata kwa kitu chenye ncha kali. Ingawa Jeshi hilo halijaweka wazi aina ya silaha iliyotumika katika mauaji hayo, lakini taarifa kutoka katika eneo la tukio zinadai mtuhumiwa alitumia panga kumuua ndugu yake Kamanda wa Polisi , Simon Maigwa, amesema, Jumamosi ya Novemba 12, 2022 saa 4 asubuhi, Jeshi hilo lilipokea taarifa za kuuawa kwa mtu huyo na mwili wake kuwekwa kwenye shimo jirani na nyumba wanayoishi wawili hao. Kulingana na taarifa hiyo, marehemu aliuawa Novemba 6, 2022 na kwamba mwili wake uligunduliwa jana Jumamosi Novemba 12, 2022 saa 4 asubuhi huku ukiwa umekatwakatwa sehemu mbalimbali za mwili na baadhi ya viungo kutenganishwa kabisa na mwili. Kwa mujibu wa Kamanda Maigwa, kiini cha mauaji hayo bado hakijafamika ingawa mtuhumiwa alikiri kuhusika na upelelezi wa tukio hilo unakamishwa na Jeshi hilo n

VIONGOZI WA SERIKALI 4 WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI,WANANCHI 27 WASAKWA TANGA

Image
 Jeshi la Polisi limewakamata viongozi wanne wa Serikali wilayani Handeni mkoani Tanga kwa tuhuma za kuuza ardhi ekari zaidi ya 500 na mbao 1,000 kinyume na utaratibu. Viongozi hao wamekamatwa leo Jumapili Novemba 13, 20 kufuatia agizo la Mkuu wa mkoa wa Tanga, Omary Mgumba Mgumba ametoa agizo hilo akiwa kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kwamsisi kusikiliza kero za wananchi ambapo amesema viongozi hao wametumia vibaya madaraka yao. Pia, mkuu huyo wa mkoa ameagiza kukamatwa wananchi 27 ambao wapo kwenye orodha ya kudai kununua mashamba lakini hawako kihalali ila wametengenezwa na viongozi. Viongozi waliokamatwa ni Mtendaji wa Kata ya Kwamsisi, Eric Chipindula, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kwedikabu, Rajabu Makamba, Mtendaji wa Kijiji hicho Zahara Sempule na Ofisa Misitu wa wilaya Elinihaki Mdee. "Takukuru fuatilieni hili suala lakini polisi kamateni hawa viongozi wote na wapelekwe ndani kwaajili ya mahojiano zaidi kwani wameshindwa kutumia vizuri nafasi zao", amesema Mku

BREAKING NEWS CCM YATOA MAJINA YA WAGOMBEA TAIFA YA

Image
 

RPC RUKWA-VITENDO VYA ULAWITI VINAZIDI KUONGEZEKA

Image
Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa limewataka wananachi kukemea na kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya Ulawaiti ambavyo vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku na kuwasababishia watoto madhara makubwa ya kiafya hali itakayosaidia kulinda Afya za watoto  na kukuza maadili kwa jamii. Kamanda Theopista Mallya amefika Katika kanisa la Waadventista wasabato siku ya jumamosi lililopo mjini Sumbawanga na kutoa elimu kwa waaumi wa kanisa hilo kutoa ushirikiano Katika kukemea tabia zisizofaa Katika jamii. Baadh ya waumini wamesema wazazi wamekuwa wakipuuzia  wajibu wao Katika kulinda na kutunza familia zao na kutoa wito kwa serikalia kuendelea kuweka mikakati ya kutoa elimu zaidi kwa jamii.

LATRA SONGWE:ZAIDI YA DALADALA 5O SONGWE ZANASWA NA KUTOZWA FAINI KWA MAKOSA YA KUTOZA NAULI NJE YA UTARATIBU

Image
Mamlaka ya udhibiti wa usafili ardhini (LATRA) mkoani Songwe imewataka madereva kutii agizo la serikali kwa kufuata sheria zilizoweka za utozaji wa nauli elekezi kwa kuacha kuwatoza wananchi nauli kubwa kinyume na maelekezo ya serikali. Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake,Afisa mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri aridhini (LATRA) Joseph Bulongo alisema ofisi yake imejipanga kuhakikisha inatoa elimu za mara kwa mara kwa madereva hao ili wazingatia sheria. Alisema kumekuwa na kawaida kwa baadhi ya madereva wanaokiuka taratibu hizo na kutoza fedha za nauli nje ya utaratibu uliowekwa kwa kisingizio cha kupanda kwa mafuta na kwamba kwa atakaye kiuka utataribu huo atatozwa faini ya Tsh,250,000. Alisema nauli elekezi kutoka Mbeya hadi Tunduma ni Tshs 4500,Mlowo kwenda Vwawa Tsh,500,Mlowo Mpemba Tsh,1500,Vwawa kwenda Mpemba Tsh,1000,Mpemba kwenda Tunduma Tsh,500 na kituo hadi kituo ni Tsh,500 mwanafunzi analipa Tsh,200 na kwa upande wa bajaji alisema makubaliano ya naul

PICHA MBALIMBALI ZA MAANDALIZI YA MAZISHI YA DKT ALICE SIMWINGA

Image
Picha mbalimbali za maandalizi ya Mazishi ya Dkt Alice Simwinga aliefariki Kwa ajali ya Ndege Bukoba. Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya kesho (Jumatano) Kijiji kwao Mbimba Wilayani Mbozi.