Posts

Showing posts from April, 2024

TANROADS SONGWE WAPAMBANA USIKU NA MCHANA KUREJESHA MAWASILIANO BARABARA YA SHIGAMBA NA IBABA ILEJE

Image
 Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha wilayani ileje na kusababisha utelezi, mmomonyoko (landslide) Kupelekea magari kukwama kwa muda katika barabara ya Shigamba kwenda Ibaba hivyo kuwa kero kwa abiria na mizig. Serikali kupitia wizara ya ujenzi na Wakala ya Barabara Mkoa wa songwe wamefanya jitihada za haraka na kunasua magari yote na tayari vifaa vya kurejesha mawasiliano vinaendela kumalizia zoezi la kuireja mawasiliano Aidha, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Meneja wa Mkoa Tanroads mkoa wa Songwe Mhandisi Suleiman Bishanga amemtaka mkandarasi kuongeza magari kwa ajili ya kusomba kifusi ambacho kinahimili hali ya mvua na pia kufanya kazi usiku na mchana ili kukabiliana na hali ya mvua zinazoendelea Meneja amemshukuru Mhe.Dkt Samia S. Hassan  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha za dharura ambazo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kuwezesha kuondoa changamoto za matengenezo ya barabara.  Sambamba na hilo amemshuku Mhe Innocent Bashungwa Waziri wa Ujenzi na Mtendaj

WANANCHI ILEJE WAHOFU KULA PARACHICHI ZA KISASA KUHOFIA NGUVU ZA KIUME

Image
 Diwani wa kata ya Itale Fahari Mwampashe amemueleza Mkuu wa Mkoa wa Songwe  Daniel Chongolo kuwa wananchi wa kata yake wanaogopa kutumia maparachichi  ya kisasa kwa madai kwamba yanapunguza nguvu za kiume. Akiongea katika ziara ya Ukaguzi wa kituo cha Itale Mwampashe amesema kumekuwepo na tetesi  katani  juu ya hayo maparachichi hivyo kumtaka Mkuu wa Mkoa  wataalamu wake kuwapa ufafanuzi juu ya hilo Akijibu Mkuu wa Mkoa Daniel Chongolo amesema kwamba hizo ni tetesi za uongo tu na hayana madhara yoyote na yeye ni mmoja kati ya wakulima wa maparachichi na ameanza miaka mingine  " Niwatoe wasiwasi haya maparachichi msidanganyike kuleni yapo  vizuri na yanaongeza afya na kinga za mwili hizo imani potofu achaneni nazo" alisema Chongolo

MIMBA ZA UTOTO ILEJE ZAMCHEFUA CHONGOLO AWEKA MIKAKATI MIZITO NA POLISI

Image
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo amekemea vikali tabia ya uwepo wa mimba za utotoni hususani wanafunzi katika Wilaya ya Ileje ambapo amesema katika utawala wake hakuna mtu yeyote atakayekwepa mkono wa dola kwa kumpatia mimba mwanafunzi. RC Chongolo ameyasema hayo leo Aprili 28 wakati akiongea na wananchi katika ziara yake eneo la Shule ya Sekondari ya Wasichana (Ileje Girls) iliyopo kijiji cha Ikumbilo Kata ya Chitete wilayani Ileje. "Niwaambie wala hatutaki kusema mengi ambao wao hawawezi kuacha mabinti wadogo wasome, tutawasaidia kwenda kufanya kazi nyingine zitakazofaa zaidi ili wasionane na mabinti kwa miaka 10,20,25 mpaka 30 ili wakirudi watakuwa walimu wazuri." amesema RC Chongolo Mhe. Chongolo anatarajiwa kuendelea na ziara yake kesho kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa ziara yake ya kikazi ya siku 3 ndani ya wilaya hiyo.

RC CHONGOLO APONGEZA UKUSANYAJI MAPATO TRA ILEJE AKIPOKEA CHANGAMOTO.

Image
Serikali imeombwa kukipandisha hadhi kituo cha forodha cha Isongole wilayani Ileje Mkoani Songwe kutoka daraja C kwenda B pamoja na ujenzi wa majengo yenye hadhi mpakani....anaripoti Ibrahim Yassin,Songwe Leo Aprili 28/2024 Afisa mfawidhi kituo cha forodha Isongole katika mpaka wa Tanzania na Malawi Charles Chacha.baada ya mkuu wa Mkoa huo Daniel Chongolo kukaguana kupokea taarifa ya shughuli zinazotekelezwa mpakani hapo. Chacha amesema kutokana na kituo hicho kutokuwa na hadhi ,kwa sasa kinafanya kazi kama pacha na kituo cha forodha chaTunduma mpakani mwa Tanzania na Zambia  Chacha amesema serikali inatakiwa kukipandisha hadhi kituo hicho kimekidhi vigezo vya kuongeza wigo wa ukusabyaji mapato kutoka Sh 7.8 milioni mwaka 2019 mpaka kufikia zaidi ya Sh 400 mwaka 2024 licha ya mpaka huo kuwa na vipenyo vinavyopelekea mapato mengi kupotea. Amesema mpaka huo unapitisha bidhaa mbalimbali zinazoingia na kutoka ikiwepo, zao la Mahindi, Soya, Karanga, vinywaji, saruji ambavyo husaidia mapato

RC CHONGOLO AWAOMBA KANISA LA KKKT KUWASAIDIA KUTOKOMEZA MAUAJI,LISHE NA UBAKAJI SONGWE

Image
 Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo ameshiriki katika ibada maalumu ya Kanisa la KKKT Jimbo la Tunduma ikiongozwa na Askofu Mkuu wa makanisa ya KKKT Tanzania Alex Malasusa iliofanyika katika mji wa Tunduma sambamba na uzinduzi wa ukumbi wa kanisa hilo. Akiongea katika hafla hiyo Chongoloa amesema mkoa wa Songwe ni moja kati ya mikoa mikubwa na inayosifika kwa kilimo lakini cha ajabu ni moja ya  mikoa yenye changamoto ya lishe hivyo amemuomba askofu Malasusa kupitia kaanisa la KKKT Jimbo la Tunduma kuhakikisha wanahubiri pia lishe ili kunusuru Mkoa na janga la udumavu Aidha pia mkuu wa mkoa  alimueleza askofu na waumini walioshuhudia uzinduzi huo jambo lingine linausumbua mkoa wa Songwe ni tatizo la  mimba za utotoni na ndoa za utotoni hivyo amewaomba waumini wa KKKT kuisaidia serikali katika kukemea vitendo hivyo na kushiriki katika Malezi Bora ya watoto wetu Akimalizia hotuba yake Chongolo amekemea vitendo vya mauaji kukithiri ndani ya maeneo mbalimbali ya mkoa.  Kwa upande wake A

CHONGOLO KUANZA ILEJE KESHO

Image
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo anatarajia kuanza ziara ya kikazi Wilayani Ileje kuanzia tarehe 28-01 Mei ikiwa ni ziara yake ya kwanza wilayani tangu aliteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Songwe.Katika ziara hiyo Chongolo anatarajia kuambata na timu ya wataalamu toka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe wakiongozwa na Katibu tawala wa Mkoa wa Songwe Happiness Seneda. Kwa mujibu wa ratiba iliotolewa na Halmashauri ya Ileje Chongolo atapokelewa Mbebe saa tano asubuhi Kisha kuelekea shule ya wasichana Ileje sekondari katika ziara hiyo Chongolo atakuwa na mkutano wa hadhara na Wananchi uwanja wa Itumba na pia atakutana na Madiwani na Kamati ya Siasa kabla ya kukutana na watumishi wa Ileje. Kabla ya kurejea Mkoa Songwe Chongolo anatarajia kufanya Mikutano mitatu ya hadhara kata tofauti na pia anatarajia kuwa mgeni rasmi siku ya Wafanyakazi Mei mosi.

DC KIHONGOSI ATAJA BIL,124 ZIMETUMIKA UJENZI WA MIRADI MOMBA

Image
Mkuu wa wilaya ya Momba mkoani Songwe Kennan Kihongosi ame tumia sherehe za  siku ya Muungano wa Tanganyika kutaja mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Dkt,Samia Suluhu akisema alitoa Bilioni 124 zilizojenga miradi....anaripoti Ibrahim Yassin,Songwe. Alisema serikali ya awamu ya sita inafanya kazi kubwa ya kuwa ondolea wananchi changamoto zinazowakumba hivyo kazi iliyopo ni kuhakikisha miradi inatunza ili iweze kusaidia hadi vizazi vijavyo kwa ni amegusa kila sekta ikiwemo Elimu, ,Afya ,Maji, Miundo mbinu na Nishati. Dc Kihongosi aliyasema hayo jana Aprili 26/2024 wakati wa maadhi misho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania na Zanzibar yaliyofanyika kijiji na kata ya Kamsamba wilayani Momba mkoani humo. Alisema kwenye elimu zimetumika,Bilioni 31,Afya Bilioni 14.4,Vifaa Tiba Bilioni 1.6 Maji Bilioni 17.8 huku vitongoji 142 vikiwekewa ume me ambapo vitongoji 153 kazi inaendelea na pia Bilioni 6 zikitumika ujenzi wa barabara,makalavati na madaraja ndani ya miaka mitatu. Alisema katika kipindi cha

SONGWE YATAJA MAFANIKO YA SEKTA YA ELIMU TANGU KUANZISHWA KWA MKOA 2015

Image
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Happiness Seneda amesema Mkoa wa Songwe ni Mkoa kitinda mimba hapa Nchini ukiwa ni Mkoa wa 26 katika Mikoa yote 26 Tanzania bara na ulianzishwa mwaka 2015 kwa tamko la Mheshimiwa Rais. Akiongea katika Sherehe za Muungano Mkoani Songwe zilizofanyika Wilayani Mbozi Seneda ameyataja mafanikio ya Mkoa baada ya kuanzisha kwake katika programu mbalimbali za Elimu ambazo baada ya muungano na kwa awamu mbalimbali za Uongozi. " Mkoa wetu wa Songwe tunayo mafaniko katika Elimu kwa kipindi hiki cha awamu ya sita ya uongozi chini yake Daktari Samia Suluhu Hassani na kwa kweli ameupiga mwingi na anaendeleaje kuupiga mwingi" alisema Seneda Yafuatayo ni mafanikio sita ya Elimu Mkoa Songwe - Mkoa ulinza na shule za msingi 393 kwa kuna shule 554. Shule za sekondari toka 86 hadi 154 - Uanzishwaji wa elimu bure ambapo umewezesha kupanda kwa takwimu za wanaohitimu kidato cha nne kuanzia mwaka 2021 wahitimu 8,417 na mpaka 2023 wahitimu 9,457  - Uwekezaji wa fedha kwen

TAKUKURU YABAINI MBINU CHAFU INAYOTUMIWA NA MAWAKALA WA FEDHA KUWAIBIA WATEJA WAO

Image
   TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Morogoro imebaini mbinu chafu zinazotumiwa na baadhi ya mawakala kuwaibia wateja wao pindi wanapohitaji kufanya miamala ya kuweka fedha kupitia akaunti zao za kibenki. - Mwakilishi wa Mkuu wa Takukuru mkoa huo, Christopher Mwakajinga amesema hayo Aprili 23, 2024 alipokuwa akitoa taarifa kwa umma ya utekelezaji kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha kuanzia Januari 2024 hadi Machi 2024. - Mwakajinga amesema , uchunguzi uliofanywa na Takukuru mkoa uligundua kuwepo mawakala wasio waaminifu wanaopokea fedha toka kwa wateja wanaohitaji huduma ya kuwekewa fedha kwenye akaunti zao za kibenki. - Amesema Takukuru iligundua fedha hizo haziingizwi kwenye akaunti walizopewa na wateja wao na badala yake walikuwa wanatoa stakabadhi batili ( Fake)za kieletroniki ili kuwaaminisha wateja wao kuwa wamewawekea fedha katika akaunti zao kitu ambacho hakikuwa kweli. - Amesema kuwa Takukuru mkoa ilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili ambao ni maw

ACHENI TABIA ZA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI

Image
 Wananchi wa Kijiji cha Itewe Kata ya Itaka Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe wametakiwa kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi pindi uhalifu unapotokea katika maeneo yao bali wametakiwa kutoa taarifa hizo kwa Jeshi la Polisi ili ziweze kushughulikiwa kwa haraka. Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Wilaya ya Mbozi Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Julias Kishai Aprili 23, 2024 alipofika kijijini hapo kutoa elimu juu ya madhara ya kujichukulia sheria mkononi. Mrakibu Kishai alisema “acheni kujichukulia sheria mkononi toeni taarifa za uhalifu na wahalifu, katika kituo cha Polisi kilichopo karibu nanyi ikiwa ni pamoja na kuwakamata wahalifu hao na kuwafikisha kituo cha Polisi au kwa viongozi wa amani ili taratibu za kisheria zichukuliwe dhidi yao. Naye Polisi Kata wa Kata hiyo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Kajembula Mwakalinga aliwataka wananchi wa kijiji hicho kuacha tabia ya kuziamini imani za kishilikina ambazo zinapelekea mtu kujichukulia sheria mkononi bila kufuata

MCHENGERWA: TUTAZIPIMA HALMASHAURI KWA KUBUNI VYANZO VIPYA VYA MAPATO

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kigezo cha ziada ya kuzipima Halmashauri zote nchini kuanzia mwaka wa fedha ujao ni kila Halmashauri kubuni vyanzo vipya vya mapato kuanzia viwili na kuendelea kwa kila mwaka wa fedha. Mhe.Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa kufungua Mkutano wa 38 wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa - ALAT Taifa unaofanyika Zanzibar. Alisema nguvu ya kila Halmashauri ni mapato na ili iweze kutekeleza miradi yenye tija lazima kuwe na mapato ya uhakika. "Hili tulishalijadili na kamati tendaji ya ALAT na kukubaliana sasa kuanzia mwaka ujao wa fedha kigezo hili kitaingizwa rasmi katika vigezo vya upimaji wa utendaji kazi kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa,"alisema. Aidha Mhe. Mchengerwa alizitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinafanya makadirio ya ukusanyaji wa mapato kwa kuzingatia takwimu sahihi za vyanzo vya mapato hivyo kila Halmashauri ina wajibu wa kufanya tathmini ya vyanzo vya

AJIRA MPYA KUPELEKWA KWENYE ZAHANATI ZENYE UHABA WA WATUMISHI

Image
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa – TAMISEMI anayeshughulikia Afya Mhe. Dkt. Festo Dugange amesema Serikali inatarajia kutoa kipaumbele katika zahanati zilizo na mtumishi mmoja kwa kuongeza idadi ya watumishi katika ajira mpya zitakazotangazwa ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi. Dkt. Dugange amesema hayo bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu wakati akijibu swali la mbunge wa jimbo la Bukene Mhe. Selemani Zedi alitaka kujua lini Serikali itaongeza Waganga na Wauguzi katika Zahanati za Buhulyu, Luhumbo, Mambali, Ikindwa, Lukuyi, Mbutu na Karitu zilizopo katika jimbo hilo. “Tayari Rais ametoa kibali cha watumishi katika sekta ya Afya lakini pia watumishi wa sekta nyingine na serikali inatoa ‘commitment’ leo kwamba zahanati hizi ambazo zinamtumishi mmoja mmoja tutahakikisha kwenye ajira hizi ambazo zitafuata tutapeleka watumishi ili waweze kutoa huduma kwa wananchi” amesema Dkt. Dugange Akifafanua kuhusu changamoto ya watumishi wa Afya

WATUMISHI WANANDOA KUTOTENGANISHWA KIKAZI SASA KUFANYA KAZI PAMOJA

Image
  SERIKALI imesia kilio cha wabunge cha kutaka watumishi wa serikali walio katika ndoa kutotenganishwa na wenza wao sehemu wanapofanya kazi, ikisema mwaka huu wa fedha watahakikisha wenza wanapohamishwa wanakwenda na wenza wao. “Kila mtumishi mwenye mwenza wa kweli atakwenda kufanya kazi mahali pamoja, siyo lazima kiwe kituo kimoja cha kazi kama ni walimu basi mmoja atafundisha shule hii na mwingine atafundisha shule hii. Lakini mahali ambapo jioni wanakwenda kulala pamoja.” “Ukiwa na cheti cha ndoa na umefunga ndoa ya kweli maana kuna ndoa nyingine za uongo uongo, hili hatuwezi kulikubali, tutahakikisha mwanya huu wa msawazo basi kila mtumishi tunawaunganisha ili waweze kufanya kazi kwa raha na starehe,” amesema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene. Amebainisha jambo hilo limekuwa likiwakera na wabunge wengi wamekuwa wakipeleka maombi katika ofisi yake na hatua hiyo itaongeza tija katika utendaji wa kazi

SIGARA ZA MAGENDO NI HATARI KWA UCHUMI WA NCHI

Image
  WADAU wa maendeleo mkoani Songwe wametakiwa kuunganisha nguvu kwa pamoja katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya Sigara ili kulinda mapato ya serikali na afya ya umma, ikiwemo kuimarisha amani na usalama wa Taifa. Rai hiyo, imetolewa Aprili 19, 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Frida Mgomi, wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku moja ya ya kujadili biashara haramu ya sigara Mkoa wa Songwe iliyoandaliwa na kwa pamoja kati ya Kampuni ya sigara Tanzania (TCC) na ofisi ya Mkuu  ya Mkoa. Mgomi ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo katika kikao hicho,  amesema kuwa, matokeo hasi yatakayotokea ikiwa biashara haramu ya sigara itaachwa bila uangalizi ni hatari kwa uchumi na usalama wa nchi kwa kuwa biashara haramu ya sigara ndio biashara kubwa haramu ya bidhaa kwa thamani na ya pili baada ya dawa za kulevya kwa mapato yatokanayo na magendo. "Tunajua kuwa kuwepo kwa sigara za magendo na soko haramu husababisha ukwepaji kodi kwani mapato hayo yanayopotea yangeweza

BIL. 183.63 KUKAMILISHA MABOMA 6,415 YA SEKTA YA AFYA NA ELIMU

Image
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema katika mwaka wa fedha 2024/25 TAMISEMI imepanga kukamilisha ujenzi wa maboma 6,415 ya miundombinu ya sekta ya afya na elimu kwa gharama ya Shilingi bilioni 183.63. Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2024/25. Waziri Mchengerwa amesema kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 52.86 ni fedha za ruzuku ya serikali kuu na Shilingi bilioni 130.77 ni fedha zitokanazo na mapato ya ndani ya halmashauri na kuongeza kuwa, ukamilishaji wa maboma mengine utaendelea kadri ya upatikanaji wa fedha. “Ninawalekeza makatibu tawala wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri kusimamia utekelezaji wa mwongozo wa uanzishaji wa maboma ili kuzuia uanzishaji wa maboma usiozingatia mwongozo na taratibu zilizopo” Mhe. Mchengerwa amesisitiza. Mhe. Mchengerwa ameanisha kuwa, Novemba mwaka jana

WAKULIMA WA ZABIBU DODOMA KUNUFAIKA NA UJENZI WA KIWANDA CHAMWINO

Image
Wakulima wa zao la Zabibu kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na Mkoa wa Dodoma kwa ujumla, wanatarajia kunufaika na kilimo cha zao hilo kufuatia ujenzi wa kiwanda cha kuchakata Zabibu kinachojengwa na Serikali kwenye Kata ya Chinangali 11 ambacho kitasaidia kuhifadhi zabibu iliyovunwa pamoja na mchuzi wake kwa ajili ya soko. Hayo yamebainishwa leo Aprili 19, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alipofanya Mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kata ya Mvumi Makulu katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kikazi pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Mkoa wa Dodoma. Jawabu la ujenzi wa kiwanda hicho limefuatia kero iliyoulizwa na mwananchi juu ya ukosefu wa soko la zabibu. Mhe. Senyamule amesema Serikali sikivu ya awamu ya Sita inatambua umuhimu wa kilimo ndio maana inajenga kiwanda hicho ili kuwapunguzia adha wananchi wake kwa kupata uhakika wa soko.  "Ujenzi wa kiwanda hiki unakuja kama mkombozi kwa Wakulima wa Zabibu kwa kuwa zabibu z

VIONGOZI MKOA WA SONGWE WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYABIASHARA

Image
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Zanzibar,  Mhe. Omar Said Shaban ametoa wito kwa viongozi waliopo mkoa wa Songwe kuhakikisha wanatatua changamoto za wafanyabiashara wa mkoa huo ili zisigeuke kuwa kero. Ametoa wito huo leo Alhamisi Aprili 18, 2024 wakati alipotembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe iliyopo Nselewa, Mbozi. "Serikali zetu zote mbili zinadhamira ya dhati wananchi wake waweze kufikia malengo yao kwa kutatua changamoto wanazokabiliana nazo ili wajikwamue kiuchumi" Hii ndio faida ya Muuungano, niwashukuru kwa kuendelea kuijenga Songwe katika taarifa yenu mmeonesha mafanikio na changamoto pia njia za kukabiliana na changamoto hizo" amesema  Ameeleza kuwa Songwe ni mkoa wa kimkakati ambao unanufaika na furasa zinazopatikana  katika nchi jirani. "Tupo mpakani tunapakana na nchi zenye fusa za kibiashara Songwe ni geti kuu la nchi za SADC ikiwa na geti linalopitisha fursa mbalimbali za ajita uwekezaji, uzalishaji pamoja na kilimo" ameeleza &

TANZANIA NA ZAMBIA ZATATUA KERO NNE ZA KIBIASHARA, MAWAZIRI WA VIWANDA KUKUTANA TUNDUMA LEO

Image
  Tanzania na Zambia zimefanikiwa kufuta kero nne kati ya keo 15 zilizokuwepo awali ili kirahisisha michakato ya kibiashara na nchi hizo kutegemeana kibiashara. Hayo yamesemwa Jumatano Aprili 17, 2024 na Katibu Mkuu wa Wizra ya Viwanda na Biashara wa Tanzania, ndugu Hashil Abdallah wakati wa kikao cha pamoja cha makatibu wakuu wa nchi zote mbili katika sekta hiyo. Akizungumza katika kikao hicho, ndugu Hashil amesema kuwa kikao hicho ni utekelezaji wa maelekezo ya wakuu wa nchi zote mbili Tanzania na Zambia ambao walikutana jijijni Lusaka mwezi Oktoba, 2023 ambapo miongoni mwa makubaliano ni pamoja na mawazili wa pande mbili wanaohusika wakae na watatue changamoto zinazowagusa wafanyabiashara katika nchi hizo. “Kikao hiki lilikuwa cha makatibu wakuu na kikao cha mawazili kitafanuika kesho (Leo Alhamisi) hapa mpakani Tunduma. Tunatarajia kikao hicho kitakuwa muhimu zaidi katika utatuzi wa kero na changamoto mbalimbali za ufanyaji biashara katika nchi zetu hizi” amesema Katib Mkuu huyo na

MWALIMU ATOKA NDUKI SHULENI KUWAKIMBIA WANAOMDAI

Image
  WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Luwa katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, walikatisha masomo kwa takribani saa tatu baada ya wajasiliamali kufika shuleni hapo na kumfanyia shambulio la aibu Mwalimu Mkuu wa Shule kwa madai ya kushinikiza walipwe fedha wanazomdai mwalimu aliyekopa bidhaa kwao. Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Mwenyekiti wa Kijiji, Stedius Pastory, amesema tukio hilo lilitokea majira ya saa 3 asubuhi wakati mwalimu waliyekuwa wakimdai akiwa shuleni hapo akiendelea na majukumu yake. Amesema mwalimu aliyedaiwa baada ya kuwaona wajasiriamali hao wakifika shuleni hapo na gari lao, ghafla alitimua mbio na kukimbilia kwenye shamba la mahindi karibu na shule hiyo ndipo mmoja kati yao alianza kumkimbiza. “Baada ya kushindwa kumkamata, alirejea katika eneo la shule na kuungana na mwenzake aliyekuwa amebaki kwenye gari na kwenda moja kwa moja walimvamia ia mwalimu mkuu aliyekuwa akizungumza na wazazi wa wanafunzi waliokuwa wamefika kulipa michango kisha kumkaba, kumkat

SERIKALI YATANGAZA AJIRA MPYA ZA WATENDAJI 3865

Image
  Waziri Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Seriali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa amesema ofisi yake inakamilisha taratibu za kuajiri watendaji wa kata 525, watendaji wa vijiji 1,986, watendaji wa mitaa 1,333 na maofisa tarafa 21. Amesema hayo leo Jumanne, Aprili 16, 2024 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25, yanayohusisha mafungu ya Tamisemi, Tume ya Utumishi wa Walimu na mikoa.

ANAYETAFUTA MADARAKA KWA MAFARAKANO HAFAI NDANI YA CCM - BALOZI DKT. NCHIMBI

Image
  "Mtu yeyote anayetafuta madaraka kwa mafarakano, kwa misingi ya ukabila, kwa misingi ya dini hawafai kuwa kiongozi wa serikali wala katika chama chetu cha mapinduzi, kila mtanzania anatakiwa kukumbuka kuwa viongozi sahihi wataisimamia serikali sahii" "Chama kibovu kitazaa serikali mbovu, chama kisicho makini kitazaa serikali isiyo makini, chama imara kinaanza kujengwa katika mashina, tutambue kwamba hiyo ndio ngazi ya kwanza ya umuhimu wa pekee katika chama chetu na wao watambue wao ndio wa kwanza kuusimamia wajibu wa wananchama" "Hii ndicho chama pekee kinachoongelea majukumu ya chama kwa wanachama wake na huwezi kuyatenganisha mafanikio ya serikali na CCM kwakuwa CCM madhubuti ndio yenye kuleta maendeleo kwa taifa hili."

MACHIFU SONGWE WATOA OVYO KWA WANAOMCHAFUA RAIS SAMIA MITANDAONI

Image
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi amepewa heshima ya uchifu ndani ya Mkoa wa Songwe na sasa anaitwa Chifu Nchimbi. Chifu Nchimbi amekabidhiwa Shuka jeupe kama ishara ya CCM kuendelea kushika madaraka, amepewa kiti maalum kwa ajili ya kukitumia wakati akiendelea kuchapa kazi pamoja na mkuki kama ishara ya ulinzi katika eneo lake la kazi ili kumuepusha na mabaya. Akizungumza mara baada ya kumsimika uchifu, Mwenyekiti wa Machifu Mkoa wa Songwe, Chifu Msangwale amemuomba Balozi Nchimbi kukemea masuala ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kwani baadhi ya watu wamekuwa wakiitumia kumchafua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Chifu Hangaya.

NCHIMBI APIGA MARUFUKU KUENDELEZA MAKUNDI BAADA YA UCHAGUZI WA NDANI

Image
"Niwasihi wana CCM kataeni viongozi wa kuandikiwa, wa kuletwa mfukoni ninyi mnaishi na watu kwenye maeneo yenu na mnawajua , chagueni watu kwa sifa na mtu apewe kwa sifa zake sio za rafiki au mpambe wake" "...lakini tujue kwenye uchaguzi kuna kusinda na kushindwa hivyo ni lazima tukubali matokeo mara baada ya chaguzi" "Makosa makubwa ni kuendeleza makundi ya uchaguzi baada ya uchaguzi , makundi yaishe mara tu baada ya uchaguzi kutangazwa" "Nafasi kubwa kulikonzote ndani ya CCM ni UANACHAMA, usichaguliwe kuwa kiongozi ukajiona wewe ndio mkubwa kuliko wote, wewe ni mtumishi na mda wowote unaweza kutumika sehemu nyingine kwa maslahi ya watu wote na sio kutumia nafasi yak kwa kuweka makundi" "Viongozi lazima watambue nafasi zao za utumishi, ukiwa Mbunge unajua wewe ni mtumishi wa wananchi wako, ukiwa Waziri utambue wewe ni mtumisi wa wananchi wako ukitaka kujifanya boss lazima utapata changamoto kwenye uendeshaji wa eneo lako" Balozi Dkt. E

WALIOHAMA NGORONGORO WAMTUMIA SALAAMU RAIS SAMIA

Image
  Wananchi waliohama kwa hiyari kutoka eneo la hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga wamemuomba mkuu wa mkoa huo mhe. Balozi Dkt.Batilda Salha Burian kumfikishia salaam za shukrani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwahamisha kwa hiyari kutoka ndani ya hifadhi hiyo na kuwajengea huduma bora za kijamii nje ya Hifadhi. Wananchi hao wakiongozwa na makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro mhe. Emmanuel Gabriel Tonge na madiwani waliohama kutoka Ngorongoro kuelekea katika Kijiji hicho wamesema kuwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amewaondoa kwenye mateso ya muda mrefu ya kuishi na wanyama hatarishi, kutokuwa na uhuru wa kufanya shughuli za kiuchumi kutokana na kuzuiliwa na sheria za hifadhi pamoja na Watoto wao kushindwa kupata elimu bora walipokuwa Ngorongoro. “Mhe. mkuu wa mkoa tunakuomba sana mfikishie salaam zetu Mhe. Rais wetu Dkt.Samia, huyu mama amejawa na utu, huruma na upendo kwetu sisi wan

TISA MBARONI KWA MAUAJI YA MLINZI

Image
  HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linawashikilia watu tisa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mlinzi, Samweli Nofola (28), mkazi wa Kijiji cha Mtewele kilichopo Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe. Hayo yamethibitishwa leo Aprili 14, 2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga wakati akizungumza na Mwananchi Digital. Amesema tukio hilo la mauaji limetokea katika Mtaa wa Uzunguni, Kata ya Maguvani, usiku wa kuamkia April 13, 2024, saa 8:30 usiku. Kamanda Banga amesema marehemu alikuwa mlinzi wa kampuni ya ulinzi iliyopo mjini Makambako na siku ya tukio, watu wasiojulikana walimuua mlinzi huyo na kuvunja maduka manne na kuiba vitu mbalimbali.