Posts

Showing posts from January, 2023

TABIA ZA WABUNGE MKOA WA SONGWE ZAMKERA MWENYEKITI CCM MKOA

Image
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Songwe Radwell Mwampashe ameshangazwa na baadhi ya Wabunge Mkoani Songwe kutofika ofisi za Chama kujitambulisha kwa  Uongozi wa chama ambao uchanguzi wa Viongozi hao ulifanyika mwishoni mwa mwaka 2022.Akiongea atika hafla ya kuapishwa kwa Wakuu wa Wilaya wapya Wilaya  za Mkoa wa Songwe waliopata uteuzi wa Rais hivi Karibuni hafla iliofanyika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Songwe makao makuu ya Mkoa Mbozi. Radwell amesema Wabunge wa Mkoa wa Songwe baadhi hawajui sababu hawajafika katika Ofisi yake kujitambulisha na amemueleza Mhe Mlugo kama Mwenyekiti wao kuwafikishia salamu zake Wabunge hao kwani itafika kipindi  chama kitashindwa kuwasaidia pindi wanapopata changamoto. "Mhe Mlugo wewe huwa nakuona na umefika ofisi za Chama wengine nawashangaa hawataki kuja kujitambulisha na kufika ofisini kwangu waambie utafika muda wao wa kututafuta maofisini"alisema Mwenyekiti Radwell Aidha upande wa Wananchi baadhi ya Wanachama wa CCM waliokuwepo nda

BARAZA LA MADIWANI LAMKATAA MENEJA RUWASA

Image
  Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Kaliua limeazimia kutofanya kazi na Mapambano Mashini ambaye ni  kaimu meneja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini na Vijijini (Ruwasa) wilayani  Kaliua kwa madai ya kulidharau baraza hilo. Tabora. Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua limeazimia kutofanya kazi na Mapambano Mashini ambaye ni  kaimu meneja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini na Vijijini (Ruwasa) wilayani  Kaliua kwa madai ya kulidharau baraza hilo.  Uamuzi huo umesomwa kwa niaba yao na mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, Japhael Lufungija baada ya kumjadili na  kufikia uamuzi huo ulioungwa mkono na wote. Katika kikao hicho, baraza lilikuwa linataka kusikiliza  na kutoa maoni kuhusu rasimu ya bajeti  ya Ruwasa kama utaratibu unavyotaka na kaimu meneja huyo baada ya kuulizwa amejipangaje kuhusu kuwasilisha bajeti hiyo ili madiwani waweze kutoa maoni yao, alijibu hana cha kufanya na kwamba mwenye uamuzi ni bodi ya Ruwasa Taif

RAS SENEDA NA DC MOMBA WATEMBELEA GYM YA TUNDUMA WAMPA BIG UP MWEKEZAJI

Image
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Bi Happyness Seneda akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Momba Fakii Lulandala pamoja na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama Wilaya  wametembelea Gym ya Mwaitebele  iliopo Tunduma Msikitini jirani na Kisimani ambapo wakiwa hapo walipata fursa ya kufanya mazoezi ya viungo kwa kutumia mashine mbalimbali zilizopo ndani ya Gym hiyo. "Nimefika ndani ya Mkoa huu wa Songwe hii gym ni kiboko ni kubwa na ina kila kitu nitoe wito kwa Dc Momba himiza Watumishi wetu na Wananchi hata mara moja kwa wiki wajenge Utamaduni wa kuja hapa kufanya mazoezi na Mimi nitatenga siku niwe nakuja hapa kufanya Mazoezi" Seneda. Aidha Seneda amempongeza Mwaitebele kwa uwekezaji huo ndani ya Mkoa wa Songwe na kutaka wadau wengine waige mfano huo katika maeneo ya Mkoa huu Ili kuwajengea Wananchi sehemu ya kujenga miili yao na kuimalika kiafya. Fa

SERIKALI KUWAPA WATENDAJI WA KATA PIKIPIKI

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki amesema Pikipiki zipatazo 916 zitagawiwa kwa Watendaji wa Kata ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. Waziri Kairkuki ameyasema hayo Januari 20, 2023 wakati alipomuwakilisha Makamu wa Rais katika hafla ya kuufahamisha umma mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika Mkoa wa Dodoma. Akijibu ombi la Mtendaji wa Kata ya Uhuru katika Jiji la Dodoma Christina Mpete kuhusu uwezeshaji wa vyombo vya usafiri hususani ni Pikipiki kwa watendaji hao ili waweze kutekeleza majukumu yetu ipasavyo Mhe. Kairuki amesema  “niwape habari kuwa ombi hilo limekuja wakati muafaka ambako Serikali imeshanunua Pikipiki hizo zitagawiwa wakati wowote kuanzia sasa na tunaenda kwa awamu kwa sasa watendaji 916 watapatiwa Pikipiki hizo.

MENEJA LATRA SONGWE AFANYA UKAGUZI WA NAULI NA TIKETI STENDI VWAWA

Image
     (Meneja wa latra Songwe Joseph Bulongo akikagua tiketi kwa abiria) Meneja wa latra Mkoa wa Songwe Joseph Bulongo amefanya ukaguzi wa magari ya abiria a katika stendi ya mabasi wilaya ya Mbozi ambapo amebaini makosa mbalimbali yakiwemo mabasi kutotumia tiketi za kietroniki pamoja na kutoza nauli kinyume na taratibu. "Nimekuja hapa mwenyewe baada ya kupigia simu na abiria kuwa amekatiwa shilingi 700 na daladala toka Hanseketwa mpaka Vwawa badala ya shilingi 500 tumeikamata Daladala na abiria amerudishiwa cheji yake na tumeipiga faini daladala hiyo"amesema meneja Katika hatua nyingine Latra imefanya ukaguzi kwenye mabasi yaendayo  Mkoa jirani wa Rukwa ambapo katika ukaguzi wa baadhi ya mabasi yamekutwa hayajatumia tiketi za mfumo wa kieletroniki na baadhi zikiwa zimeandikwa kwa mikono. ( Meneja akiwaelekeza makondakta jinsi ya kutumia simu janja Ili kujua bei halisi za nauli Mikoani) Sambamba na hayo Meneja wa latra alitoa elimu kwa makondakta kutumia simu janja Ili kujua v

WATOTO WATATU FAMILIA MOJA WATEKETEA KWA MOTO

Image
 Watoto watatu familia moja walivyoteketea kwa moto Rombo Eneo la sehemu ya nyumba iliyoungua na  kuteketeza watoto watatu wa kiume katika kijiji cha Lessoroma, wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro. Rombo. Ni tukio linaloweza kudumu katika kumbukumbu ya maisha ya Karesma Theodory (39) wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro, baada ya kushuhudia watoto wake watatu wakiteketea kwa moto. “Nilisikia watoto wakiniita, mama mama huku moto ukiwa umeshika kasi,” alisimulia Karesma ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Lessoroma wilayani Rombo na kueleza namna alivyojitoa mhanga kuwaokoa wanawe pasipo mafanikio. Tukio hilo lililoibua simanzi, lilitokea usiku wa kuamkia juzi kijijini humo kwa kile kinachodaiwa chanzo ni kibatari ambacho watoto walikuwa wakikichezea ndani ya nyumba yao. Watoto hao waliofariki dunia kwa kuteketea kwa moto wakati mama yao akiwa ametoka nje akiongea na simu na mume anayeishi nchini Kenya ni Erick (9), Joshua (7) na Gidion Theodory (2). Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maiga

HAKIMU AUWAWA KWA KIPIGO CHA WANANCHI RUNGWE

Image
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, Dk Vicent Anney amesema watu wawili wameuawa  akiwemo hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Handeni, Joachim Mwakyoma baada ya kupigwa na  wananchi wenye hasira. Mbeya. Mkuu wa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, Dk Vicent Anney amesema watu wawili wameuawa  akiwemo hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Handeni, Joachim Mwakyoma baada ya kupigwa na  wananchi wenye hasira. Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumapili Januari 22, 2023, Dk Anney amesema tukio hilo limetolea katika kijiji cha kibole halmashauri ya Busokelo. Amesema hakimu huyo alikuwa ameambatana na wenzake wawili kwenda kwenye shamba lenye mgogoro na wanakijiji walishinda kesi katika  Mahakamani Kuu  Desemba mwaka 2022  baada ya kesi hiyo kusikilizwa mahakamani kwa miaka zaidi ya 10. Dk Anney amesema taarifa za awali zinaeleza kuwa kitendo cha hakimu na wenzake kuingia katika shamba hilo kiliwashtua wananchi waliowafuata na kuwahoji na yakaibuka malumbano. Amesema  katika tukio hilo wananchi wawili

UZINDUZI SIKU YA WIKI YA SHERIA NCHINI KANDA YA SUMBAWANGA

Image
Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Rukwa wameiomba Wizara ya Katiba na Sheria, kupitia upya sheria iliyoanzisha mabaraza ya kata nchini, ili yafanye kazi kwa mujibu wa sheria, tofauti na ilivyo hivi sasa mabaraza hayo ya kata yamekuwa yakitoa hukumu kwa wananchi badala ya kufanya usuluhishi. Wakazi hao wameyatoa maombi hayo wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria Mjini Sumbawanga, Mkoani Rukwa, kwamba utendaji wa mabaraza hayo kwa kutokufuata kanuni, taratibu na sheria za nchi, migogoro ya ardhi imekuwa haiwezi kwisha katika maeneo mengi ya nchi. Wamesema ikiwezekana mabaraza hayo ya kata yafutwe, kwakuwa yamechangia kwa kiasi kikubwa kutengeneza migogoro miongoni mwa jamii, kwa kuwa tu wanafanya kazi ambazo sio za kwao. Msimamizi wa Baraza la ardhi la wilaya ya Sumbawanga, JUSTINA RWEZAURA, amekiri kweli mabaraza ya kata yamekuwa yakitoa hukumu ya mashauri yanayowafikia huko Vijijini, wakati sheria haijawapa mamlaka ya kutoa hukumu wanaposikiliza mashauri ya ardhi, badala yake mabaraza ya ardhi

SONGWE WATUMIA MAZOEZI KUHAMASISHA UANDIKISHAJI WANAFUNZI SHULEN

Image
Viongozi wa Mkoa wa Songwe kwa kushirikiana na wananchi, Taasisi binafsi na za Serikali wametumia mazoezi ya jogging kuhamasisha uandikishaji wa wanafunzi shuleni haswa kwa kidato cha kwanza ambao hadi sasa ni 76 ndio waliofanikiwa kuripoti shuleni. Mazoezi maalumu ya jogging ambayo yameitwa kwa jina la Back to School special jogging yenye lengo la kuhamasisha wanafunzi kujiandikisha shuleni yamefanyika leo, 21 Januari kwa Wilaya zote za Mkoa wa Songwe na kimkoa imefanyika wilayani Mbozi na kuongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe. Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Bi.Happiness Seneda   amewataka wazazi kuendelea kuwapeleka watoto shuleni hususani kidato cha kwanza ambao idadi kubwa ya wanafunzi bado hawajaripoti shule ikiwa mpaka sasa ni asilimia 76% ndio waliofanikiwa kuripoti, uku darasa la awali ni 82%, la kwanza ni 96%. "Tunataka watoto wote wafike shuleni ata kama hana sare, daftari au mahitaji yoyote ya Shule kwani Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tuweze kujua wana

ULAWITI,UBAKAJI NA MAUAJI KAMANDA SONGWE AWATUMA SALAMU KUPITIA JOGGING"JESHI LA POLISI TUMEJIPANGA"

Image
.    ( Kamanda wa Polisi Songwe akifanya mazoezi ya Viungo Uwanja wa CCM Mbozi)  Mamia ya Wananchi wa Mkoa Songwe wamejitokeza katika mazoezi ya pamoja Jogging iliofanyika Wilayani Mbozi mapema leo asubuhi katika Viwanja vya CCM Mbozi.kabla ya kuingia katika Viwanja hivyo kulitanguliwa na mbio fupi zilizoanzia boma la Halmashauri ya Mbozi mpaka Ilembo eneo maarufu kama Mtambwe. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe ACP Theopista Malya akiongea na mamia ya Wananchi wa Songwe waliojitokeza katika Jogging hiyo wakati wa salamu za Viongozi amekemea tabia ya mauaji husasani Wilaya ya Mbozi ambapo amesema jeshi la Polisi limejipanga vilivyo kuhakikisha linakomesha tabia hiyo ambapo pia amewaomba Wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo pindi wanapopata taarifa au kumuhisi mtu anajiuhusisha na tabia za kihalifu na pia kamanda amewasihi Wananchi pindi wanataka kurudi nyumbani usiku wawatumie bodaboda au bajaji wanaowafahamu vyema Ili kuepuka kufanyiwa vitendo vya kiharifu na hata kuuwawa ambapo ka

MUUAJI WA MFANYAKAZI WA TANESCO SONGWE NAE AUWAWA

Image
  Polisi Mkoa wa Songwe imesema mtu anayedaiwa kumuua kikatili mfanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Angela Shekinyau (33) usiku wa kuamkia Jumatatu ya wiki hii naye ameuawa wakati akijaribu kukimbia akiwa chini ya ulinzi. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Januari 18, 2023, Kamanda wa Polisi Mkoa Theopista Mallya amesema polisi walimkamata mtuhumiwa Isaya Juma Mazuge maarufu kwa jina la ‘Wa Uyole’. Kamanda huyo amesema baada ya kukamatwa alitoa ushirikiano kwa kuonyesha vitu vya marehemu Agela ikiwamo simu ya Iphone 11PRO MAX na kuwataja wenzake. Ameendelea kusema kuwa, mtuhumiwa huyo pia alikuwa na Bastola iliyotengenezwa kienyeji na kwamba waliikuta ikiwa na ganda la shotgun pamoja na mapanga. Amesema mtuhumiwa alikuwa ameficha silaha hizo kwenye Msitu wa Vwawa Day na baada ya kuonyesha ushirikiano aligeuka ghafla na kuanza kukimbia jambo lililowafanya polisi warushe risasi mbili juu na moja ilifyatuliwa kwake na hatimaye kumpiga na kusababisha kifo. Kamand

ASILIMIA 63 YA WANAFUNZI SONGWE HAWAJARIPOTI MASHULENI

Image
  Zaidi ya wanafunzi 13,000 sawa na asilimia 63 wa kidato cha kwanza mkoani Songwe waliochaguliwa kuanza masomo Januari 9 mwaka huu, hawajaripoti shuleni hadi leo Ijumaa. Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Happiness Seneda amesema hayo leo wakati akitoa salamu za mkoa katika kikao kazi cha wasimamizi wa elimu katika shule za msingi na sekondari mkoani hapa kuwa kunahitajika jitihada ili kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza waanze pasipo kuwa na visingizio. Amesema wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu ni kuwa ni 22,986 lakini hadi Januari 11 wanafunzi 7,772 ndiyo walioripoti, amewataka wazazi kuwapeleka wanafunzi hao shule bila kujali kama wana sare au hawana. Pia, Seneda amewataka walimu na viongozi wa elimu kuhakikisha wanatatua haraka changamoto za walimu na kuwapa mrejesho ili kutoa nafasi waweze kutimiza wajibu wao ipasavyo. "Uandikishwaji wa darasa la awali hadi jana (Alhamisi) ni watoto 23,860 kati ya wanafunz

WANNE WAFARIKI AJALINI MOROGORO

Image
  Watu wanne wamefariki dunia kufuatia ajali ya lori na gari dogo aina ya Toyota Spacio katika eneo la Kwambe Dumila wilayani Kilosa mkoani Morogoro na kusababisha barabara kufungwa kwa saa kadhaa. Akizungumza na Mwananchi Digital kwa simu leo Januari 14 Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Majid Mwanga amesema gari hilo ndogo lilikuwa na watu sita akiwemo dereva ambaye ni mtumishi wa Serikali. Mwanga amesema kwa sasa wanaendelea kufanya mawasiliano kujua ni mtumishi wa idara gani. Aidha amesema imetambulika kuwa waliokuwemo ndani ya gari hiyo woye ni familia moja, ambapo aliwataka madereva kuendelea kuwa makini wanapokuwa barabarani hasa kwa kipindi hiki cha Mvua. Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mtakatifu Joseph Dumila, Manyele Kapongo amesema wamepokea miili ya watu hao (marehemu) na majeruhi wawili. Kapongo amesema kwa sasa wanaendelea na matibabu ya majeruhi hao wawili ambao ni mama na mtoto. Aidha mashuhuda wa ajali hiyo wanasema kuwa magari hayo yaligongana uso kwa uso na ambapo gari ndogo

MKURUGENZI JIJI LA MWANZA ASHTAKIWA TAMISEMI

Image
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima 'amemshtaki' mkurugenzi wa jiji hilo, Sekiete Yahya kwa Wizara ya Tamisemi ambayo ndio mamlaka yake ya nidhamu, akimtuhumu kuhusika na uuzaji wa viwanja viwili vyenye thamani ya Sh1 bilioni. Mwanza. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima 'amemshtaki' mkurugenzi wa jiji hilo, Selemani Sekiete kwa Wizara ya Tamisemi ambayo ndio mamlaka yake ya nidhamu, akimtuhumu kuhusika na uuzaji wa viwanja viwili vyenye thamani ya Sh1 bilioni. Wakati barua ya mashtaka ikitua Tamisemi, Malima ameagiza watumishi wanne wa jiji hilo kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kwa tuhuma za uuzaji wa viwanja hivyo. Viwanja hivyo namba 194 na 195 vipo mtaa wa Rwegasore jijini Mwanza. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo  Ijumaa Januari 13, 2023,  Malima amewataja wanaosimamishwa kazi kwa nyadhifa zao kuwa ni mhasibu wa Jiji, mwanasheria, ofisa manunuzi na ofisa mipango. Watumishi hao wa umma wanadaiwa kuuza viwanja hivyo vilivyopo mtaa wa kibiashara

DED NA WENZIE 6 MBARONI KWA UHUJUMU UCHUMI

Image
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iramba mkoani Singida, Augustino Matomola na wenzake sita wamefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakituhumiwa kwa uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya ofisi. Kahama. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iramba mkoani Singida, Augustino Matomola na wenzake sita wamefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakituhumiwa kwa uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya ofisi. Watuhumiwa hao walifikishwa katika mahakama hiyo jana Ijumaa Januari 13 mbele ya Hakimu mkazi Mfawidhi, Edmund Kente na kusomewa mashitaka hayo wanayodaiwa kuyatenda wakiwa watumishi wa Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama na kusababisha hasara ya Sh138 milioni. Akisoma mashitaka hayo, wakili wa Serikali Satuninus Kamala amesema washitakiwa katika kesi hiyo namba 1/2023 walitenda kosa hilo mnamo Mei 14, 2019. Mbali na Matomola, wakili Kamala amewata

WATUMIA MAJI MLOWO WAMTOSA RASMI MAGESA,WACHAGUA VIONGOZI WAPYA

Image
 Kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Songwe Waziri Kindamba kutaka mamlaka zinazomsimamia Mwenyekiti wa jumuia wa watumi Maji Mlowo Poul Magesa kumsimamisha na kuviagiza Vyombo vimchunguze kutoka na malalamiko ya kutumia ubabe na lugha zisizofaa kwa Wananchi pia matumizi mabaya ya madaraka. Leo katika Ukumbi wa shule ya sekondari Mahenje umefanyika uchaguzi wa Jumuiya hiyo na kupata Viongozi wapya huku Jumuiya hiyo ikiagana na Magesa rasmi na kumaliza historia yake ya Uenyekiti wa Jumuiya hiyo huku akisubiria majibu ya uchunguzi dhidi yake unaofanywa na Vyombo vya dola na endapo itabainika basi safari ya kupelekwa mahakamani kwake haitokwepeka.  Katika hali ya kushangaza Mbunge wa Jimbo la Mbozi George Mwenisongole aliibuka katika Mkutano huo na kusema ameshangazwa na uwepo wa uchaguzi huo na yeye kutokupewa taarifa na amesema Mkuu wa Wilaya ya Mbozi na Ocd wa Mbozi wanapaswa kuwajibishwa kutokana na kile kinachodaiwa kumkumbatia na kumtetea Magesa ikiwa ni pamoja na kukalia kimya malala

KAMPUNI ZA SIMU ZAWAKANA WALIOPANDISHA VOCHA ZA SIMU

Image
 Siku chache tangu Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania, TCRA-CCC kukemea baadhi ya wafanyabiashara kupandisha bei ya vocha, Umoja wa Kampuni za Simu Tanzania (TAMNOA) umewataka wananchi kutonunua vocha kwa bei ya juu zaidi ya iliyochapishwa.   Dar es Salaam. Siku chache tangu Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania, TCRA-CCC kukemea baadhi ya wafanyabiashara kupandisha bei ya vocha, Umoja wa Kampuni za Simu Tanzania (TAMNOA) umewataka wananchi kutonunua vocha kwa bei ya juu zaidi ya iliyochapishwa. Januari 10, 2023, TCRA-CCC ilisema mtu yeyote anayeuza vocha kwa bei tofauti na iliyoidhinishwa anafanya kosa la jinai. Kauli hiyo imekuja baada ya malalamiko ya wananchi kupanda kwa vocha kutoka Sh500 hadi Sh550 au Sh600 wakati iliyokuwa ikiuzwa Sh1, 000 ikiuzwa kwa Sh 1,100 katika maeneo mbalimbali Tanzania. Kupitia taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana Jumatano Januari 11, 2023 na kusainiwa na Mwenyekiti wa TAMNOA, Philip Besim

BREAKING NEWS: RC SONGWE AMSIMAMISHA MWENYEKITI MAGESA AVIKABIDHI VYOMBO VIMCHUNGUZE

Image
  Kufuatia sakata la Mwenyekiti wa watumia Maji Mji wa Mlowo Poul Magesa kulalamikiwa na wananchi kufanya vitendo visivyoendana na Maadili ya kazi ikiwemo kuchukua kuwapiga watu faini na kutowapa risti Mkuu wa Mkoa wa Songwe Waziri Kindamba amemsimamisha Mwenyekiti huyo sambamba na kuviagiza Vyombo  ya usalama Mkoa wa Songwe shutuma zinazomkabili na ikibainika hatua kali zichukuliwe dhidi yake  Kindamba amesema amesikia malalamiko ya Wananchi na Serikali ya awamu ya sita ipo Kwa ajili ya kusikiliza Wananchi hivyo kitendo kinacholalamikiwa na Wananchi hakiwezi kuachwa hivyi hivyo ni lazima kichunguzwe na ikibainika  hatua zaidi zitachukuliwa  "Kwa sasa namsimamisha na kuviagiza Vyombo vya usalama kuchunguza shutma zake na ikibainika apelekwe vyombo vya sheria Ili sheria ichukue mkondo wake. Aidha Wananchi wa Vijiji vya Mbozi na Msuto wamejitokeza na kutoa malalamiko mapya kuwa aliwaamulu kufyeka mazao yao  ya mahindi na kuwapiga faini ya laki tatu na walipoomba risti aligoma kuwapa

BEI ZA VOCHA ZA SIMU ZAPAA MJI WA MLOWO,MKOA SONGWE

Image
Bei za vocha za mitandaa mbalimbali ya simu za mikononi zimepaa katika Mji wa Mlowo uliopo katika Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe sababu kuu ikiwa wauzaji wa jumla wamepandisha bei ya kujumlia vocha hizo. Katika maduka mengi ya Mji wa Mlowo vocha zimepanda ambapo vocha shilingi 500 inauzawa shilingi 600 na vocha shilingi 1000 inauzwa kati ya 1100 hadi 1200 kutokana na bei atakayokutajia muuzaji. Mwandishi wetu alishuhudia mteja wa vocha akiuziwa vocha ya mtandao mmoja Kwa shilingi 1200 na mnunuzi alipopuliza sababu alijibiwa kuwa wauzaji wakubwa wa vocha Mlowo wamepandisha bei za Vocha za Jumla. "Kiukweli Mji wa Mlowo inabidi Serikali itusaidie kuna wajanja wengi wanapandisha vitu watakavyo wao Mbolea wamejipandishia bei sasa Hadi vocha jamani tamaa hizi mbona zimezidi zamani walisingizia mafuta yamepanda bei sasa sijui watasingizia nini"alilalamika Suzana Mwamengo Mkazi wa Mlowo kwa Maswala. hata hivyo kuwatafuta wafanyabiashara wakubwa wa kujumlisha vocha Mlowo lakini asilimi

MBOZI WAZIDI KUJIIMARISHA KIMAZINGIRA WAZINDUA UPANDAJI MITI KATA YA NANYALA

Image
  Diwani wa kata ya Nanyala ambae pia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Mbozi George Mushani amezindua rasmi kampeni ya upandaji wa miti katika Tarafa ya Iyula ambapo Uzinduzi huo umefanyika katika kata ya Nanyala. Kabla ya kuzindua kampeni hiyo Mushani waliwaeleza Wananchi waliofika  katika Ofisi za kata ya Nanyala kuwa kampeni hiyo si kwa ajili ya Serikali tu bali ni faida kwa Wananchi na ustawi wa nchi ndio maana miti hiyo wanawapa wakapande kwenye  kaya zao na ni jukumu la kila Mwananchi kuitunza miti hiyo. "Niwaombe sana Wananchi tuitunze miti hii mpaka ikue ili utusaidie sisi na vizazi vyetu vijavyo" Katika hatua nyingine Mheshimiwa Mushani amaechangia kiasi cha shilingi laki mbili ili zitumike kununua miche mingine na nikatika kufunga mkono juhudi za agizo la Mkuu wa Mkoa wa Songwe Waziri Kindamba kupanda miti kumi Kila kaya vijijini na Miti mitano kaya za mjini. Katika Uzinduzi huo pia ukihudhuliwa na afisa tarafa ya Iyula  Edward Lugongo ambae ameendelea kuwasisitiza w

WAWILI MBARONI KWA KUVUNJA OFISI ZA TAKUKURU

Image
Ofisi hizo za Takukuru wilaya ya Handeni zilivunjwa Novemba 30 mwaka jana na watu wasiojulikana na kuibiwa bastola mbili na risasi 50. Handeni. Kufuatia tukio la kuvunjwa kwa ofisi ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) wilayani hapa na kuibiwa kwa bastola mbili na risasi 50.  watu wa wawili wamepandishwa kizimbani wakikabiliwa na makosa manne yanayohusu tukio hilo.  Watu hao wametajwa kuwa ni pamoja na James Alex (48) mkazi wa Vibaoni na Ally Waziri (24), Mkazi wa Bomani aliyekuwa mlinzi wa ofisi hiyo.  Akiwasomea mashtaka hayo leo Ijumaa Januari 6, 2023 katika mahakama ya wilaya Handeni, Mwendesha Mashtaka Seif Makono, mbele ya Hakimu, Veronica Siao amesema, watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashitaka ambayo ni pamoja na kuvunja ofisi usiku, wizi, kula njama ya kufanya uhalifu na kushindwa kuzuia uhalifu kufanyika kwa mshtakiwa Ally Waziri, ambaye alikuwa ni mlinzi wa ofisi hizo. Mwendesha mashitaka Makono ametaja makosa mengine kuwa ni kula njama na uzembe wa kushindwa kuz

TFS,MARMO WAING'ARISHA MBOZI AGIZO LA RC LA UPANDAJI MITI LAANZA KUTEKELEZWA KWA KASI

Image
.       ( Afisa Mazingira Wilaya ya Mbozi Hamisi Nzunda)   Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Songwe la Upandaji miti Mkoani Songwe linaonekana  kutekelezwa kwa vitendo na kasi kubwa Wilayani Mbozi ambapo karibu kila tarafa zinaendelea na zinduzi  mbalimbali za upandaji miti. Afisa mazingira Wilaya Mbozi Hamisi Nzunda amesema wao kama halmashauri wamelipokea agizo  la Mkuu wa Mkoa wa Songwe Waziri Kindamba na wameanza pia kuwashirikisha wadau mbalimbali ambapo tayari wamepata baadhi ya miche na wameanza kuigawa kwa kaya miche mitano na mingine mitano wanakaya watajinunulia       (Meneja Tfs Mbozi Fred Mgeni) "hili naomba niliweke sawa tuna baadhi ya wadau wamejitolea kutupa miche na sisi tunaigawa kwa Wananchi ni miche michache hivyo haiwezi kuwatosha wote hivyo niseme tu neno kwa Wananchi kuendelea kutafuta miche na kupanda kwani hatua ya ukaguzi kila kaya utafuata"-amesema Nzunda Aidha Nzunda amewashukuru wadau mbalimbali wanaojitolea miti ya kupanda katika kipindi hiki cha kampeni y

PANGUA PANGUA POLISI YAENDELEA IGP APANGUA MAKAMANDA

Image
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amefanya mabadiliko ya makamanda wa polisi wa mikoa katika kuboresha na kuongeza ufanisi wa utendaji kwenye mikoa mitatu. Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Januari 06, 2023 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime imeeleza kuwa katika mabadiliko hayo, IGP Wambura amemhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Muslim kwenda Kitengo cha Mipango Makao Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake ikichukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Alex Mukama ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe. IGP Wambura amemhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Theopista Mallya kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe. Aidha, amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Shadrack Masija ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu Namba Moja Mkoa wa Simiyu kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa.

VIONGOZI WA AMCOS MBOZI WASOMBWA NA POLISI KWA AGIZO LA WAZIRI BASHE

Image
  Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameagiza kukamatwa kwa viongozi chama cha msingi cha ushirika cha zao la kahawa cha Isansa baada wakulima kulalamika kutolipwa fedha zao licha ya kahawa yao kuuzwa.  Bashe aliyekuwa akiendelea na ziara katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, msafara wake ulisimamishwa na wakulima wa kijiji cha Isansa wilayani Mbozi ambao walimueleza changamoto hiyo ya kutopewa fedha zao. Mbunge wa Mbozi, George Mwenisongole alianza kwa kumweleza Bashe kuwa Amcos hiyo imekuwa ni mateso kwa wakulima kwa kushindwa kuwalipa fedha zao kwa wakati. “Nikuombe Waziri Bashe, hawa wakulima ni masikini hawana lolote la kufanya, wamepima kahawa yao, imeuzwa hadi sasa hawajalipwa hawajui wataishi vipi, hebu tusaidie,” alisema Mwenisongole. Katibu wa chama hicho cha ushirika, Sued Mgalla alipohojiwa na Waziri Bashe kama kahawa ya wakulima hao imeuzwa alijibu imeuzwa na fedha zipo benki. Sued alisema fedha walizopata kwa kuuza kahawa ya wakulima hao zilikuwa benki kwa sababu bado waliku

AFISA TARAFA MBOZI AGAWA MICHE 1000 YA MITI IKAPANDWE KWENYE KAYA KAMA AGIZO LA MKUU WA MKOA LINAVYOTAKA UPANDAJI MITI

Image
Zoezi la Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe Omary Kindamba la kupanda miti kila kaya ndani ya Mkoa wa Songwe likiendelea kutekelezwa maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Songwe. Wilaya ya Mbozi kupitia afisa Mazingira Hamis Nzunda wameanza kutekeleza kampeni hiyo kwa Tarafa za Wilaya ya Mbozi na zoezi hilo linaendelea kwenye Tarafa ya Iyula  Edward Lugongo afisa tarafa ya Iyula amezindua kampeni ya upandaji miti katika kata ya Ruanda iliopo Tarafa ya Iyula ambapo zaidi ya Miti 1000 imetolewa Kwa kaya mbali mbali katani hapo ambapo kila kaya imepata miti mitano na mingine mitano kila kaya itajighalamia yenyewe Ili kufikia kumi kama agizo la Mkuu wa Mkoa linavyotaka Kila kaya kupanda miti kumi. "Tunawapeni miti hii mitano mitano kama kuwahamisha lakini Kila kaya inatakiwa kupanda miti kumi na ni jukumu letu kuitunza miti hii na ifikapo tarehe 15 ya mwezi huu tutaanza kukagua kama kila kaya imepanda miti na atakae kaidi hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kupelekwa mbele ya vyombo vya sheri

RC SONGWE " TUTASHIRIKIANA NA VIONGOZI WA KIMILA KUKUZA VITUO VYA UTALII WA MKOA WA SONGWE ILI TUWEZE KUKUZA PIA UCHUMI KUPITIA UTALII"

Image
Mkuu wa mkoa wa Songwe, Waziri Kindamba amesema mkoa huo umejipanga kuvumbua vivutio vya kitalii ili kuimarisha uchumi kupitia sekta ya utalii. Kindamba amesema hayo leo Jumatano Desemba 4, 2023 wakati alipoambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo kutembelea baadhi ya maaeneo ya vivutio vya kitalii yaliyopo katika mkoa huo. Katika ziara hiyo, Mkuu huyo wa mkoa pia  ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe (RAS), Happiness Seneda na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbozi George Musyani. Wengine walishiriki katika ziara hiyo ni viongozi wa dini  akiwemo Shekhe Hilal Kipozeo na Mchungaji maarufu Richard Hananja na baadhi ya machifu. Miongoni mwa maeneo ambayo viongozi hao walitembelea ni pamoja na michoro na unyayo ya kale Nkangamo wilayani Momba, majimoto kata ya Nanyala na kimondo cha Ndolezi Kata ya Mlangali vyote vilivyopo wilaya ya Mbozi. Ziara hiyo ni utekelezaji wa mikakati ya mkoa huo ya kuboresha maeneo ya vivutio vya utalii na  kutunza misitu na vyanzo vya maji ili

RAIS ARUHUSU MIKUTANO YA HADHARA

Image
 Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameruhusu mikutano ya hadhara ikiwa ni miongoni mwa agenda za muda mrefu vyama vya upinzani kutaka mikutano hiyo iruhusiwe. Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameruhusu mikutano ya hadhara iiliyokuwa ikililiwa kwa muda mrefu na vyama vya upinzani kutaka ruhusiwe.  Leo Jumanne, Januari 3, 2023  Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Samia amesema; "uwepo wangu leo hapa mahali nimekuja  kufanya ruhusa ya mikutano hii, nimekuja kutangaza kuondoa zuio la kuzuia mikutano ya hadhara na ninasema kwamba, sasa linaondoka." Rais Samia amesema mikutano hiyo kisheria, ni haki haki kwa vyama vya siasa kuiendesha huku akisema kwa upande wa Serikali wamejipanga kutekeleza wajibu wao wa kulinda mikutano hiyo. Rais Samia akizungumza na viongozi wa kisiasa Ili kuendelea na mikutano hiyo, Rais Samia amesema jukumu sasa linabaki kwa vyama vya siasa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola kama sheria na kanuni zinavyoelekeza ili vipatiwe ulinzi. Rais a