Posts

Showing posts from August, 2024

DED MOMBA APONGEZWA NA BARAZA LA MADIWANI KWA UKUSANYAJI MAPATO

Image
Baraza la Madiwani limekutana Kujadili hesabu za mwisho kwa mwaka wa fedha 2023/2024. Na limepitisha hesabu hizo. Mkutano huo umefanyika leo tar Septemba 29. 2024 katika ukumbi wa mkutano wa Halmashauri.  Katika mkutano huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba Mhe. Mathew Chikoti amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri pamoja na watumishi wote kwa juhudi na umoja waliouonesha katika ukusanyaji wa mapato. Juhudi hizo zimefanya kuwa na Makusanyo kwa 168% ikiwa  Makisio yalikuwa Bilion 1.8 na kiasi kilichokusanywa ni Bilioni 3.1 sawa na zidio la Bilioni 1.3. 'Madiwani na watumishi wote kwa pamoja tusimamie ukusanyaji wa mapato' amesema Chikoti.

UBUNIFU WA NAMTUMBO KUJIBU MASWALI YA KURASA ZAO ZA MITANDAO YAO YAWAKOSHA WENGI

Image
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Namtumbo Philemon Magesa ameendelea na utaratibu wake wa kusikiliza na kutatua kero  kwa njia mbalimbali ikiwe kurasa za mitandao ya kijamii ya Halmashauri ya Namtumbo.

ZEGE LAANZA KUMWANGWA ENEO LILILOKUWA MAARUFU KWA UPORAJI WAFANYABIASHARA BARABARA YA MLOWO-KAMSAMBA MKOANI SONGWW

Image
Zoezi la kumwaga zege mlima wa Nyimbili maarufu kama Benki kuu barabara ya Mlowo Kamsamba limeanza kutekelezwa na Mkandarasi kupitia Wakala wa barabara Mkoa wa Songwe (Tanroads) ambapo sambamba na uwekaji wa zege hilo pia unaendana na upunguzaji wa ukali wa mwinuko katika mlima huo  maarufu kwa jina la benki kuu. Eneo hilo ambalo lilijulikana zaidi miaka ya nyuma kama benki kuu kutokana na kuwa na Vitendo vya utekaji magari na uporaji  hali iliopelekea watu wengi kufanyiwa vitendo vya Ukatili na udhalilishaji ambapo Wadau wa njia hiyo wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwatengenezea zege hilo na kupunguza mlima. "Kwa kweli tuna kila sababu ya kushukuru eneo hili kudhibitiwa kwani sisi madereva wa kamsamba eneo hili la benki kuu limekuwa eneo hatari kwa Usalama wa maisha yetu na abiria wetu tumetekwa sana na magari yetu tena mchana kweupe ndani ya msitu huu " amesema Emanuel Mwanga dereva wa fuso njia ya Kamsamba. Baadhi ya wafanyabiashara wa Ng'ombe na Samaki nao

SAKATA LA WATU KUPOTEA MIILI TISA YAFUKULIWA DODOMA

Image
  Jeshi la Polisi limesema baada ya kuendelea na uchunguzi na mahojiano kuhusu vifo vya Watu watatu ambao miili yao imefukuliwa nyumbani kwa Mganga wa kienyeji aitwaye Nkamba Kasubi Mkoani Singida, hatimaye jana August 27,2024 Mganga huyo alikubali kuwaongoza Polisi hadi kwenye Mji wake mwingine uliopo Kijiji cha Porobanguma, Tarafa ya Kwamtoro Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma na kuonesha mashimo mengine sita ambayo walifukia Watu wengine wakiwemo Watoto waliowaua na kuwazika na kufanya miili iliyofukuliwa kwa Mganga kufikia tisa huku mwili mwingine wa 10 ukiokotwa porini. Taarifa iliyotolewa leo August 28,2024 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime imesema “Baada ya taratibu za ufukuaji kufanyika ilipatikana miili ya Seni Jishabi (28), Mkazi wa Kijiji cha Porobanguma ambaye alipotea toka March 3, 2024 na walidai kumuua na kumzika April 2024, Mohamed Juma (27), Mkazi wa Nyamikumbi A Mkoa wa Singida ambaye alipotea May 15, 2024 na wao wameeleza walimuua kwa kumnyonga kisha kumzika, D

DED MAGESA AUNDA TIMU NAMTUMBO YA KUFUATILIA NA KUTATHIMINI MIRADI KABLA YA MALIPO

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Ndg. Philemon Mwita Magesa ameunda kikosi kazi (Value for Money Audit Team) ambacho kimekuwa kikihusika na Ufuatiliaji na Kufanya Tathmini ya Miradi Mbalimbali kabla ya Kufanya Malipo. "Uwepo wa kikosi kazi hiki cha Ufuatiliaji na Tathmini ya Miradi kabla ya Kufanya malipo (Value for Money Audit Team) inasaidia kufanya Malipo kwa Mkandarasi,Fundi au Mzabuni aliyekidhi Vigezo vya Mahitaji yetu na Si vinginevyo" - Amesema Magesa Akizungumza Katika kikao kazi na Watendaji kata 21 za Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Magesa amewataka watendaji kata Kuwa Makini na Miradi uku akizitaja Faida za kikosi kazi hicho cha Ufuatiliaji Miradi Kabla ya Malipo (Value for Money Audit Team) Ikiwa ni Kuhakikisha Mradi unatekelezwa kwa Viwango kama ilivyopangwa na Serikali. pia kikosi kazi kitakuwa kinaangalia Vifaa na Mahitaji yanayo Nunuliwa kama yapo katika Mpango wa Mradi huo ili Mkandarasi,fundi au Mzabuni aweze kulipwa Stahiki kihala

BINTI AKAMATWA KWA WIZI WA MTOTO

Image
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kumkamata mwanamke aliyejulikana kwa jina la Hadija Juma (24) mkazi wa Kijiji cha Sengerema wilaya ya Uyui Mkoa wa Tabora kwa tuhuma ya kuiba mtoto mchanga mwenye jinsi ya kike katika kituo cha afya Mbika Halmashauri ya Ushetu Mkoa wa Shinyanga. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumamosi Agosti 24,2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amesema mtoto huyo aliibiwa Agosti 20,2024 saa 12 jioni ndipo jeshi la polisi lilianza kufanya ufuatiliaji na kufanikiwa kumkamata mwanamke huyo Agosti 22,2024 akiwa na mtoto huyo. “Mtoto huyo alizaliwa Agosti 17,2024 katika kituo cha afya Mbika na mama yake mzazi kuendelea kuwepo katika kituo hicho kwa uangalizi baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji… na siku ya tukio Agosti 20,2024 majira ya saa 12 jioni wakati mama akiendelea kufanya mazoezi ndipo akabaini mtoto hayupo. Baada ya kupokea taarifa hizo ufuatiliaji wa haraka ulifanyika na Agosti 22,2024 saa tatu usiku askari wali

DIWANI KYALAMWENE ATWAA UMAKAMU MWENYEKITI HALMASHAURI YA MOMBA

Image
 Mhe. JOSHUA KYALAMBWENE MAKAMU MWENYEKITI MPYA WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOMBA. Katika kikao cha Baraza Kuu la Madiwani la robo nne ya kwa mwaka wa fedha 2023/2024 wajumbe wa Baraza hilo walimchagua Mhe. Joshua kuwa Makamu wa Mwenyekiti wa Halmashauri. Katika uchaguzi huo Mhe. Joshua hakuwa na mgombea mwenza,amepigiwa kura zote za NDIYO sawa na asilimia 100 hivyo alitangazwa kuwa Makamu Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba. Kikao hicho kilijumuisha wajumbe mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya Mhe. Elias Mwandobo, Kamati ya Usalama ya Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg Fabian Manoza Said, Wakuu wa Tasisi mbalimbali, pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo. Baada ya uchaguzi Mhe. Kyalambwene amewashukuru sana wajumbe waliomchawaliomchagua na kuahidi kushirikiana nao vyema katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba.

ANAEDAIWA KUMUUA HAUSIGELI AKAMATWA

Image
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Jackson Magoti (34), Mkazi wa Michese Tanesco mkoani Dodoma kwa tuhuma za mauaji ya mfanyakazi wa nyumbani, Sainethi Kakululu (20) mkazi wa mtaa wa Ipuli, Mahina jijini Mwanza. Taarifa ya kukamatwa mtuhumiwa huyo ilitolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Wilbrod Mutafungwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo. DCP Mutafungwa alisema mtuhumiwa huyo alitiwa mbaroni Agosti 16, mwaka huu saa 5:30 asubuhi jijini Dodoma baada ya kufuatiliwa kwa muda mrefu kufuatia mauaji aliyoyatekeleza Agosti 5, mwaka huu saa 11:30 jioni nyumbani kwa Jackkline Ngowi, ambapo alimuua mfanyakazi huyo kwa kumkaba shingo. Kufuatia matukio hayo, Kamanda huyo wa Polisi amewataka wananchi wa mkoa wa Mwanza kutoa taarifa za waalifu na uhalifu haraka ili jeshi hilo lichukue hatua mara moja, huku wakiendelea kufanya msako katika visiwa, mialo na Ziwa Viktoria kwa ajili ya kudhibiti uhali

MOLLEL ATAKA FEDHA ZA LISHE ZIWAFIKIE WALENGWA

Image
  Naibu waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesisitiza umuhimu wa kuzingatia lishe na matumizi sahihi ya fedha za lishe ikiwa ni kuwafikia walengwa husika wanaostahili kupata huduma hiyo Dkt. Mollel ameyasema hayo Agosti 22, 2024, wakati wa Kikao kilichowakutanisha kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wadau wa lishe katika kuangali hali ya lishe katika mkoa wa Songwe ambapo hali ya lishe imekua nzuri tofauti na mwaka 2022/23 kwa kupanda hadi nafasi ya 7 kitaifa. Aidha Dkt. Mollel amepongeza juhudi za mkoa wa Songwe katika kukabiliana na udumavu na kuzingatia lishe kwani lishe bora kwa watoto husaidia katika kukuza akili na hivyo kupelekea taifa lenye watu wenye weledi mzuri. “Niwapongeze kwa juhudi hizi ambazo mmepitia, awali Songwe haikua vizuri kwenye lishe lakini kwa sasa mafanikio makubwa nimeyaona na hii itasaidia katika kukuza kizazi chenye akili kwani lishe husaidia katika ukuaji wa akili” Amesema Dkt. Mollel Awali akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongol

DC BUSEGA APIGWA MAWE

Image
 Wakati baadhi ya Wananchi wakikiri kuwa kuna Watu kadhaa wanahofiwa kufariki kutokana na kupigwa risasi na Polisi wakijaribu kuwatawanya kwenye maandamano yaliyofanywa na Wananchi huko Busega Mkoani Simiyu leo, imethibitika kuwa Mkuu wa Wilaya ya Busega Faiza Salim pamoja na Maofisa wengine wamejeruhiwa kwa mawe na Wananchi hao.  imeelezwa kuwa Wananchi walimrushia Mkuu huyo wa Wilaya mawe wakati akiwasogelea kwa nia ya kuwasikiliza ambapo hawakutaka Kiongozi huyo kufanya chochote na kuanza kumrushia mawe yaliyopelekea kujeruhiwa kwenye ubavu na mgongoni huku Maofisa wengine aliokuwa ameambatana nao ambao ni Kamanda wa Zimamoto Simiyu na Kaimu Afisa wa TAKUKURU Simiyu wakijeruhiwa kichwani na kupelekea kushonwa nyuzi. Kwa sasa hali zao zinaendelea vizuri na wameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupata matibabu. Wananchi wa Busega waliandamana leo hadi Kituo cha Polisi baada ya kuchoshwa na kushamiri kwa matukio ya Watoto wao kupotea katika eneo la Lamadi bila Polisi kuchukua hatua za

NAMTUMBO WATOA HUDUMA YA KUJIBU KERO ZA WANANCHI KUPITIA KURASA ZAO ZA MITANDAO

Image
  Halmashauri ya Namtumbo iliopo Mkoani Ruvuma imeazisha utaratibu wa kujibu maoni ya Wananchi wanayoyatoa kupitia ukurasa wa mtandao wa Instagram wa Halmashauri hiyo kitendo kinachonyesha ukomavu wa Viongozi wa Halmashauri hiyo inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya Ngollo Malenya ambae ameoneka akiwajibu maoni yao kupitia ukurasa huo. Philemon Magesa mkurugenzi wa halmashauri hiyo akiongea na mwandishi wetu amesema hao kama halmashauri kupitia mwongozo wa Sera ya matumizi bora, sahihi na salama ya mifumo na vifaa vya Tehama Serikalini ya mwaka 2014 ; Sura ya 2 (1)(2) na (3) inayohusiana na kusimamia na kuendesha Tovuti ya Serikali na Mitandao ya Kijamii inasema: Kwa mujibu wa Mwongozo huu, Tovuti ni mfumo wa ukusanyaji, uhifadhi na usambazaji wa habari, picha na nyaraka kwa njia ya mtandao. Mfumo huu pia unaweza kutumika kwa ajili ya kutoa mrejesho na huduma mbalimbali za Serikali. Mwongozo huu unahusu Tovuti, Tovuti kuu (portal), blogu na mitandao yote ya jamii. Wao wapo kutekeleza Sera na

RPC GEITA AONGOZA KUAGA MWILI WA ASKARI KALONGE KUZIKWA SONGWE

Image
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Safia Jongo amewaongoza Maafisa, Wakaguzi, Askari na waombolezaji kumuaga aliyekuwa Koplo wa Polisi (CPL) Frank Abraham Kalonge aliyefariki dunia Agosti 16, 2024 Katika Hospitali ya SDA Kasamwa - Geita na kuagwa Agosti 17, 2024 katika kambi ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoani Geita

MSANII HARMONISE AHUKUMIWA KUILIPA FIDIA CRDB BENKI KWA KUSHINDWA KULIPA MADENI KWA WAKATI

Image
   Msanii wa Bongo fleva Rajab Abdul (Harmonize) atakiwa kuilipa Benki ya CRDB fidia ya Millioni 10, gharama za kesi na Deni la Mkopo la Tsh. Milioni 103 baada ya kushindwa kulipa kikamilifu Mkopo wa Tsh. Milioni 300 tokea Mwaka 2019 - Aidha, CRDB na Harmonize walikubaliana angefungua akaunti ya Kibiashara katika benki hiyo kisha kuweka Tsh. Milioni 100 na kuifanya akaunti hiyo kuwa akaunti yake kuu katika shughuli zake za Kibiashara, lakini alikiuka makubaliano hayo - Benki ya CRDB ilifikia uamuzi wa kwenda Mahakamani baada ya usumbufu wa ulipaji deni kutoka kwa msanii huyo, ambapo Mahakama ilitoa wito mara kadhaa kwa Msanii huyo lakini hakufika Mahakamani

MTOTO MCHANGA AMEOKOTWA MTARONI TUNDUMA

Image
Mtoto Mchanga anayekadiliwa kuzaliwa muda mfupi ameokotwa mtaroni katika mtaa wa Mpemba kata ya Mpemba Mjini Tunduma Mkoani Songwe akiwa ametelekezwa na mtu asiyefahamika baada ya kujifungua. Wakizungumza  wananchi wa Shina 8 mtaa wa Mpemba Halmshauri ya mji Tunduma wamesikitishwa na kitendo cha Mtu asiyefahamika kutelekeza mtoto mtaroni baada ya kujifungua.REGINA KAMWELA mkazi wa Mpemba Tunduma,EUDIA KANDONGA mkazi wa Mpemba Tunduma na BENI SILINGWE Afisa usafirishaji Bodaboda Amani Kandonga Balozi wa shina namba 8 Mtaa huo amethibitisha kuokotwa kwa mtoto huyo huku akilaani watu wanaofanya matukio ya kuzaa watoto na kutelekeza vichanga. Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Halmshauri ya mji Tunduma Dkt Erasto Luvanda amekiri kupokea kichanga hicho kikiwa kimepigwa baridi kutokana na kukaa muda mrefu katika mtaro jambo lililopelekea kifo wakati kikipatiwa matibabu.

RAIS AFANYA UTEUZI MZITO

Image
 

RC MANYARA ATINGA NA KIVAZI CHA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDA

Image
  Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga leo Agosti 14, 2024, ametembelea Shule ya mpya wasichana ya Manyara Girls na kuongea na wanafunzi pamoja na kuwakaribisha rasmi Mkoa wa Manyara wanafunzi 110 waliokwishawasili shuleni hapo na kuanza masomo yao ya kidato cha tano (5) kwa mchepuo wa Sayansi (PCM na PCB) shule hiyo iliyopo Kata ya Maiska Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara. Mhe. Mkuu wa Mkoa, amewashukuru na kuwapongeza wazazi walioleta watoto wao katika shule hiyo mpya na kuwahakikishia watoto wao watapata Elimu na huduma bora, ulinzi na usalama wakati wote watakapo kuwepo shuleni hapo. Sambaba na hilo RC Sendiga, ameagiza umaliziaji wa miundombinu yote ambayo bado haijakamilika ikamilike mapema ili wanafunzi waweze kupata huduma hizo hasa ya bwalo.

POLISI WAELEZA SABABU KIFO CHA MANDOJO

Image
  JESHI la Polisi mkoani Dodoma, limetaja sababu za kifo cha msanii wa nyimbo za Bongo Fleva, Joseph Francis maarufu Mandojo, kuwa ni kukutwa kwenye kibanda cha mlinzi ambaye aliita mwizi na watu kujitokeza na kumshambulia. Mandojo anadaiwa kuuawa kwa kupigwa na watu wasiojulikana kwa kutuhumiwa kuwa ni mwizi katika uzio wa Kanisa Katoliki eneo la Nzuguni B, jijini Dodoma. Aidha, taarifa kutoka eneo hilo zinadai kuwa msanii huyo alikwenda kanisani hapo kwa ajili ya kusali. Akizungumza na Nipashe, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Anania Amo, alisema Mandojo alikutwa na mlinzi wa eneo hilo majira ya saa 10:00 alfajiri ndani ya kibanda chake.  Alisema baada ya mlinzi kuona hivyo, alipiga kelele kisha watu waliokuwapo eneo hilo na wengine wanaodhaniwa kuwa ni waamini wa kanisa hilo waliokuwa kanisani, walimshambulia kwa kumpiga hadi kufariki dunia.  "Mandojo alituhumiwa mwizi, mlinzi alipopiga kelele kwa muda ule watu walijitokeza na kuanza

WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SONGWE WASISITIZWA KURIPOTI HABARI ZINAZOELIMISHA JAMII MADHARA YA RUSHWA

Image
  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imewapa mafunzo  waandishi wa habari wa Mkoa wa Songwe ili kuwejengea uwezi wa namna ya kuepuka rushwa na kuelimisha jamii juu ya atheri za rushwa. Mafunzo hayo yalilenga kuimarisha uwezo wa waandishi katika kufichua na kuripoti rushwa katika sekta mbalimbali za umma na binafsi yametolewa na Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Songwe,  Frida Wikesi katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.       (Mwenyekiti wa krabu wa Waandishi wa habari Mkoani Songwe Stephan Simbeye akitoa neno) Akitoa mafunzo hayo, Kamanda huyo amesema kuwa wanahabari ni kundi muhimu ambalo linaweza kusambaza elimu kwa jamii kwa haraka huku akiwasisitiza kuandika habari zinazoelimisha na kufichua vitendo vya rushwa. "Tunaelekea kipindi cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu, huku ndiko kunakolalamikiwa kuhusika na masuala ya rushwa nawaomba muandike habari za mapambano dhidi ya rushwa" amesema  Kamanda Wikesi na kuongeza;     ( Waandishi wa h

CCM SONGWE YAWAONYA WABUNGE NA MADIWANI KUCHAFUANA MITANDAONI

Image
  Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Songwe kimelaani vikali vitendo vya kuchafuana katika mitandao ya kijamii hususani mtandao wa Whatsapp kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na katibu  uenezi siasa na mafunzo Yusuph Ally imedai kuwepo kwa Viongozi,Madiwani,wabunge na wanachama wanatumia mitandao ya kijamii Mkoani Songwe kuchafuana kama taarifa inavyosomeka hii hapa.  TAARIFA KWA UMMA  HABARI ZENU WANACHAMA, MAKADA NA VIONGOZI WOTE WA CCM MKOA WA SONGWE! Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Songwe kinasikitishwa na kinalaani kampeni za kupakana matope baadhi ya waheshimiwa wabunge, madiwani na viongozi wa chama wa mkoa wetu wa Songwe zinazoendelea kwenye makundi songezi ya whatsap. *Jambo hili ni kosa la kukichafua na kukipaka matope chama kitu ambacho ni utovu wa nidhamu unaopelekea kwenye makosa ya maadili.* _Mijadala yote ya chama na hoja humalizwa kwenye vikao halali vya chama._ *Kwa muktadha huu, chama kinakemea na kupiga marufuku mijadala yote ya kupakana matope inayoendelea kwenye mitandao ya kij

WATIA NIA WANAOTUMIA MISIBA KUPATA UMAARUFU WAONYWA

Image
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Salim Abri Asas, amesema baadhi ya watia nia katika wilaya ya Iringa Vijijini wamekuwa wakitumia mbinu zisizo za kimaadili, kama vile kuomba misiba itokee ili wapambe wao wapate nafasi ya kutoa rambirambi na kujipatia umaarufu wa kisiasa. Akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Iringa Vijijini, Asas amesema kuwa baadhi ya wagombea wamekuwa wakiwatumia wapambe wao kupeleka rambirambi kwenye misiba hiyo akionya hali hiyo kuwa inakiuka kanuni za chama cha mapinduzi CCM, ambazo zinahitaji utaratibu wa haki katika upatikanaji wa nafasi za uongozi lakini inatengeneza makundi yasiyo na afya ndani ya chama. ASAS amesema wapambe hao wanashindwa kujihusisha katika kusaidia jamii kwenye changamoto mbalimbali kama afya, elimu, miundombinu na badala yake wanatafuta misiba kujijenga kisiasa akionya kwamba watakapokatwa waendelee kusaidia jamii na sio kuisaidia jamii katika kipindi hiki tu cha kusaka uongozi. Hatahivyo Asas amesema w

WANANCHI 260 WAIBURUZA HALMASHAURI MAHAKAMANI

Image
  Wananchi 260 wakiongozwa na wakili Saimoni mbwambo wamefungua shauri dogo kwenye mahakama kuu kanda ya Tanga dhidi ya halmashauri ya wilaya ya muheza  kwa madai ya kutaka kuchukua mashamba yao kuwapa wawekezaji bila kufuata utaratibu . Awali Wakili saimoni mbwambo akiwawakilisha wananchi hao amesema kua wamefungua shauri hilo dogo kwa wanakijiji  10 ambao watawawakilisha wenzao 250 kutoka vijiji sita ikiwemo mangamlima , mamboleo, zenith, miyanga, vilivyopo tarafa ya bwembera ambapo wanakusudia kufungua shauri la ardhi mahakamani hapo mara baada ya maombi yao madogo ya watu 10 yatakapokubaliwa kuwawakilisha wenzao  watapeleka shauri hilo ili kuitaka halmashauri kuacha kuwasumbua wananchi hao ambao wamekua wakitumia mashamba hayo kwa zaidi ya miaka 40 kwa shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo na badala yake kama wanayataka ufuatwe utaratibu wa kuwapa fidia inayostahili kulingana na mashamba hayo ambayo ni zaidi heka 1000 Shauri linatarajia kushikilizwa tena tarehe 28 mwezi wa 8 2024 kwa

CHONGOLO ATOA MIEZI MIWILI KWA WAKURUGENZI SONGWE KUWEKA MAONEO YA MAONYESHO YA KILIMO MAOFISINI MWAO

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo kuanzisha sehemu za maonesho ya kilimo kwenye maeneo ya ofisi au makazi yao ili wananchi waweze kujifunza. Mhe. Chongolo ametoa maagizo hayo baada ya kutembelea na kukagua mabanda ya maonesho ya wakulima maarufu Nanenane katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. Mhe. Chongolo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika viwanja hivyo Jumanne Agosti 6, 2024, amesema kuwa kama walivyotengeneza viunga vya mbogamboga kwenye maonesho ya Nanenane hivyohivyo wafanye kwenye maeneo yao iloi wananchi waweze kuhamasika na kujifuynza. Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa atapita kukagua utekelezaji wa agizo hilo ndani ya miezi miwili.

MBOZI YAPAA UKUSANYAJI WA MAPATO, YAFIKIA ASILIMIA 116

Image
Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imevuka malengo ya ukusanyaji mapato kwa mwaka wa Fedha 2023/24, ikikusanya asilimia 116. Akizungumza katika kikao cha Baraza kamili la madiwani (Taarifa za Kata) Jumanne Agosti 6, 2024  kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Makamu Mwenyekiti Mhe. Samson Nzunda amesema kuwa lengo lilikuwa ni kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 5.025 lakini imekusanya bilioni 5.83 ambayo ni sawa na asilimia 116. Amesema kuwa ufanisi huo ukilinganishwa na miaka ya nyuma Kuna ongezeko la zaidi ya asilimia 10 "Umoja wetu ndio umetufanya kuvuka lengo kwa mwaka wa fedha ulioisha ndio maana mwaka  2024/25 tumeongeza makadirio mpaka bilioni 6.6 na kutokana na vyanzo tulivyonavyo tutafikia malengo" amesema  na kuongeza; "Kutokana na vyanzo vyetu tunaweza fika bilioni 7 na angalau siku moja Mbozi iwe Halmashauri inayoongoza kwa mapato katika Mkoa wa Songwe" amesema Katika Baraza hilo imetolewa taarifa juu ya mikakati ya ukusanya

KASI YA WANAWAKE MAONYESHO YA NANE NANE MBEYA YAMVUTIA SENEDA

Image
 Katibu tawala Mkoa wa Songwe Happiness Seneda amekuwa ni mmoja kati ya Viongozi waliojitokeza katika maonyesho ya nane nane ya Kanda ya nyanda za juu kusini yanayoendelea Mkoani Mbeya leo tarehe 06/08/2024 Akiongea mara ya baada ya kutembelea mabanda ya wajasiliamali katika maonyesho  hayo amesema kuwa amevutiwa na kasi kubwa ya  Wanawake kujitokeza katika maonyesho na kutujenga nyesha ujasiliamali na kuitikia kwa nguvu tarajio la Rais Samia la kutaka wanawake kujitokeza katika fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi "Nimeridhishwa sana na Wanawake kujitokeza katika maonyesho haya kuonyesha bidhaa mbalimbali za ujasiliamali hili ndio tarajio la Rais wetu Daktari Samia Suluhu Hassani kuona Wanawake wanajikwamua kiuchumi" alisema Seneda Maonyeshe ya nane Mkoani Mbeya yanatarajiwa kufungwa tarehe 08/08/2024