Machapisho

MWALIMU ADAIWA KUMLAWITI MWANAFUNZI CHOONI

Picha
 Baada ya kusambaa video mtandaoni, akimuonesha mtoto darasa la tatu akisimulia namna alivyofanyiwa ukatili na mwalimu wake, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima amesema hatua zimeshachukuliwa dhidi ya mtuhumiwa. Dk Gwajima  ametoa majibu kupitia  mtandao wake wa kijamii wa Twitter,akiandika "shtaka la mtuhumiwa lipo polisi RB namba ARS/RB/3429/2023. Wako watoa  huduma ambao wamevaa vazi la kondoo kumbe ni wanyama wakali dhidi ya watoto . Wazazi semeni na watoto msisubiri tukio limkute, semanae sasahivi hapo ulipo 'mwanangu marufuku mtu kuleta agenda za kugusa mwili wako wala kupita pembeni na kukueleza lolote kukuambia usiseme wala asikutishe ukanyamaza piga kelele toa taarifa'"aliandika. Hata hivyo katika maelezo yake amependekeza mbinu mpya kwa jamii, watoto kuwa na filimbi wakiona dalili za hatari ya mtu kutaka kushika mwili wake wapulize, kama mkakati moja wapo wa kukabiliana na vitendo hivyo. Kwa uchache katika vid...

MWANDISHI WA HABARI AVAMIWA NYUMBANI KWAKE, WEZI WAWEKA PASI KITANDANI

Picha
Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Kanda ya Kati, Sharon Sauwa amevamiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana na kufanya uharibufu wa mali na vitu mbalimbali wakati yeye  hayupo. Dodoma. Nyumba ya Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Kanda ya Kati, Sharon Sauwa imevamiwa, kuvunjwa na watu wasiojulikana kisha kufanya uharibifu mkubwa wa mali lakini hawakuchukua kitu. Tukio hilo lilitokea jana Jumamosi ya Aprili 1, 2023 asubuhi wakati Sharon akiwa kazini na tayari Polisi wamefungua jalada la uchunguzi DOM/RB/4252/2023 la kuvunja, kuharibu mali na kujaribu kuiba kwa ajili kubaini nini makusudi ya waharifu hao. Watu hao wanaokadiriwa walikuwa zaidi ya mmoja, walivunja vioo vya madirisha manne, milango miwili na kusambaza nyaraka mbalimbali walizozikuta ndani. ALSO READ Mwalimu adaiwa kumlawiti mwanafunzi chooni Mbali na uvunjaji huo, majiko ya umeme na swichi viliwashwa, pasi iliunganishwa...

RAIS DKT SAMIA AFANYA MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI

Picha
 

MAJALIWA :VIRIBA TUMBO VYAWA JANGA LA KITAIFATAIFA

Picha
  Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amesema kuwa tatizo la uzito uliozidi na kiriba tumbo limekuwa janga la kitafa katika mikoa ya Kilimanjaro, Dar es Salaam, Unguja na Mjini Magharibi huku udumavu nao ukishika kasi katika mikoa ya Iringa, Njombe na Rukwa.  Akizungumza leo Jumamosi Aprili mosi wakati akizindua mbio za Mwenge kitaifa alisema kuwa tatizo la kiliba tumbo ni kubwa katika mikoa ya Kilimanjaro  kwa asilimia 49, Dar es salaam kwa asilimia 48.6,  Unguja kwa asilimia 39.4 na Magharibi kwa asilimia 47.4 hali hii inaelekea kuwa janga kitaifa. Huku utapia mlo ukiwa katika mikoa ya Iringa 56.9, Mbeya 31.5, na Njombe 50.4 Rukwa 49.8 Geita 38.6, Ruvuma 35.6, Kagera 34.3, Simiyu 33.2 Tabora  33.1, Katavi 32.2, Manyara 32, Songwe 31.1. Mwenge ‘kunusa’ kila halmashauri maagizo 15 ya Waziri Mkuu Kitaifa 3 hours ago “Hali hii ya watu kuwa na uzito ulizidi ni janga la kitaifa na kisababishi cha kuongezeka kwa magonjwa kama ya moyo na kisukari, saratani nafikiri ni wakati...

ILEJE YAWANOA WAFANYABIASHARA MFUMO MPYA WA TAUSI

Picha
Wafanyabiashara wilayani Ileje mkoani Songwe watakiwa kutumia mfumo mpya wa TAUSI kulipia mapato Ili kuondoa ufujaji na upotevu wa fedha. Wito huo umetolewa Machi 29,2023 na mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Farida Mgomi wakati akizungumza na wafanyabiashara hao katika kikao Cha Baraza la biashara la Wilaya ambacho pamoja na agenda zingine, kulikuwa na lengo la kutoa elimu kwa wafanyabishara juu ya matumizi ya Mfumo mpya wa TAUSI. Mgomi amesema mfumo huo ni rafiki kama alivyo ndege Tausi ambapo kwa namna moja au nyingine utaweza kusaidia  kutatua chanagamoto za  ukusanyaji wa mapato sambamba na kupunguza hoja za Mkaguzi wa nje wa Hesabu za Serikali. Hata hivyo Mgomi ameitaka halmashauri kuwa tayari kuacha kutumia mfumo ule wa zamani wa LGRCIS na kuingia kwenye mfumo mpya wa TAUSI "Hakikisheni mnasajili pos zote kwenye mfumo mpya wa Tausi  na makusanyo ya fedha zote zinapelekwe benki", amesema Mgomi. Mgomi amesema serikali imekuwa ikiboresha mazingira rafiki kwa wafanyabiashara hiv...

MADEREVA NEW FORCE NA SAULI WAKAMATWA KWA KUFUKUZANA, DEREVA SUPER FEO ALA NDUKI KUKWEPA POLISI

Picha
  Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoani Iringa, Moss Ndozero baada ya kuwanasa madereva wa mabasi ya Saulu,Super Feo na New Force wakifukuzana Muktasari: Mtindo wa madereva kupeana ishara ya eneo lenye askari na hivyo kupunguza mwendo umewaponza madereva wa mabasi ya Sauli, Super Feo na New Force baada ya kuwekewa mtego. Iringa. Madereva wa mabasi ya Sauli, Super Feo na New Force wamekamatwa kwa tuhuma za kuendesha mwendo wa kasi, huku wakikimbizana baada ya Mkuu wa Usalama Barabarani (RTO) mkoani Iringa, Mosi Ndozero kuwawekea mtego. Awali, Ndozero alipata taarifa za mwendo wa kasi wa mabasi hayo, hivyo akaamua kuweka mtego uliosababisha wakamatwe licha ya madereva waliokuwa wanapishana nao kuwaambia, eneo hilo hakuna askari.  Kwa sababu hawakubaini mtego huo, ishara kutoka kwa madereva wenzao zilionyesha mbele yao hakuna askari. Akizungumza baada ya kuyakamata mabasi hayo jana Machi 29, 2023, katika Mji wa Mafinga, wilayani Mufindi, Ndozero amesema awali alipokea taarifa kwamba ...

MBOZI NA MOMBA ZAPATA HATI SAFI RIPOTI YA CAG

Picha
Halmashauri za Mbozi na Momba zilizopo Mkoani Songwe ni miongoni mwa halmashauri zilipopata hati safi huku Halmashauri ya Songwe ikiwa ni halmashauri pekee iliopata hata yenye mashaka kulingana na ripoti ya CAG. Rais wa Dkt Samia Hassan amewataka Viongozi na Watendaji wa serikali kuzisoma na kuzielewa vyema taarifa za rushwa na za ukaguzi wa hesabu za serikali ili ziwasaidie kujitathimini. Kwa mujibu wa taarifa ya CAG Halmashauri  za Mbozi,Momba, Tunduma na Ileje zimefanikiwa kupata hati safi huku Halmashauri ya Songwe ikiambulia hati yenye mashaka na kuwa ni halmashauri moja tu katika Mkoa wa Songwe yenye hati yenye mashaka. Wakiongea kwa nyakati tofauti juu ya mapokeo ya hati hizo baadhi ya wakurugenzi wamewashukuru Madiwani na Watumishi wa halmashauri zao pamoja na Wananchi. "Kiukweli sisi Mbozi tumefarijika sana kwa hii hati tuliopata na kwa upande wangu binafsi hii ni hati yangu ya kwanza kupata toka nimeletwa kuwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Mbozi lakini hizi sio juhudi zan...

DC AKAGUA VIFAA TIBA HOSPITALI YA WILAYA YA SONGWE

Picha
Mkuu wa Wilaya ya Songwe Mhe. Solomon Itunda ameiongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Abdallah Mgonja kukagua vifaa tiba vya kisasa vinavyoendelea kuletwa katika Hospitali ya Wilaya ya Songwe. Kufuatia ukaguzi huo, Mhe. Itunda amempongeza Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan  Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Wilaya ya Songwe shilingi bilioni 3.5 za ujenzi wa Hospitali hiyo pamoja na vifaa vya kisasa vyenye thamani ya Tsh milioni 247. Mkuu wa Wilaya huyo ameielekeza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha wanatunza vifaa na majengo hayo, sambamba na kutoa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia utu na miiko ya kazi yao.

AFUNGWA MAISHA AKIPINGA KIFUNGO CHA MIAKA 30

Picha
 Rufaa ya pili aliyokata mkazi wa Kijiji cha Mwanambaya, Wilaya ya Mkuranga, Denis Joseph, kupinga kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kumbaka na kumlawiti mwanafunzi imegeuka msiba baada ya kujikuta akiambulia kifungo cha maisha. Mahakama ya Rufani imekubaliana na Wakili wa Serikali, Elizabeth Olomi kuwa adhabu ya kifungo cha miaka 30 alichopewa Joseph, maarufu kama Saa Moja kwa shitaka la ulawiti ilikuwa kinyume na sheria. Wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, Olomi aliikumbusha Mahakama kuwa kifungo alichopewa Joseph kilikuwa kinyume na kifungu cha 154 (2) cha Kanuni ya Adhabu kinachotoa adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu yeyote anayetiwa hatiani kwa kulawiti mtoto cha umri wa chini ya miaka 18.  wanaotuhumiwa kulawiti, kumrekodi aliyelawitiwa “Katika kesi iliyo mbele yetu, kwa kuwa mwathirika wa kosa hilo alikuwa na umri wa miaka 10 siku ya tukio, kifungo sahihi kilitakiwa kiwe kama kilivyotamkwa na sheria. “Kwa hiyo, tunatumia mamlaka tuliyopewa kuweka kando kifungo cha mi...

MALAWI WARIDHISHWA NA USHIRIKISHWAJI WA JAMII KATIKA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI ILEJE

Picha
Timu ya utekelezaji wa Mradi wa Bonde la Mto Songwe kutoka Wilaya ya Chitipa-Malawi imepongeza namna wananchi wanavyoshirikishwa katika mradi huo upande wa Tanzania katika wilaya ya Ileje. Pongezi hizo zimetolewa na watalaam hao wakiongozwa na Mkuu wa msafara Mhe.MaCMillan Magomero ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Chitipa wakati wa majumuisho katika Kata ya Malangali-Ileje. Mhe.Magomero amesema kuwa maelezo waliyoyapata toka kwa wananchi tangu mwanzo katika vijiji vya Ilondo,Bulanga na Malangali yanakidhi maelezo ya mezani waliyokuwa wameyapata siku ya mwanzo katika kikao kwenye Ukumbi wa VIM. Naye Franklin Mwalwanda Ofisa mmoja wa wageni hao ameeleza kufurahishwa kwake na namna  wanawake wanavyoshikishwa katika  mradi huo akisema kuwa kwa kufanya hivyo ni utekelezaji wa agenda ya kimataifa ya kuwawezesha wanawake. Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe.Farida Mgomi ameshukuru viongozi wa juu wa mataifa haya mawili kwa kuruhusu ushirikiano huo kuwepo akisisitiza kuwa atasimamia na kuhakikisha...

BARABARA KM 5 MBIONI KUANZA KUJENGWA LANDANI-KIWIRA ILEJE.

Picha
MKANDARASI aliyepewa kazi ya kujenga barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Kilomita 5 kwa gharama ya shilingi bilioni 5.7 ya Kiwira-Landani wilayani Ileje mkoani Songwe atakakiwa kumaliza mradi huo ndani ya mwaka mmoja kama mkataba unavyolekeza. Akimkabidhi mkandarasi atakayetekeleza mradi huo Machi 21,2023 kutoka Kampuni ya IRA GENERAL ENTERPRISES COMPANY LIMITED mkuu wa wilaya hiyo Farida Mgomi amemtaka mkandarasi huyo kufanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa. Mgomi amesema tayari serikali imemlipa mkandarasi huyo asilimia 15 ya fedha ili kumwezesha kuanza kazi bila kisingizio cha kukosa fedha na matarajio ni kutaka adha ya mzunguko wa kilomita 38 upungue na kuanza kutumia barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 5. “Kukamilika kwa barabara hiyo kutaongeza pato la halmasahuri na Taifa kwani uzalishaji utaongezeka mara dufu, na wawekezaji wataongezeka”, amesema Mgomi.. Meneja wa TARURA Mkoa wa Songwe Mhandisi  Kilian Daudi Haule amesema maagizo yaliyotolewa ya kuwasimaia wakanda...

BARABARA YA ISOKO-KATENGELE KUJENGWA KWA ZEGE

Picha
Kutokana na Barabara ya Isoko-Katengele kuwa na miinuko mikali pamoja na kona kali zipatazo 62, Wakala wa Barabara za vijijini na mjini (TARURA) imeanza kujenga Barabara hiyo kwa kutumia zege kwa sehemu zote ambazo zina kona kali na miinuko ili kurahisisha mawasiliano kwa watumiaji wa Barabara haswa wakazi wa Kata ya Kafule, Sange, Ibaba, Ngulugulu na lubanda ambao wamekuwa wakipata adha kipindi cha mvua kwenda katika Hospitali kongwe ya Isoko ambayo imejengwa enzi za ukoloni 1889 pamoja na kusafirisha mazao yao.   Meneja wa TARURA Wilaya ya Ileje, Mhandisi Lugano Mwambingu amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamilia  kwa dhati kuwaondolea changamoto ya mawasiliano wananchi wanaotumia Barabara kwa kutoa fedha za matengenezo milioni 649, 882,000. Mhandisi Mwambingu amesema kazi nyingine zinazofanyika ni pamoja na kukata magema ya Barabara kwa ajili ya utanuzi wa Barabara, kujenga gabion na kuumba tuta kazi zote zinaendelea. "Kwa kuzingat...

MWALIMU ADAIWA KUMUUA MWENZIE DARASANI

Picha
  Mwalimu wa Shule ya Msingi Igaka, Samwel Subi anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Geita kwa tuhuma za kumuua mwalimu mwezake Emanuel Chacha kwa kumchoma na kisu akiwa darasani. Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limetokea Machi 15 saa 3:45 asubuhi wakati walimu hao wakiandaa mtihani kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la kwanza. “Kata ya Isulwabutundwe mwanaume wa miaka 35 katika Shule ya Msingi Igaka aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kwenye chembe ya moyo na mwanaume mwingine mwenye miaka 35 ambae ni mwalimu mwenzake. Walimu wote wawili walikuwa darasani wakiandaa mtihani ndipo mtuhumiwa alitoa kisu na kumchoma mwenzake kwenye chembe cha moyo,” amesema Kamanda Jongo. Kamanda alisema chanzo cha tukio hilo inadaiwa kuwa ni ugomvi baina ya walimu hao ambao walikuwa wanagombea uongozi kwenye kitengo cha elimu ya kujitegemea. “Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea mwalimu amekamatwa na amekiri na sababu anadai aliona wal...

WATANO WAFARIKI UGONJWA USIOJULIKANA BUKOBA

Picha
  Wizara ya Afya imetangaza kuzuka kwa ugonjwa wa usiojulikana katika vijiji viwili, wilayani Bukoba Vijijini mkoani Kagera nchini Tanzania ambapo watu watano wamefariki dunia huku wengine wawili wakiendelea na matibabu hospitalini. Dodoma. Watu watano kati ya saba waliougua ugonjwa usiojulikana katika Wilaya ya Bukoba Vijijini Mkoani Kagera wamefariki dunia. Taarifa iliyotolewa jana Alhamis Machi 16, 2023 na Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu amesema ugonjwa huo umetokea katika vijiji vya Bulinda na Butayaibega vilivyopo katika kata za Marua Kanyangereko wilayani humo. Profesa Nagu amesema watu hao walipata dalili za homa, kutapika, kutokwa na damu maeneo mbalimbali ya mwili na figo kushindwa kufanya kazi. “Wengine (watu) wawili wako hospitali wanaendelea matibabu. Mwenendo wa ugonjwa huo unaashiria uwezekano kuwa ni ugonjwa wa kuambukiza,” amesema Profesa Tumaini bila kusema ni ugonjwa gani. Amesema Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu kuhusu mwenendo wa ugonjwa h...

DC ILEJE ASHIRIKI MAFUNZO YA UONGOZI KWA WAKUU WA WILAYA DODOMA.

Picha
  Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe. Farida Mgomi katika picha akishiriki  mafunzo ya uongozi yaliyoanza leo Machi 13_18,2023 Kwa wakuu wa wilaya za Tanzania Bara wakiwa katika Ukumbi wa Mtumba Jijini Dodoma. Mafunzo hayo yamefunguliwa rasmi na makamu wa rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Philipo Mpango. Mafunzo ya wakuu wa wilaya yameandaliwa na ofisi ya Rais Taimisemi Kwa ajili ya kuwajengea uwezo wakuu wa wilaya.

DC ILEJE AWAAGIZA MAAFISA UGANI KUTOA ELIMU KWA WAKULIMA

Picha
Baada ya kugawiwa pikipiki 29 Kwa maafisa Ugani wilayani Ileje mkoani Songwe mkuu wa wilaya hiyo Mhe.Farida Mgomi amewaagiza maafisa hao kuwatembelea wakulima mashambani kutoa elimu ya kilimo bora na si wakulima kuwafuata maofisini. Mhe.Mgomi ametoa maagizo hayo Machi, 11,2023 wakati akigawa pikipiki 29 Kwa maafisa ugani wanaohudumia kata 18 zenye vijiji 71 wilayani humo hafla ambayo imefanyika katika ofisi za halmashauri ya Ileje. Mhe.Mgomi amesema asilimia kubwa ya uchumi Kwa wananchi wa Ileje na mapato ya halmashauri hiyo hutokana na kilimo, hivyo pikipiki hizo zitumike kuwatembelea wakulima kubaini fursa na changamoto zinazowakabili Ili kuzipatia ufumbuzi. Mhe. Mgomi amesema Kila afisa ugani kwenye eneo lake ahakikishe anatambua fursa za mazao yanayostawi kwenye kata yake na kuweka mikakati namna ya kuwawezesha wakulima waongeze uzalishaji wa mazao hayo kibiashara ili kiwainue kiuchumi. "Pikipiki hizo hazijaja Kwa bahati mbaya bali zimekuja Kwa ajili ya kufikia 2030 kuongeza a...

DC ILEJE AZIASA AMCOS KUJENGA UAMINIFU KWA WAKULIMA WA KAHAWA

Picha
Wakati wilaya ya Ileje mkoani Songwe ikipambana kutengeneza mazingira rafiki Kwa wakulima wa mazao ya kimkakati ikiwepo Kahawa, Pareto, Iriki na mengine vyama vya ushirika vimeaswa kujenga uaminifu Kwa wakulima. Wito huo umetolewa Machi 8,2023  na mkuu wa wilaya hiyo Farida Mgomi wakati wa kikao Cha wadau wa kahawa kilichowakutanisha wakulima, viongozi wa Amcos na baadhi ya makampuni yanayonunuza zao la kahawa kikao kilichofanyika ukumbi wa halmashauri Ileje. Mgomi amesema viongozi wa AMCOS wanapaswa kusimamia maslahi ya wakulima wa Kahawa kuwapa fedha zao kwa wakati ili wakulima waongeze wigo wa kulima zao hilo. "Mazao yanunuliwe kupitia vyama vya ushirika Kwa mujibu wa Sheria na hairuhusiwi mtu yeyote kununua anavyotaka yeye kwa kuwarubuni wakulima na kuwadhulumu fedha zao", amesema Mgomi. Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Ileje Geodfrey Mnauye amesema ili kuongeza uzalishaji wa kahawa wazalishaji wa mbegu hiyo TACRI wanapaswa kuzalisha mbegu kwa wingi na yenye ubora ku...

HIZI HAPA BARABARA ZILIZOPENDEKEZWA KUPANDISHWA HADHI MKOANI SONGWE

Picha
 Kikao cha bodi ya barabara Mkoani Songwe kikiongozwa na Mwenyekiti ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Francis Michael kilichofanyika jana 06 machi 2023 katika ukumbi mdogo Mkuu wa Mkoa wa Songwe kimependekeza na kupitisha mapendekezo ya  baadhi ya barabara kupandishwa hadhi na kuanza kuhudumiwa na Wakala wa barabara tanroads badala ya Tarura. Katika kikaoa hicho kilichohudhuliwa pia na Mbunge wa Ileje ambae pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi Godfrey Kasekenya Mwenyekiti wa CCM Mkoa Songwe Radwell Mwampashe, Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa taasisi na Wajumbe toka taasisi mbali mbali kwa pamoja walilidhia hoja ya kuzipandisha hadhi barabara 6 ambapo kabla ya kufunga hoja Mkuu wa Wilaya ya Songwe Solomoni Itanda aliomba barabara mbili toka Wilayani Songwe zipandishwe hadhi hiyo lakini kikao kiliazimia barabara moja ya Kininga-ngwala  ndio iingizwe kwenye mpango huo na nyingine iletwe kikao kijacho. Hizi hapa barabara zilizopitishwa Itumbula-Namkukwe-Galula(Momba-Songwe Galula-Itindi-...

MAHAKAMA YAVUNJA NDOA YA KAFULILA

Picha
  Miaka mitano tangu wanandoa waliobobea katika siasa David Kafulila na Jesca Kishoa kutengana, Kituo Jumuishi cha Mahakama kilichopo Mahakama ya Wilaya ya Temeke imetoa hukumu ya kuvunja rasmi ndoa hiyo tangu Februari 20 mwaka huu. Dar es Salaam.  Kituo Jumuishi Huduma za Kimahakama, Mirathi na Ndoa, Temeke kimeivunja rasmi ndoa kati ya wanasiasa machachari David Kafulila na Jesca Kishoa kupitia shauri la ndoa No 217 ya 2022. Ndoa hiyo iliyofungwa Aprili 22, 2014 ilivunjwa rasmi Februari 20, 2023 baada ya wanandoa hao kutengana tangu mwaka 2019 kabla Mahakama ione ndoa hiyo imevunjika kiasi cha kutorekebishika. Wakati hati ya madai ikionyesha kiini cha mgogoro huo ni ugomvi na utengano, Mahakama imevunja ndoa baina ya wawili hao huku ikitoa amri kwa mama kubaki na watoto na kila mzazi kuwa na wajibu wa kuchangia gharama za matunzo kwa asilimia 50. “Maombi ya Jesca Kishoa akiitaka Mahakama ione ndoa kati yake na David Kafulila imevunjika kiasi cha kutorekebishika na kuomba amr...

TUNDUMA WAPEWA SIKU 14 KUKAMILISHA SOKO LA MAJENGO

Picha
Baada ya wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga kuitaka serikali kuharakisha ujenzi wa soko la Majengo halmashauri ya mji wa Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe katibu Tawala mkoani humo Happiness Seneda ameuagiza uongozi wa halmashauri hiyo kutumia wiki mbili kumaliza ujenzi huo. Seneda ametoa maagizo hayo baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kujionea mwenendo wa ujenzi wa soko hilo huku akisema imekuwa ni mara ya tatu kufika hapo na kukuta ujenzi hauendelei. Seneda amesema soko hilo likamilike mapema ili kuwa rahisishia wafanyabiashara kufanya kazi zao kwenye mazingira rafiki na salama kwa walaji. “Nimekuja hapa mara mbili na hili staki lijirudie tena ndani ya wiki mbili majengo yakamilike ,hivyo nakuja baada ya hizo wiki mbili kama mtakuwa hamjakamilika sitakuwa na msamalia mtume”, amesema Seneda. Mkuu wa wilaya hiyo Faki  Lulandala amesema kuanzia sasa atakuwa anashinda eneo la ujenzi kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama kuhakikisha ujenzi wa soko hilo...

WANANCHI ILEJE WAMKATAA MWENYEKITI WA KIJIJI

Picha
Wananchi wa kijiji cha Shinji kata ya Mbebe wilayani Ileje mkoani Songwe wamesema hawana Imani na mwenyekiti wa kijiji hicho Ali  Kalinga akishutumiwa kuwamilikisha baadhi ya wananchi wakiwepo ndugu zake eneo lililotengwa na wananchi kwa ajili ya matumizi ya malisho Zaidi ya hekari 50. Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara na Kaimu afisa Tarafa ya Bulambya Frank Mwampamba ambaye alimwakilisha mkuu was wilaya hiyo Farida Mgomi walisema mwenyekiti huyo alihusika kugawa maeneo hayo bila kushirikisha wajumbe wa halmashauri ya kijiji na wananchi waliopitisha kutenga eneo hilo tangu miaka ya nyuma. Lingisoni Sikanyika mkazi wa kijiji hicho alisema mwenyekiti huyo alitumia madaraka yake kuwagawia kwa nguvu baadi ya ndugu zake na kushindwa kuwaondoa wananchi wengine waliovamia eneo Hilo  Zaidi ya hekari 20. Sikanyika alisema mwenyekiti wetu atupishe kwenye kiti tumeshindwa kuendelea kufanya naye kazi kwani yeye yupo mbele kuharibu matumizi bora ya mpango aridhi ya kijiji ambayo wanan...

MKUU WA POLISI(OCD),OFISA UPELELEZI (OC CID)WASIMAMISHWA KAZI KWA UNYANYASAJI

Picha
  Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni amewasimamisha kazi Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) na Ofisa Upelelezi Wilaya ya Kilombero baada ya kulalamikiwa na wananchi kuwa wanawanyanyasa. Kilombero. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni amewasimamisha kazi Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD), SSP Shedrack Kigomanya na Ofisa Upelelezi Wilaya ya Kilombero, SP Daud Mshana baada ya kulalamikiwa na wananchi kuwa wanawanyanyasa.  Masauni amechukua hatua hiyo jana Jumatatu, Februari 20, 2023 akiwa kwenye ziara wilayani Kilosa ambapo pamoja na kukagua baadhi vituo vya polisi na magereza yaliyopo pia alizungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara. Waziri Masauni pia amemwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillus Wambura kuwachunguza na kuwahamisha viongozi hao ili kujenga imani kwa wananchi na pia kuimarisha dhana ya uwajibikaji. Vile vile amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama kuwahamisha askari wote wanaotajwa kunyanyasa wananchi na kuleta askari w...

OFISI SERIKALI ZA MITAA ZAONGOZA KUTOLEWA MALALAMIKO MKOANI SONGWE

Picha
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushw (TAKUKURU) Mkoa wa Songwe imefanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo 68 yenye thamani ya shilingi bilioni 11.564 katika Halmashauri zote za Mkoa wa Songwe na kubaini kasoro kadha, ikiwemo fedha za mikopo ya asilimia 10 kwa ajili ya Wanawake, Vijana na Walemavu. Taarifa hiyo ilitolewa jana na Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Songwe, Mohamed Shariff, kwa waandishi wa Habari, wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa ofisi hiyo katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Oktoba hadi Disemba 2022. Alisema katika miradi yote iliyofuatitiliwa  baadhi ya miradi ilibainika  kuwa na upungufu ambapo taasisi hiyo ilichukua hatua mbalimbali kwa wahusika kwa lengo la kuzia vitendo vya rushwa na ubadhirifu. Miongoni mwa miradi iliyobainika kuwa na upungufu ni ile ya sekta ya Afya kwenye ujenzi wa zahanati na vituo vya afya,ujenzi wa vyumba vya madarasa katika sekta ya Elimu, pamoja na Miundombinu ya barabara. Eneo lingine ambalo TAKUKURU ilifanya ufuatilia...

MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE ADAIWA KUJINYONGA

Picha
  Mwanafunzi wa darasa la nne Shule ya Msingi Kambarage Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Mkoa wa Pwani, Tatu Machemba amepoteza maisha ikielezwa kuwa amejinyonga kwa kutumia kamba chumbani nyumbani kwao Mtaa wa Mkoani mjini Kibaha, Pwani.  Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi leo Jumatatu Februari 20, 2023, Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkoani,  Shabani Rashidi amesema kuwa taarifa za tukio hilo zilimfikia juzi kwa njia ya simu na kabla ya kwenda aliwasiliana na Jeshi la Polisi. "Nilipigiwa simu nikijukishwa tukio hilo juzi na kabla ya kwenda niliwasiliana na Jeshi la Polisi tukaenda eneo la tukio nyumbani kwa familia hiyo," amesema Amesema kuwa baada ya kufika eneo la tukio waliingia na kukuta mwili wa mwanafunzi huyo kichwa chake kimechomekwa kwenye kamba na yeye amepiga magoti," amesema. Mwenyekiti huyo amesema kinacholeta maswali kwa baadhi ya wananchi ni mazingira yaliyokutwa kwani mwili wa marehemu haukuwa unaning'inia bali alikutwa amepiga magoti. "Sasa hali hiyo...

POLISI SITA WAFUKUZWA KAZI

Picha
 Jeshi la Polisi mkoani Arusha limewafukuza kazi askari wake sita katika kipindi cha miezi sita, kutokana na makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu yasiyoendana na maadili ya jeshi hilo. Arusha. Jeshi la Polisi mkoani Arusha limewafukuza kazi askari wake sita katika kipindi cha miezi sita, kutokana na makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu yasiyoendana na maadili ya jeshi hilo. Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake leo Febuari 20, 2023 bila kuwataja majina ya askari hao, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Justine Masejo amesema kuwa askari hao walifukuzwa kazi katika kipindi hicho baada ya uchunguzi wa kijeshi kukamilika kutokana na makosa yaliyokuwa yakiwakabili. Amesema kuwa utaratibu wa kuchukuliana hatua za kinidhamu ndani ya Jeshi la Polisi ni jambo la kawaida hasa kwa askari wanapokiuka maadili ya jeshi hilo "Katika kipindi cha miezi sita tumewafukuza askari wetu sita, wakikabiliwa na makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu, kama mnavyojua askari wetu wanaoajiriwa wanatoka kwe...

WEZI WAVAMIA NYUMBANI KWA KAMANDA WA POLISI WAIBA BUNDUKI

Picha
  Wezi katika kaunti ya Busia walivaamia nyumbani kwa kamanda huyo usiku wa manane na kuiba bunduki aina ya Czeska, polisi wameanza upelelezi wa tukio hilo. Kenya. Polisi katika kaunti ya Busia wameanza msako kutafuta bastola aina ya Czeska iliyoibwa kwenye nyumba ya kamanda wa polisi wa kaunti hiyo usiku wa Jumamosi, Februari 18 ambapo wezi mbali na bastola waliiba redio na mtungi wa gesi. Inasadikika wezi hao walinyunyiza dawa ya kulewesha kupitia dirisha la chumba alichokuwa amelala kamanda huyo kabla ya kutekeleza tukio lao kkitu ambacho kilimsababishia maumivu ya kichwa na kupata kiznguzungu alipoamka. Kamanda wa polisi wa kaunti hiyo ya Busia, Bishar Muhumed SSP amethibitisha kutokea kwa tukio hilo usiku wa jana na wezi hao walipora vitu ikiwemo bastola anayomiliki kamanda huyo. Maofisa wa usalama wametembelea eneo la tukio na kikosi cha wapelelezi wakiwa na mbwa wa kundi la K9 kwa ajili ya kuchukua harufu ambapo aliwapeleka barabara inayokwenda Uganda lakini huyo alipoteza d...

MAJAMBAZI YATEKA GARI LA MAITI SONGWE YAPORA SIMU NA FEDHA

Picha
  Jeshi la Polisi Mkoani Songwe limethibitisha Majambazi kuteka gari la Serikali lililokuwa limebeba maiti ya mwanafunzi katika Msitu maarufu wa Nyimbili uliopo kata ya Ntungwa tarafa ya Kamsamba Wilayani Momba. Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake kamanda wa polisi Mkoa wa Songwe (ACP)Theopista Mallya amesema siku ya Februari 16,2023 katika misitu wa Nyimbili uliopo barabara ya Mlowo Kamsamba unaounganisha Wilaya za Momba na Mbozi mida ya saa saba na nusu usiku gari la Serikali  SM 14056 likiwa limebeba maiti ya mwanafunzi wa shule ya Msingi Itumbula kwenda Kijiji cha Msanyila Mbozi aliezama katika bwawa wakati anaogelea na kwenye hili gari alikuwemo Afisa Elimu wa kata ya Ivuna ambae jina lake halikutajwa na wenzie watano wakisafirisha mwili wa marehemu lakini walipofika eneo la Msitu wa Nyimbili walikuwa Magogo yamewekwa mbele yao na hapo ndio walipotekwa na Majambazi na kuporwa fedha 216,000 pamoja na simu zao vyote thamani yake ni 1,200,000 zote kwa pamoja. Kamanda...