Posts

Showing posts from March, 2024

JELA MAISHA KWA KOSA LA KULAWITI

Image
Mahakama ya Wilaya Singida ememuhukumu kwenda jela maisha kijana Mohamed Jumanne ambaye pia anajulikana kwa jina la Salanda, (22) Mkulima na Mkazi wa VETA, Kata ya Utemini, Manispaa ya Singida kwa kosa la kulawiti. Mshitakiwa Mohamedi alitenda kosa hilo Machi 27, 2023 kwa kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 7 katika maeneo ya VETA ambapo Jeshi la Polisi limefanya upelelezi wa tukio hilo na kumkamata mtuhumiwa huyo kisha kufikishwa mahakamani Mei 10, 2023. Aidha, Mahakama hiyo imetoa hukumu hiyo baada ya pande zote mbili za Jamhuri na upande wa Mshitakiwa kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo. Hukumu hiyo imetolewa Machi 27, 2024 mbele ya Mh. Fadhili Ennock Luvinga Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Singida.

WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI ILI KUTOKOMEZA UKATILI

Image
Wazazi na walezi wilayani Mbozi wametakiwa kuendelea kushirikana kwa ukaribu na Jeshi la Polisi ili kuweza kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinavyojitokeza kwenye jamii. Akizungumza wakati alipohudhuria Ibada ya misa takatifu ya Sikukuu ya Pasaka katika kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mbeya Parokia ya Mtakatifu Patrick, Machi 31, 2024, Kamanda wa Polisi mkoani Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Agustino Senga, alisema ni vyema wazazi na walezi kukaa karibu na watoto wao ili kujua ukatili wanaofanyiwa ili kubaini na kudhibiti ukatili huo mapema kwa kutoa taarifa Polisi kwani kufanya hivyo kutapunguza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto. Aidha, Kamanda Senga alisema ili kuwa na kizazi bora na chenye maadili na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto ni lazima kuimarisha malezi bora kwa watoto kwa kuwapa nafasi ya kuwasikiliza na kuwa karibu nao ikiwa ni pamoja na kufuatilia mabadiliko ya tabia zao.  “Haya maovu yanayotokea kati

RAIS AFANYA UTEUZI HUU

Image
 Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango, Dr. Migiro aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza  kabla ya mkataba wake kuisha na nafasi yake kuchukuliwa na Balozi Mbelwa Kairuki August 16,2023 akitokea China  ambako alikuwa anaiwakilisha Tanzanka kama Balozi Nchini humo. Rais amemteua Fakii Raphael Lulandala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, kabla ya uteuzi huu Lulandala alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM). Amemteua pia Dkt. Edwin Paul Mhede kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Mhede aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na anachukua nafasi ya Agnes Kisaka Meena ambaye amehamishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji. Wengine walioteuliwa ni Gilbert Kalima ambaye ametuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, kabla ya uteuzi huu Kalima alikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi. Rais Samia amemuhamisha pia Mha

SONGWE :WATANO JELA MIAKA SABA KWA WIZI WA BIA

Image
 *WATANO JELA MIAKA SABA KWA WIZI WA BIA.* Mbozi Songwe: Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Mbozi Machi 28, 2024 imewahukumu Wakazi 05 wa Vwawa Mkoani Songwe kifungo cha Miaka 07 Jela kila mmoja kwa kukutwa na hatia ya kuvunja na kuiba vinywaji vikali vya aina mbalimbali na Tv flat screen inch 43 kampuni ya LG mali hizo zikiwa na thamani ya shilingi 2,641,000/= Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Chami Changwe kwa Michael Nzunda, Samson Sichala, Allen Lwinga, Asheli Mlawizi na Steve Sanga ambao walikiri kufanya kosa hilo mnamo Machi 4, 2023 katika grocery hiyo maeneo ya Vwawa Kati Wilayani Mbozi. Watuhumiwa hao walikamatwa maeneo na tarehe tofauti tofauti mwaka 2023 ndani ya Mkoa wa Songwe, na hukumu hiyo imetolewa kwa watuhumiwa hao ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.

MBUNGE SENDEKA ANUSULIKA KUUWAWA KWA RISASI NA DEREVA WAKE

Image
  ARUSHA: Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole- Sendeka (CCM) amesema yeye na dereva wake hawakuumia katika jaribio la kuuawa baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana wakati akielekea jimboni kwake. “Ni kweli tumeshambuliwa na watu ambao haikuwa rahisi kuwafahamu kwa wakati ule. Walikuwa kwenye gari wakitufuata na tulipofika kati ya kijiji cha Ng’abolo na Ndido katika wilaya ya Kiteto walianza kutushambulia,” amesema Ole Sendeka. “Ni kama risasi nne au tano hivi tulizoona kwa sasa … nilianza kufyatua risasi muda ule walivyoanza kutufyatulia risasi na kwa bahati dereva alibadili mwelekeo na ndio pona yetu.” Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Lucas Mwakatundu amethibitisha kuwa tukio hilo limetokea jioni ya leo Ijumaa Machi 29, 2024, majira ya saa 12:45 jioni. Amesema polisi inaendelea na uchunguzi, hata hivyo Ole Sendeka na dereva wake wote ni wazima na hawakudhurika kabisa.

NITUMIE HELA KWENYE NAMBA HII” 11 MBARONI FAINI M.6, KIFUNGO MIAKA MITATU JELA DAR

Image
  DAR ES SALAAM, 29 Machi, 2024 MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu wakazi 11 wa Ifakara Morogoro kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya shilingi milioni sita kwa kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutoa taarifa za uongo mtandaoni. Washtakiwa hao ni Fredrick Kanepela, Julius Mwabula, Amiry Luwiso, Tareeq Sadrudin, Ashraf Awadhi, Frank Kifyoga, Samson Tandike, Michael Haule, Mussa Maganga, Helman Lwambano na Kelvin Mkapila. Hukumu hiyo ilitolewa Machi 26, Mwaka huu Mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mwandamizi Annah Magutu baada ya washtakiwa hao kusomewa na kukiri mashtaka yanayowakabili. Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi Magutu alisema hukumu hiyo imetolewa kwa washtakiwa 11 kati ya washtakiwa 23 wanaokabiliwa na kesi hiyo. Alisema washtakiwa hao 11 waliohukumiwa waliomba kuingia makubaliano ya kumaliza kesi kwa kukiri makosa yao yaani 'Plea bargaining. Awali washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao na jopo

UJENZI WA DARAJA LENYE KIVUKO CHA CHINI (UNDERPASS) MBOZI LAKAMILIKA ASILIMIA 65

Image
Ujenzi wa daraja la kivuko cha chini linalojengwa katika Kijiji cha lumbila almaarufu njia panda ya Iyula katika barabara ya Ruanda -Isongole Wilayani Mbozi Mkoani Songwe ambalo litakuwa na fursa mbalimbali za kibiashara ndani yake limefikia zaidi ya asilimia 65% huku likiwatarajia kuufungua mji wa Ruanda kutokana na aina ya ujenzi wa daraja hilo ,huku likienda kupunguza ajali kutokana na kuwa magari yatakuwa yanapita juu na watumiaji wa miguu wakipita chini. Hayo yamebainishwa na Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe Mhandisi Suleiman Bishanga huku akisema kuwa mradi huo ni moja kati ya miradi inayotekelezwa Mkoani Songwe ambao utaenda kubadilisha Mji wa Ruanda na kufungua fursa mbalimbali kWa wakazi na watumiaji wa barabara hiyo. Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi na watumiaji wa barabara ya Ruanda Isongole kupitia iyula ambako mradi huo unajengwa wameishukuru Serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa daraja hilo huku wakiom

MWENYEKITI WA KIJIJI JELA MIAKA MINNE KWA RUSHWA YA 60,000/=

Image
  Mahakama ya Wilaya Kiteto, Imemhukumu MAMBE MOHAMED MAMBE, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nasetan, Kata ya Engusero, Wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara. Mshtakiwa ametiwa hatiani na kuamriwa kwenda Jela miaka minne au kulipa faini ya shilingi 1,000,000/= kwa makosa ya kuomba na kupokea hongo kiasi cha shilingi 60,000/= kinyume na k/f 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 kama ilivyofanyiwa marejeo Mwaka 2022. Hukumu hiyo dhidi ya MAMBE MOHAMED MAMBE katika kesi ya jinai Na.20/2023, imetolewa na Mhe. Boniface Lihamwike, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kiteto, Machi 27, 2024. Mshtakiwa aliomba hongo ya sh. 60,000/= ili asimchukulie hatua za kisheria mwananchi ambaye alifanya mkutano wa wafugaji bila kibali cha serikali ya kijiji. Mshtakiwa ameshindwa kulipa faini na amepelekwa magereza kutumikia kifungo chake.

MKUU WA POLISI AHUKUMIWA KUNYONGWA

Image
  MAHAKAMA ya Iran, imemuhukumu kifo Mkuu wa Polisi kaskazini mwa Iran baada ya kushtakiwa kwa kuua mtu wakati wa maandamano yaliyotokea nchini humo mwaka 2022. Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kuwa, Mkuu wa Polisi, Jafar Javan mardi, alikamatwa mwezi Desemba mwaka 2022 kutokana na mauaji ya mwandamanaji wakati wa maandamano makubwa yaliyochochewa na kifo cha Mahsa Amini akiwa chini ya ulinzi wa polisi. Amini mwenye umri wa miaka 22, alifariki mwezi Septemba 2022 akiwa chini ya ulinzi wa polisi kufuatia kukamatwa kwake kwa madai ya kukiuka sheria kali ya nchi kuhusu mavazi kwa wanawake.

MASHABIKI WA SIMBA TOKA TUNDUMA WAPATA AJALI MMOJA ADAIWA KUFARIKI

Image
Simba imeeleza kupokea kwa masikitiko taarifa ya ajali za mashabiki wake zilizotokea usiku wa kuamkia leo wakati wakiwa njiani kwenda Dar es Salaam kutazama mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly. Ajali ya kwanza ni ya mashabiki wa Tawi la Kiwira Rungwe la mkoani Mbeya ambayo imetokea eneo la Vigwaza mkoani Pwani, ambapo mtu mmoja amefariki dunia. Ajali nyingine ni ya mashabiki wa Tawi la Wekundu wa Border kutoka Tunduma mkoani Songwe iliyotokea Doma mkoani Morogoro ambapo mtu mmoja ameumia. Simba imesema viongozi wake wanaelekea eneo la Vigwaza kwa ajili ya kutoa msaada kwa waathirika na kwamba inatoa pole kwa wote walioathirika na ajali hizo.

TUCHUKUE TAHADHARI KUELEKEA KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU YA PASAKA

Image
Wananchi wa Mkoa wa Songwe wametakiwa kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Pasaka. Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Agustino Senga wakati akizungumza kupitia kipindi maalum cha redio Tunduma Fm 92.1 MHz"iliyopo mjini Tunduma Machi 28, 2024. Kamanda Senga aliwataka wananchi kuchukua tahadhari mbalimbali hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kipindi cha sikukuu ya Pasaka kutokana na mvua zinazonyesha akiwataka kuepuka kukaa mabondeni na kuwakataza watoto kucheza na kuogelea kwenye madibwi na mito hasa ukizingatia kwa sasa watoto wengi wapo mikononi mwa wazazi kutokana na kufungwa kwa Shule. Aidha, Kamanda Senga aliwasihi wananchi kuepukana na unywaji wa pombe uliopindukia  ambao unaweza kupelekea wafanye vitendo vya kihalifu na ukatili katika jamii na kufanya hivyo Jeshi la Polisi litachukua hatua kali kwa watu hao. Pia Kamanda Senga aliwataka madereva kufuata sheria za usalama barabarani

SIKUKUU INAPITA, UHAI AUNUNULIWI

Image
Madereva na wamiliki wa vyombo vya moto mkoani Songwe wametakiwa kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani ili kujiepusha na ajali zinazoweza kuepukika kuelekea kipindi cha sikukuu ya Pasaka. Rai hiyo imetolewa na Polisi Kata ya Ipunga Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Eletisia Mtweve Machi 26, 2024 wakati alipokua anatoa elimu juu ya thamani ya uhai wa mwanadamu kwa waendesha pikipiki za magurudumu mawili maarufu Bodaboda katika Kijiwe cha Shingo Fene kilichopo Kijiji cha Ipunga wilayani Mbozi. “Kumbukeni uhai aununuliwi sehemu yoyote hapa duniani hivyo ni wajibu wenu kufuata sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya, pombe na kujiepusha kubeba abiria usiyemfahamu nyakati za usiku ukiwa peke yako ili kulinda usalama wako kwanza" alisema Mkaguzi Mtweve. Aidha, alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi/walezi na jamii kiujumla kuendelea kuwa karibu na watoto wao katika nyakati hizi za mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo ili kuwaepus

POLISI WAPYA 68 WAWASILI MKOANI SONGWE

Image
Askari wapya kutoka shule ya Polisi Moshi wamepokelewa Mkoani Songwe tarehe 27, Machi 2024 baada ya kuhitimu mafunzo yao ya awali Machi 25 mwaka huu wakiwa wako tayari kwa ulinzi wa raia na mali zao Mkoani humo. Askari hao wamepokelewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Agustino Senga na kuwataka kufanya kazi kwa uweledi ili kuendelea kulinda taswira nzuri ya Jeshi la Polisi kwa jamii. "Tutakuwa nanyi kwa miezi miwili kwa lengo la kuendelea na mafunzo ya nadharia na vitendo ili kuwaongezea maarifa katika utendaji wa kazi zetu za kila siku ikiwa ni pamoja na kuyatambua maeneo yenu ya kazi mkiwa mnayafanya kwa vitendo yale yote mliyofundishwa ili kuendelea kuzuia uhalifu na wahalifu Mkoani hapa" alisema kamanda Senga.  “Askari mnatakiwa kutojihusisha na vitendo ambavyo vinaleta taswira mbaya kwa Jeshi la Polisi, mnapaswa kufanya kazi kwa kufuata wimbo wa maadili ya Afisa wa Jeshi la Polisi na kuzingatia kauli mbiu yetu ambayo nidhamu

DAWATI LA JINSIA MOMBA WATETA NA WANAFUNZI TUNDUMA

Image
Mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Momba Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Bahati Simchile amewataka wanafunzi wa Shule ya Sekondari Danida iliyopo Mjini Tunduma Mkoani Songwe kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto kwa Jeshi la Polisi pindi wafanyiwapo au waonapo ili aweze kuzichukulia hatua za haraka. Alisema hayo Machi 26, 2024 alipotembelea Shule hiyo kwaajili ya kutoa Elimu ya masuala ya Ukatili wa kijinsia ambapo amewafundisha nini maana ya ukatili, sababu, aina, madhara ya ukatili na jinsi ya kuepuka kufanyiwa vitendo hivyo pindi wawapo shuleni, njiani, nyumbani na mtaani. Kwa upande wa wanafunzi hao wameahidi awatokaa kimya watatoa taarifa za ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto kwa Jeshi la Polisi ili kupunguza vitendo hivyo katika jamii. Kutoka Dawati la Habari Polisi Songwe.

ASKARI KATA ILEJE ATOA SOMO LA UMUHIMU WA KINAWAKA MIKONO SHULE YA MSINGI KALEMBO

Image
 Picha mbalimbali za matukio zikimuonesha Polisi Kata wa Kata ya Kalembo Mkaguzi Msaidizi Raphael Magoma wakifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya Msingi Kalembo iliyopo Wilayani Ileje baada ya kuwapa elimu ya umuhimu wa kunawa mikono kabla na baada ya kula. Mkaguzi Magoma aliwataka wanafunzi hao kutumia muda mwingi kujifunza ili kuongeza maarifa ambayo ni sehemu kubwa ya mafanikio katika maisha yao. Vilevile aliwaomba walimu kuendelea kuwajengea uwezo wa kujieleza mbele ya watu ili waweze kuwa na uwezo wa kujiamini katika kujibu maswali. Elimu hiyo ilitolewa leo tarehe 22, Machi 2024.

HII HAPA MIRADI MIKUBWA TISA YA KIMKAKATI MKOANI SONGWE INAYOTEKELEZWA NA TANROADS

Image
  Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imekusudia kutekeleza miradi mikubwa 9 ya kimkakati 9 ikiwemo upanuzi wa barabara kuu ya TANZAM kipande cha Igawa – Tunduma (km 218) na Ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja wa magari katika barabara hiyo eneo la Iboya Mkoani Songwe. Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe Mha. Suleiman Bishanga amesema hayo tarehe 19 Machi 2024; alipozungumza na Kipindi cha TANROADS Mkoa kwa Mkoa kuhusu mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika sekta ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja. Amemtaja mkandarasi anayejenga barabara hiyo ya njia nne kwa utaratibu wa EPC + F ni M/s China Civil and Engineering Construction Coopration (CCECC) kutoka China; ambaye tayari ameshaanza maandalizi ya kuainisha maeneo ya kujenga kambi. Amesema pia mradi huo utakuwa na barabara za mchepuo (Bypass) ili kuondoa msongamano wa magari hasa malori katikati ya mji. Amesema miradi mingine ambayo ipo kwenye mipango y

RC DODOMA ATOA WITO KWA SHULE KUJENGA ENEO LA SHULE

Image
  MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ametoa wito kwa shule zote zilizopo Mkoani Dodoma kuhakikisha zinatafuta maeneo kwaajili ya michezo kwa wanafunzi kwasababu michezo inajenga  afya ya akili na mwili. Wito huo aliutoa katika hafla ya uzinduzi wa wiki ya wadau wa elimu kwa Mkoa wa Dodoma pamoja na ugawaji wa mipira 1000 kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kwa Halmashauri zote zilizopo Dodoma lengo likiwa kuwasaidia wanafunzi kuendelea kujifunza michezo kwa ufanisi. “Nimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono sekta ya michezo kwa kuhakikisha Tanzania inajiandaa kushindana katika mashindano makubwa duniani, pia kwa kuwaandaa vijana kwaajili ya kuitumikia timu ya Taifa na kufanya vizuri katika sekta ya michezo duniani. Nitoe shukrani kwa uongozi wa TFF kwa kutuwezesha mipira ambayo itatumika katika kuinua vipaji kwa wanafunzi katika mkoa wa Dodoma” alisema Senyamule. Alisema shule zote zitakazopata mipira zitafuatiliwa na kuhakik

DEREVA WA GARI LA SERIKALI MIKONO MWA POLISI KWA KUMJERUHI MWANAE

Image
  JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Dereva wa serikali, James Mrema kwa tuhuma za kumfanyia ukatili kwa kumpiga na kumsababishia maumivu makali mtoto wake mwenye umri wa miaka tisa. Akizungumza na Nipashe Digital kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Theopista Mallya, amesema "Jeshi la polisi linamshikilia dereva wa gari la serikali aliyefahamika kwa jina James Mrema(39) kwa kumpiga mtoto wake na kumsababishia maumivu makali hadi kulazwa katika hospitali ya rufani ya Mkoa wa Dodoma." Amesema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo na utakapo kamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.Awali, Dk.Baraka Monday wa Hospitali ya Rufani ya mkoa wa Dodoma, amekiri kupokelewa kwa mtoto huyo hospitalini hapo na mwili wake umekutwa na majeraha ya kupigwa huku mguu na mkono ukiwa umevimba.

RAIS AJIUZULU AANDIKA BARUA

Image
  Rais wa Vietnam, Vo Van Thuong ametangaza kujiuzulu jana Machi 20, 2024 ikiwa ni baada ya kukaa mwaka mmoja madarakani. Bunge la nchi hiyo limeidhinisha kujiuzulu kwake. Sababu ya kuchukua hatua hiyo imetajwa kuwa ni ukiukaji wa kanuni za chama, kulingana na ripoti za ndani nchini humo, pamoja na mapungufu aliyonayo rais huyo wakati ambao nchi hiyo ipo kwenye kampeni ya kupinga ufisadi. Uamuzi wa Bunge umekuja baada ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti jana Jumatano kukubali uamuzi wa Rais huyo, aliyehudumu kuanzia Machi 2, 2023. Imeelezwa ukiukwaji na dosari zake zimeathiri vibaya mtazamo wa umma pamoja na sifa ya chama na serikali, japokuwa haijafafanuliwa zaidi juu ya dosari hizo. Thuong anakuwa Rais wa pili kujiuzulu katika kipindi cha miaka miwili huku kukiwa na operesheni kali dhidi ya ufisadi ambao umesababisha baadhi ya wanasiasa kufukuzwa kazi, na viongozi wakuu wa biashara kushitakiwa kwa udanganyifu na ufisadi. Thuong, mwenye umri wa miaka 54, alikuwa Rais mwenye umri md

WANAFUNZI WAIBA VITI VYA SHULE NA KUUZA

Image
  Wanafunzi watano wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Chuno, Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mkoani Mtwara wamefukuzwa Shule kutokana na kuwa na tabia ya wizi wa kuiba viti vya Shule na kwenda kuviuza kama chuma chakavu. Mkuu wa Shule hiyo, Hamisi Kaoneka, amesema tukio hilo la wizi limetokea March 7, 2024 usiku ambapo Wanafunzi hao walibainika wakibeba viti hivyo na kwenda kuviuza “Tukaenda mpaka kwenye eneo ambalo wanauza chuma chakavu ni maeneo ya Chuno uwanjani pale, kufika pale bahati nzuri ule muda nafika pale ndio walikuwa wanapakia kwenye lori, Wanafunzi hao sio mara ya kwanza kukabiliwa na kesi ya wizi, walishawahi kushitakiwa Shuleni kwa kuiba mabati mtaani na kwenda kuyauza kama chuma chakavu” Mkuu huyo wa Shule amesema hayo wakati wa kikao cha Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Mwalimu Hassan Nyange na Viongozi wa elimu ngazi za Shule za Msingi na Sekondari , Watendaji wa Mitaa na Kata, Maofisa elimu na baadhi ya Wakuu wa Idara wa Manispaa hiyo kujadili mu

BILIONI 431.474 KUIFUNGUA KAGERA KIMIUNDOMBINU

Image
  Katika kipindi cha miaka mitatu, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe Rais Dkt. Samia Hassan  imetoa zaidi ya shilingi bilioni 431.474 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya ujenzi wa Miundombinu ya barabara na madaraja Mkoani Kagera. Meneja wa Wakala wa Barabara  Tanroads  Mkoa wa Kagera, Mha. Ntuli Mwaikokesya amesema hayo leo tarehe 20 Machi 2024 alipozungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika sekta ya ujenzi. Amesema fedha hizo zimeweza kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati iliyokamilika na inayoendelea kujengwa ambayo ni pamoja na Ujenzi wa barabara ya Nyakanazi –Kidahwe; kipande cha Nyakanazi- Kabingo (Km 50), barabara ya Bugene-Kasulo- Kumunazi (Km 128.5), kipande cha Bugene - Burigi chato (Km 60), Ujenzi wa daraja la kitengule (140m) na barabara unganishi (km 18) na Ukarabati wa barabara ya Lusahunga–Rusumo (km 92) kwa kiwango cha lami. Miradi mingine ni Ujenzi wa barabara ya kutoka Kagera sugar Juntion(Bunazi) –Kagera

JELA MIKA 30 KWA KUBAKA KIKONGWE CHA MIAKA 80.

Image
Mahakama ya Wilaya Morogoro imemuhukumu Sadick Elias (24) Mkazi Pulambili Kata ya Kidugaro Tarafa ya Ngerengere Wilaya Morogoro vijijini kwenda Jela miaka 30 kwa kosa la kumbaka kikongwe wa miaka 80. Akisoma hukumu hiyo Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Morogoro Mh. Robert Kasele alisema kuwa tukio hilo lilitokea Julai 29, 2023 huko Pulambili Kata ya Kidugalo Wilaya ya Morogoro Vijijini ambapo mshitakiwa alifungua komeo na kuingia ndani ya nyumba ya Kikongwe huyo kisha kutenda kosa hilo. Julai 30, 2023 Mtuhumiwa alikamatwa na Jeshi la Polisi na ushahidi ulipo kamilika mtuhumiwa alifikishwa Mahakamani na kutiwa hatiani kwa kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 kwenda jela kwa kutenda kosa la kubaka.

RPC MALLYA AKABIDHIWA OFISI DODOMA

Image
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya Machi 20, 2024 amekabidhiwa rasmi Ofisi kama Kamanda wa mkoa huo baada ya kuhamishwa kutoka mkoa wa Songwe. Wakati wa makabidhiano hayo, Kamanda Mallya alimshukuru aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa huo SACP Martine Otieno baada ya kumkabidhi Ofisi hiyo na kuhaidi kuendelea kudumisha amani ya mkoa wa Dodoma. Pia, Kamanda Mallya aliwataka Polisi Kata kuendelea kutoa elimu ya Polisi jamii kwa kukemea uhalifu kwa kuanza na ulinzi shirikishi na kuhakikisha kila kata inakomesha uhalifu kikamilifu. Lakini pia amewataka Wakuu wa Polisi Wilaya (OCD's) kusimamia kata zao ili kuweza kuondoa uhalifu na kuifanya Dodoma kuwa salama.

AMBAKISYE NA WENZIE MBARONI KWA KUGUSHI HATI

Image
  Machi 18, 2024, shauri la Rushwa na Uhujumu Uchumi Na. 7060/2024, lilifunguliwa mbele ya Mhe. Atupye Benson Fungo ambaye ni Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbogwe dhidi ya:- 1. Ambakisye Amani Mfwango ambaye ni Mwalimu Mkuu; 2. Beatrice David Musiba ambaye ni Mwalimu wa Kawaida wote wa Shule ya Msingi Bukandwe. Walimu hao walifikishwa Mahakamani na Ofisi ya TAKUKURU (W) ya Mbogwe, ikiongozwa na Wakili wa Jamhuri Chali Kadeghe. Washitakiwa wamefikishwa Mahakamani kwa mashtaka ya Ubadhirifu wa Mali za Umma; Kugushi nyaraka za vikao vya Kamati ya Shule ya Msingi Kanegere sambamba na kugushi hati ya malipo yenye thamani ya shilingi 1,500,000/= kwa manufaa yao binafsi, jambo ambalo ni kinyume na vifungu vya 333, 335(d)&(i) na 337 vyote vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyorejewa Mwaka 2022. Makosa haya pia ni kinyume na Vifungu vya 28(1) na 31 vyote vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2011, ikisomwa pamoja na Aya ya 21 ya Jedwali la kwanza, vifungu vya

TRENI ZA MIZIGO KUANZA SAFARI TANZANIA NA ZAMBIA

Image
  Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara) limesaini mkataba na sekta binafsi ya kuleta treni ambazo zitabeba mizigo kutoka bandarini na kupeleka nchi Jirani. Mkataba huo umesainiwa leo Machi 20, 2024 Makao Makuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Tazara, Bruno Ching’andu na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Usafirishaji Makontena ya Bravo Group Limited, Angelina Ngalula ambaye pia ni Mwenyekiti wa wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF). Akizungumza Ching’andu amesema makubaliano hayo yanalenga kupanua ukuaji wa uchumi na fursa za biashara ndani ya ukanda wa Dar es Salaam sambamba na kuimarisha biashara ya ndani ya Kanda ya SADC. “Ushirikiano huu unaonyesha nguvu ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) katika kutoa huduma,” amesema Nae, Mwenyekiti wa Bravo, Angelina Ngalula ametoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya biashara ambayo yanahimiza uwekezaji na ukuaji wa biashara, na kusababisha fursa za aj