TUNDUMA:STOO YA KUHIFADHI VIFAA VYA UJENZI YAJENGWA KWA SHILINGI MILIONI 25
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mkoani Songwe limetoa siku 5 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Philemon Magesa kuhakikisha kuwa anawasilisha kwenye kamati ya fedha, taarifa ya matumizi ya shilingi milioni 383 za mradi wa ujenzi wa uzio wa soko la wamachinga Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Madiwani katika baraza hilo kutoridhishwa na taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa soko hilo, ikiwemo kibanda cha kuhifadhi vifaa vya ujenzi (Stoo) katika mradi huo kudaiwa kuwa ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi milioni 25. Mbali na kuhoji gharama za ujenzi wa stoo, Madiwani hao wamelalamikia kitendo cha Mkurugenzi huyo kukaidi agizo la kamati ya fedha ya kupeleka vifaa vyote vya ujenzi kupelekwa eneo la mradi ikiwemo mifuko 1870 ya saruji, pamoja na kubadilishwa kwa ramani ya soko hilo. Uamuzi huo ulifikiwa jana kwenye kikao cha baraza kilichoketi kwa ajili ya kupitia na kujadili taarifa za robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022/23 na kufanyika katika Ukumbi wa ofi...