Posts

Showing posts from January, 2024

Wanne mbaroni tuhuma za mauaji

Image
MWANZA:  Watu wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza Januari 31, 2024 na kusomewa shtaka la mauaji ya watu wawili katika kesi namba 2536 ya mwaka 2024. Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo ,John Jagadi mwendesha mashtaka, mkaguzi wa Polisi Juma Kiparo amewataja kwa majina washtakiwa hao kuwa ni Michael Kanzaga ( 19), Malimi Lutema ( 42), Juma Bupilipili ( 32 ) na Kulwa Wangale ( 43 ) wote wakazi wa kijiji cha Malemve wilayani Kwimba. Kiparo ameiambia mahakama hiyo kuwa washtakiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo Januari 11, 2024 huko wilayani Kwimba kwa kumuua Yusuph Mosha (33) mkazi wa Nyamhongoro na Galila Lutobeka (30) Dereva bodaboda na mkazi Nyamhongoro kwa kuwapiga mawe na kuwachoma moto wakiwatuhumu kwa wizi wa kuku kinyume na kifungu namba 196 na 197 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo ya mwaka 2022. Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlak

ZANZIBAR YA PIGA MARUFUKU MASAI KUTEMBEA NA SILAHA

Image
 Serikali ya Zanzibar imepiga marufuku wamasi kutembea na silaha za jadi mitaani kwa kile ilchosema kuwa ni kuhatarisha maisha ya watu na ni kinyume cha utamaduni visiwani humo. Katazo hilo limekuja baada ya video iliyosambaa mtandaoni ikiwaonesha wananchi wa jamii ya Kimasai wakimshambulia mfanyakazi wa halmashauri kwa silaha za jadi walipokuwa wakiendesha operesheni ya kusimamia sheria ndogo ndogo zinazozuia kufanya biashara maeneo ya barabara ya Mji Mkongwe.

MWALIMU MBOZI ADAI KUMTEKA MTOTO NA KUMFICHA CHUMBANI AKIWA AMAFUNIKA MABLANKETI

Image
Mwl, Baraka Mwashiuya mkazi wa kitongoji cha Tazara mamlaka ya mji mdogo wa Mlowo wilayani Mbozi mkoani Songwe,amekamatwa na jeshi la polisi pamoja na mkewe ambaye ni mwalimu wa sekondari ya Msense wakihojiwa kwa tuhuma ya kumficha mtoto wa miaka 8 chumbani… Ibrahim Yassin,Songwe. Akizungumza tukio hilo leo Januari 31/2024 Bibi wa mtoto huyo, Sevelina Lwesye amesema ilikuwa tarehe 29/1/2024 mjukuu wake aitwaye Bradness Kolineli Mwasote (8) hakuonekana nyumbani ndipo walipoanza kumtafuta pasipo mafanikio. Amesema ilipofika jioni waliitaarifu serikali ya kijiji ambao waliungana nao kumtafuta na kufanikiwa pasipo mafanikio lakini walipata taarifa kwa msamalia mwema mmoja akiionesha nyumba ya mwalimu Mwashihuya ndipo walipoitaarifu jeshi la polisi waliofika na kupekuwa chumba kimoja baada ya kingine na kumkuta amefunikwa na branketi 2 pamoja na godoro. Amesema baada ya hapo walimtoa mtoto akiwa amedhoofu kutokana na njaa ya kutokula kwa siku nzima,na kwamba baba wa mtoto huyo ni mchungaji

KONDOMU ZA KIKE ZAZUA GUMZO BARAZA LA MADIWANI ILEJE

Image
  Wataalamu wa afya wilaya ya Ileje mkoani Songwe wameagizwa kuanza kutoa elimu ya matumizi sahihi ya kondomu za kike ili kukabiliana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa na Ukimwi, Na Ibrahim Yassin,Ileje. Agizo hilo limetolewa leo Januari 30,2024 wakati wa kikao cha baraza la madiwani robo ya pili katika halmashauri ya Ileje baada ya kuibuka kwa ajenda ya wanawake wilayani humo kuogopa kutumia kondomu kutokana na ukubwa wake. Mwenyekiti wa kamati ya afya na ukimwi ambaye ni diwani wa kata ya Itale Fahari Mwampashi amesema hofu ya watumiaji wa kondomu hizo wanasema ukubwa ukilinganisha na maumbile yao wakitaka zipunguzwe ukubwa. 'Wanawake wanaogopa kuvaa hizo kondomu wakidai zitabakia ndani na kuhatarisha afya zao, huku wakiomba wataalamu wa afya kupitia ofisi ya mganga mkuu kuwekeza nguvu ya utoaji elimu," amesema Mwampashi. Vema Rungwe diwani viti maalumu amesema matumizi ya kondomu za kike ukubwa wake na uvaaji ni changamoto ,na kwamba hakuna msukumo wa kuzitangaza kwa jamii

AFISA ELIMU KIZIMBANI KWA KUSABABISHA VIFO VYA WATATU

Image
  OFISA Elimu Taaluma Wilaya Kwimba mkoani Mwanza, Samwel Kulinga (44) amefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka manne likiwemo la kuendesha gari kwa mwendokasi, kuwagonga na kuwasababishia vifo watu watatu. Amesomewa mashtaka hayo katika kesi ya trafiki namba 5383/2024, leo Januari 30, 2024, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kwimba, Dastan Ndeko. Akisoma mashtaka hayo wakili wa serikali, Frank Nchanila amesema shtaka lingine linalomkabili afisa elimu huyo ni kuendesha gari bila ya leseni katika barabara ya umma. Wakili Nchanila amesema waliofariki kwa kugongwa na afisa elimu huyo katika ajali iliyotokea Desemba 30, 2023, eneo la Ilamba wilayani Kwimba mkoani humo ni mwendesha baiskeli, Shauri Masasi (62), Robert Matata (35), na Sara Faustine (43). “Mshtakiwa ukiwa unaendesha gari binafsi yenye namba ya usajili T. 374 EEV Toyota Wish kwa mwendokasi uliwagonga watumiaji wengine watatu wa barabara na kuwasababishia vifo kinyume na kifungu namba 40 (1) na 63 (2) (a

DUGANGE ATAJA IDADI YA WATUMISHI WA AFYA WALIOALIWA

Image
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Dkt. Festo Dugange amesema katika miaka mitatu  Serikali ya awamu ya sita  imefanya kazi kubwa  ambapo imeweza  kuajiri watumishi wa kada ya afya 18,418. Aidha, kwa kipindi hicho serikali imegharimu sh.bilioni  195.3 kujenga miundombinu  ya Hospitali za Wilaya 136 na ukarabati wa hospitali kongwe 19. Akizungumza Januari 31, 2014 kwenye uzinduzi  wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya ngazi ya jamii jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri Dugange amesema serikali imejenga vituo vya afya 446  kwa sh.bilioni 718.18, ujenzi wa zahanati  955 kwa gharama ya Sh.bilioni 77. 41, majengo  ya dharura 80, wagonjwa mahututi  28 na nyumba za watumishi 150 kwa gharama ya sh. bilioni 45 ili kuboresha huduma za afya na kutoa huduma bora kwa wananchi. Naibu Waziri Dugange akizungumzia wahudumu wa ngazi ya jamii, amesema ni watu muhimu ndani ya jamii kwa kuwa wao ndio daraja kati ya jamii na vituo vinavyotoa huduma za afya nchini ili wananchi

WATORO MASHULENI MIKONONI MWA POLISI

Image
Mkaguzi kata ya Muriba Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Vitus Ng'itu akiwa shule ya Sekondari Muriba amebaini uwepo wa wanafunzi wengi watoro na kuweka mkakati wa kudhibiti hali hiyo kwa kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi hao Aidha,Mkaguzi huyo amewapatia elimu kuhusu faida za kupata elimu hivyo waache kutoroka.Amesema yeye atakuwa mstari wa mbele kufatilia maudhurio yao na kuhakikisha wanafunzi  watoro wanazingatia masomo kama wenzao na kuwa  mstari ulionyooka. Hata hivyo alitoa  mawasiliano yake ya namba za simu  ili waweze kumpa taarifa za uhalifu na kufichua wahalifu.

MIKOA YA SONGWE,MBEYA,NJOMBE KUWA NA MVUA KUBWA

Image
Mikoa ya Morogoro, Lindi, Iringa, Mtwara, Mbeya, Songwe, Njombe na Ruvuma inatarajiwa kupata Mvua za Juu ya Wastani kuanzia Januari 30, 2024 ikiwa ni siku chache tangu Mikoa ya Dar na Morogoro ikumbwe na Mafuriko Kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Mvua hizo zinaweza kusababisha athari kwenye miundombinu na makazi ikiwemo nyumba kuzungukwa na maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi TMA imewataka Wananchi kuchukua tahadhari na kujiandaa kwa dharura zinazoweza kujitokeza

TAKUKURU YABAINI MADUDU UJENZI WA SHULE

Image
  TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Geita imebaini uwepo wa viashiria vya ubadhilifu na ufujaji wa pesa katika miradi ya ujenzi wa shule tatu zenye jumla ya Sh bilioni 1.47. Miradi hiyo ni shule ya sekondari Nyantorotoro yenye thamani ya Sh milioni 584.2, shule ya msingi Nyantorotoro iliyogharimu Sh milioni 181.6 na shule ya msingi Museveni iliyogharimu Sh milioni 705. Naibu Mkuu wa Takukuru mkoa wa Geita, Azza Mtaita amebainisha hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Geita na kueleza tayari uchunguzi unaendelea kwa hatua za kisheria. “Katika uchunguzi kuna wale watu wamehojiwa, kuna wengine hawajahojiwa, lakini tutatambue tu kwamba tumeanzisha uchunguzi.” Amesema Mtaita. Mtaita ameeleza uchunguzi wa awali unaonyesha katika miradi ya ujenzi wa shule ya msingi na shule ya sekondari Nyantorotoro makosa makubwa ni ukiukwaji wa taratibu za maununuzi. “Hii inapelekea baadhi ya vitendea kazi au malighafi za ujenzi kununuliwa kwa bei ya juu bila kufuata

AKAMATWA NA FUVU LA BINADAMU

Image
 Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma katika kuzuia na kutanzua uhalifu kwa kipindi cha mwezi Januri,2024 tumefanikiwa kuendesha Operesheni, misako na doria mbalimbali maeneo yote ya Mkoa wa Ruvuma ambapo katika misako hiyo tarehe 07.01.2024 katika kijiji cha Nahoro, Kata ya Luegu Wilaya ya Namtumbo tulifanikiwa kumkamata mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la  Dayano Swaum Chowo, (49), Mkazi wa Naholo akiwa na Fuvu lidhaniwalo kuwa la binadamu na vipande vitatu (3) vya ngozi wanyama pori akiwa amevihifadhi ndani ya begi dogo la mgongoni na kuvificha katika nyumba anayoishi. Pia katika Operesheni hiyo tulizoendesha katika Wilaya ya Namtumbo kwa kushirikiana na Askari wa TAWA Kanda ya Kusini tulifanikiwa kukamata watuhumiwa watatu (3) waliotambulika kwa majina ya Jafari Likwata (41), Mkazi wa Minazini, Nicodemus Pius Ngonyani, (60), Mkazi wa Peramiho – Songea na Jafary George Ngesela wakiwa na Nyara za Serikari ambazo ni Meno ya Tembo mazima 18 na vipande 11 wakiwa wameyahifadhi kwenye mfu

DIWANI MWASHITETE AISHAURI MBOZI VYANZO VIPYA VYA MAPATO YA HALMASHAURI

Image
DIWANI wa kata kata ya Halungu katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe,Maarifa Mwashitete (Mchumi) ameshauri halmashauri hiyo kuingiza tozo mpya za bidgaa mbalimbali ikiwemo Miwa na mazao mengine ikiwemo toza za magari stendi ili kuongeza mapato ya halmashauri...anaripoti Ibrahim Yassin,Mbozi. Mwashitete aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa kikao cha baraza la madiwani cha kupitisha makadilio ya bajeti kilichoketi kwenye ukumbu wa halmashauri hiyo. Alisema mwaka uliopita wa 2023-2024 walikusanya Bilioni 4.6 fedha ambayo ni ndogo ukilinganisha na ukubwa wa halmashauri hiyo pamoja na vyanzo vilivyopo hivyo alishauri zao la miwa linalolimwa na kusafirishwa kwenda mikoa mbalimbali nchini ushuru wake uingizwe kwenye chanzo kipya. Alisema mwaka huu wa fedha 2024/2025 wamepitisha makadilio ya kukusanya Bilioni 6.3 na kusema ili kufikisha makusanyo hayo na hata kuvuka lengo la ukusanyaji ni lazima waainishe vyanzo vyote ikiwemo kubuni vyanzo vipya. Diwani huyo mchumi,alivitaj

CHIKOTI AWATANGAZIA KIAMA WAZAZI WASIOWAPELEKA SHULE WATOTO,MSAKO NYUMBA KWA NYUMBA KUANZA

Image
KUTOKANA na idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kusuasua katika halmashauri ya wilaya ya Momba mkoani Songwe,uongozi wa wilaya hiyo umetangaza kuwachukulia hatua wazazi au walezi watakaokwamisha watoto kujiunga na shule walizopangiwa.,,anaripoti Ibrahim Yassin Songwe. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi,leo Januari 28/2024 mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo,Mathew Chikoti amesema bado hali ya watoto kuripoti shule haijawa nzuri hivyo walianza kutoa elimu kupitia mikutano na kila mzazi anajua wajibu wa mtoto kusoma. Amesema baada ya kutoa elimu kwa wazazi hao,wataanza kutembea nyumba kwa nyumba mtaa kwa mtaa hadi mashambani kuwasaka watoto ambao hawajatipoti shule na kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi watakaoshindwa kuwapeleka watoto shule. ‘’Ndugu mwandishi suala la mtoto kwenda shule sio ombi ni lazima,mtoto licha ya kuzaliwa na baba na mama lakini ni wa Serikali hivyo anapaswa kupata haki yake ya kimsingi kwa kwenda shule,serikali imetumi

TANESCO YAWAHITAJI WAKANDARASI WA KIKE

Image
  DAR ES SALAAM: KUTOKANA na uwepo wa ushiriki mdogo wa wahindisi wakike katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), shirika hilo limezindua mpango wa uwezeshaji wa wahandisi wakike( WECDP) kama sehemu ya kuhamisisha masuala ya kijinsia kushiriki katika shughuli za uendelezaji wa miradi ya umeme nchini. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo uliofanyika leo Januari 29,2024, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga amesema kutokana na kuwepo kwa idadi ndogo ya wahandisi wanawake shirika hilo limeamua kuanzisha mkakati maalumu utakao saidia kuwepo kwa wahandisi wengi wakike watakaoajiriwa na kufanya kazi na shirika. Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Seif Shekilagha ameahidi kuwa wizara itaendelea kutoa ushirikiano kwa shirika hilo na kuufanya mradi huo kuwa mfano. Aidha, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof Nelson Boniface aliyemwakilisha makamu wa chuo

WANAFUNZI 8 WALIOKATALIWA WAFAURU GEITA

Image
  WANAFUNZI   wanane waliokataliwa na shule mbalimbali za taasisi binafsi mkoani Geita kutokana na ufaulu mbaya wamegeuka mashujaa baada ya kupata matokeo mazuri katika mtihani wa kidato cha nne 2023. Wanafunzi hao walibahatika kupata nafasi ya usajili wa masomo na kituo cha mtihani katika shule za taasisi ya Royal Family ya mjini Geita mwaka 2022 ambapo wamehitimu na kufaulu vizuri. Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Royal Family ya mjini Geita, Elikana Simon amewaambia waandishi wa habari mara baada ya Baraza la Mtihani la Taifa (NECTA) kutangaza matokeo ya kidato cha nne 2023. Elikana amesema wanafunzi hao walikuwa wamekataliwa na shule tofauti kwa madai ya kuwa na ufaulu mbaya kwenye mitihani ya majaribio lakini shule hiyo ilijidhatiti kuwapokea kwani elimu ni huduma. Amebainisha awali wanafunzi hao walikuwa tisa lakini mmoja hakuhitimu kwa changamoto za kiafya huku nane waliohitimu wanne wamepata daraja la kwanza, watatu daraja la pili na mmoja daraja la tatu. “Kwa hakika watoto wetu w

BREAKING NEWS: SHULE YA ST MARCUS MBEYA WANAFUNZI WOTE WAFAULU KIDATO CHA NNE

Image
Shule ya Sekondari ya St Marcus ilioyopo Iwambi jijini Mbeya imefaulisha wanafunzi wote matokeo kidato Cha nne 2023 na kutekeleza agizo la  Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwa vitendo juu ya kutokemeza ziro na kuondokana na adha ya Wanafunzi kufeli. Jumla ya Wanafunzi 41 wameweza kufaulu kwa kupata  alama daraja kwanza huku wana wanafunzi 20 wakiwa wamepata alama daraja la pili na wanafunzi 3 wamepata daraja na tatu huku kukiwa hakuna daraja la nne wala sifuri. Akiongea nasi Meneja wa shule za St Marcus Lwitiko Mwamundela amesema juhudi utii ndivyo vilivyopelelea shule hiyo kupata alama nzuri za ufaulu na pia amewashukuru Waalimu na wafanyakazi wa shule hizo kwa ushirikiano wanauonyesha shuleni hapo "Kiukweli tunafanya kazi kama timu na kila mtu anajua wajibu wake Waalimu wanajua wajibu wao na wanafunzi wanajua wajibu wao hivyo kwetu inakuwa rahisi kufundisha na wanafunzi kuelewa"alisema Mwamundela. Kwa upande wa mmoja wa Wazazi wenye watoto shuleni hapo Maria Mwaiza amesema hu

SIASA ZA MAJI TAKA ZATAJWA KUSHUSHA MAPATO STENDI YA MLOWO KUTOKA ZAIDI YA 200,000 HADI 80,000

Image
IMEELEZWA kuwa kutokuwepo kwa ubunifu yakinifu ya uboreshaji wa stendi kuu ya Mlowo wilayani Mbozi mkoani Songwe kumetajwa kushusha mapato yatokanayo na ushuru wa magari kutoka zaidi ya  200,000 kwa siku hadi chini ya 80,000  Ibrahim Yassin,Songwe. Hayo yamejitokeza leo Januari 25/2024 kwenye kikao cha baraza la madiwani cha kupitisha makadilio ya bajeti kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo. Akizungumza kwenye kikao hicho,Diwani kata ya Itaka Alani Mgula anasema mwaka 2020/25 halm ashauri ilibuni kujenga stendi kuu Mlowo ambayo kabla hata haikukamilika ilianza kuingiza fedha nyingi kutokana na magari kuingia na kutoka lakini kwa sasa fedha inayoingia ni kidogo mno. Naye diwani kata ya Halungu Maarifa Mwashitete anasema stendi ya Mlowo ni chanzo kikubwa ili iweze kuingiza fedha mara dufu ni bora soko la mnada wa Mwaswala uvunjwe na kuhamishiwa kwenye stendi hiyo ili kuboresha mazingira na ubora wa soko na kuingiza mapato zaidi ya halmashauri. Mkurugenzi mtendaji wa halmashau

DIWANI MBOZI ATAKA SKAVETA YA HALMASHAURI IFUNGWE GPS KUDHIBITI MAPATO

Image
  DIWANI wa kata ya Harungu wilayani Mbozi mkoani Songwe Maarifa Mwashitete,amemshauri mwenyekiti wa halmashauri hiyo George Msyani kufunga mashine ya utambuzi (GPS) ili Skaveta waliyoinunua iweze kugundulika kazi ifanyazo..anaripoti  Ibrahim Yassin,Songwe. Mwashitete ameyasema hayo leo Januari 25/2024 wakati akiwakilisha hoja hiyo kwenye kikao cha baraza la madiwani cha kupitisha bajeti ya mwaka 2023/24 kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo. Amesema halmashauri hiyo ilibuni chanzo cha mapato kununua Skaveta kwa ajili ya kuchimbia mabwawa na kutengeneza barabara ambapo kwa mtu ama kampuni kuikodi kwa siku inalipia Milioni 1 na kwamba kama hakuna usimamizi mzuri inaweza ikafanya kazi siku 6 alafu ikalipwa fedha ya siku 1. ‘’Ndugu mwandishi gari hili linakodishwa,anaweza kulikodi mtu ama kampuni akiwa nje ya wilaya kawaida kwa siku inalipiwa Milioni 1 inaweza ikakaa siku 6 badala ya kulipia Milioni 6 inalipiwa Milioni 1 hivyo ili kudhibiti mapato ni bora lifungwe Control Machi

HOSPITALI YA RUFAA SONGWE YAZINDUA MASHINE YA CT SCAN,RC AIZINDUA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Dkt Francis  Michael, amezindua Mashine mpya ya CT Scan iliyonunuliwa na Wizara ya Afya ikigharimu fedha zaidi ya Tsh.Billion moja kwa ajili ya kusaidia kusogeza huduma za kibingwa katika Hosptiali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe iliyopo Hasamba Wilayani Mbozi. Kwa kiwango kikubwa mashine hiyo inakwenda kutatua adha ya wagonjwa wengi kuhudumiwa/kupimwa magonjwa mbalimbali makubwa badala ya kusafiri kwenda Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Hospitali ya Taifa Mhimbili jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Viongozi na baadhi ya watumishi wa Hospitali hiyo alhamisi hii (Januari 25, 2024), Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt. Francis Michael, amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia na kutoa fedha shilingi Billion 1.4 ambazo zimenunua mashine hiyo ambayo itahudumia wananchi wa ndani na nje ya nchi kutokana na Hospitali hiyo kuwa eneo ambalo ni jirani na mipaka ya nchi za SADC ikiwemo Zambia. Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mk

CCM WAIPONGEZA TANROADS SONGWE KWA KUWAFUNGILIA FURSA WANA MOMBA

Image
Wakala wa Ujenzi wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe, unatumia zaidi ya Shilingi Million mia saba kujenga madaraja mawili katika Tarafa ya Kamsamba ili kuwasaidia wananchi katika shughuli za usafiri na usafirishaji ikiwemo wa mazao. Kwa mujibu wa Meneja wa TANROAD Mkoa wa Songwe Mhandisi Suleiman Bishanga, Daraja la mto Nkana limegharimu fedha zaidi ya Shilingi Million miatano na limekamilika kwa asilimia mia moja. Amesema wananchi kadhaa wameripotiwa kufariki Dunia kwenye Daraja hilo hivyo hatua ya Serikali kujenga Daraja hilo itakuwa mkombozi kwao huku Daraja lingine likigharimu zaidi ya Shilingi Million mbili. Mhandisi Bishanga, ameiambia Kamati ya Siasa kuwa pia Serikali inajenga Daraja lingine lenye gharama ya zaidi ya Shilingi Million mia mbili lengo kubwa ikiwa ni kuhakikisha Barabara inapitika bila shida hasa ikilinganishwa na mpango wa muda mrefu wa kuunganisha Barabara katika maeneo kadhaa ya kutoka ndani ya Jimbo la Momba hadi kwenda katika maeneo ya Wilaya za Mbo

CCM SONGWE YAIPONGEZA RUWASA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI.

Image
Katika kutekeleza kwa vitendo dhana ya kumtua mama ndoo kichwani, Wakala wa Maji Vijijini Wilaya ya Momba Mkoani Songwe unajenga mradi wa Maji wenye thamani ya zaidi ya Shilingi Billion moja katika vijiji vya Isanga na Kakozi na unatarajiwa kukamilika kufikia Juni 24, 2024. Hayo yamethibitika kwenye ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Songwe ambayo inaendelea kuifanya Mkoani humo baada ya kutembelea na kukagua mradi wa Maji Kakozi Isanga ambapo Tank kubwa linajengwa katika kijiji cha Kakozi na Kisima kirefu kilishachimbwa katika kijiji cha Isanga. Akizungumza kwenye ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe Radwell Mwampashi, amempongeza Meneja wa usambazaji Maji Vijijini RUWASA Mkoa wa Songwe Charles Pambe na yule wa Wilaya ya Momba Beatus Katabazi, kwa utekelezaji na usimamizi mzuri wa miradi ya Maji Mkoani humo. Amewataka wakuu wa idara nyingine kuiga mfano kwa RUWASA ambao anasema wanafanya kazi nzuri na kukiuza

KAMATI YA SIASA MKOA WA SONGWE YARIDHISHWA NA USIMAMIZI WA MIRADI WILAYANI SONGWE

Image
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Mkoa wa Songwe imewapongeza viongozi wa Serikali ya Wilaya ya Songwe, Halmashauri, Chama na taasisi za Serikali na ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Songwe kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo. Pongezi hizo zimetolewa leo Jumatatu Januari 22, 2023 na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe, Ndugu Radwel Mwampashi wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Songwe. Akitoa majumuisho ya ziara hiyo, Ndugu  Mwampashi amesema  kuwa miradi waliyoitembelea katika ziara ya sasa imekuwa na mabadiliko makubwa sana. "Miradi ya safari hii imekuwa na mabadiliko makubwa sana katika Wilaya ya Songwe kwa kweli kwa niaba ya kamati ya siasa nawapa 'big up'. Nawapongeza sana. Hakuna mradi ambao umekuwa na kasoro na siku zote Wilaya ya Songwe imekuwa roal modal ya Mkoa wa Songwe. Hongereni sana"

CCM SONGWE YAELEZA UJIO WA MAKONDA IKIJIPANGA KWA MAPOPKEZI

Image
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Songwe, chatangaza ujio wa katibu wa siasa itikadi na mafunzo Taifa Paul Makonda huku kikieleza mipango na mikakati iliyopo huku kikipongeza kazi zilizofanywa na Rais Dkt,Samia..anaripoti Ibrahim Yassin,Songwe. Akizungumza Januari 18/2023 katibu wa siasa itikadi na uenezi (CCM) mkoani humo,Ally Yusuph amesema wanategemea kumpokea kiongozi wao Paul Makonda Februari 6/2024 akitokea mkoani Rukwa ambapo atakuwa na ziara ya siku mbili mkoani humo. Amesema siku hiyo ya tarehe 6 atafanya kikao cha ndani cha viongozi wa chama na baadae atahutubia mkutano katika halmashauri ya mji Tunduma,kuelezea Ilani ya ccm ilivyotekelezwa na mikakati ijayo waliyoipanga. Amesema Januari 7 atafanya mkutano wilaya ya Mbozi katika mji wa Mlowo ikiwa ni pamoja na kuzungumza na kamati ya siasa,halmashauri kuu ccm Mkoa kupitia vikao vya ndani na pia atakaa vikao vya wazee wa kimila, viongozi wa dini na wakuu wa taasisi mbalimbali. Amesema anazungumza haya ikiwa ni jukumu lake la k

WABUNGE NA MADIWANI WASIOWAJIBIKA WAANZA KUSHUGULIKIWA NA CCM MKOA SONGWE

Image
Kutokana na Wadau mbalimbali kuwalalamikia Madiwani na baadhi ya Wabunge Mkoa wa Songwe kutoeleweka shughuli zao wazifanyazo katika kata na Majimbo yao Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Songwe imeanza kutoa semina elekezi kwa Madiwani pamoja na Wabunge lengo likiwa ni kuwakumbusha Majukumu yao na Wajibu wao wa kuwatumikia Wananchi na Chama pia. Akijibu swali la wanahabari aliloulizwa Katibu wa Siasa na Hamasa Mkoa wa Songwe Yusuph Ally juu ya uwepo wa malalamiko kwa baadhi ya madiwani kulalamikiwa ni mzigo kwa Chama na wamekuwa wakijihusisha na migogoro zaidi kuliko kuwatumikia Wananchi na kutekeleza Ilani ya Chama. Akijibu swali hilo  Yusuph Ally alikiri kuwepo kwa manunguniko hayo na Chama Mkoa kimeyasikia na tayari hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja kuwakumbusha Majukumu yao na kuepuka kuingilia Majukumu yasio yao "Katibu wetu wa Mkoa tayari ameanza kuchukua hatua mbali mbali zikiwepo Semina za kuwakumbusha na kuwaelekeza Majukumu yao na kuepuka kuingia Majukum

RAS SONGWE ASHANGAZWA WANAFUNZI ASILIMIA 57 KUTO RIPOTI SHULE,ATOA MAAGIZO KWA UONGOZI WILAYA.

Image
Katibu tawala mkoani Songwe Happiness Seneda ameshangazwa na kitendo cha baadhi ya wazazi kutowapeleka watoto shule kwa kisingizio cha ukosefu wa sare licha ya serikali kuruhusu watoto wavae nguo za nyumbani huku wakiendelea na utaratibu wa kushona sare. Seneda ameyasema hayo Januari 16/2024 wakati wa ziara ya kupitia miradi ya elimu na nyumba ya mkuu wa wilaya kuona namna ujenzi ulipofikia huku akiridhishwa na hatua za ujenzi. Akiwa katika shule mpya ya sekondari  Naming’ong’o iliyojengwa kwa Milioni 583.1 Ras Seneda alishangazwa kuona shule iliyotakiwa kuchukua wanafunzi 78 wa kidato cha kwanza  ni 35 pekee walioripoti huku shule mama ya sekondari Chitete iliyotakiwa wanafunzi 284 waliotipoti ni 78 pekee. ''Katika shule zote za wilaya ya Momba wanafunzi asilimia 57 hawajaripoti waliopo ni asilimia 43 pekee, natoa siku 7 kuhakikisha watoto wote wanaripoti,mzazi atakayekwamisha atachukuliwa hatua,,amesema Seneda. Kutokana na hali hiyo amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashau