Posts

Showing posts from February, 2023

TUNDUMA WAPEWA SIKU 14 KUKAMILISHA SOKO LA MAJENGO

Image
Baada ya wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga kuitaka serikali kuharakisha ujenzi wa soko la Majengo halmashauri ya mji wa Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe katibu Tawala mkoani humo Happiness Seneda ameuagiza uongozi wa halmashauri hiyo kutumia wiki mbili kumaliza ujenzi huo. Seneda ametoa maagizo hayo baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kujionea mwenendo wa ujenzi wa soko hilo huku akisema imekuwa ni mara ya tatu kufika hapo na kukuta ujenzi hauendelei. Seneda amesema soko hilo likamilike mapema ili kuwa rahisishia wafanyabiashara kufanya kazi zao kwenye mazingira rafiki na salama kwa walaji. “Nimekuja hapa mara mbili na hili staki lijirudie tena ndani ya wiki mbili majengo yakamilike ,hivyo nakuja baada ya hizo wiki mbili kama mtakuwa hamjakamilika sitakuwa na msamalia mtume”, amesema Seneda. Mkuu wa wilaya hiyo Faki  Lulandala amesema kuanzia sasa atakuwa anashinda eneo la ujenzi kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama kuhakikisha ujenzi wa soko hilo lin

WANANCHI ILEJE WAMKATAA MWENYEKITI WA KIJIJI

Image
Wananchi wa kijiji cha Shinji kata ya Mbebe wilayani Ileje mkoani Songwe wamesema hawana Imani na mwenyekiti wa kijiji hicho Ali  Kalinga akishutumiwa kuwamilikisha baadhi ya wananchi wakiwepo ndugu zake eneo lililotengwa na wananchi kwa ajili ya matumizi ya malisho Zaidi ya hekari 50. Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara na Kaimu afisa Tarafa ya Bulambya Frank Mwampamba ambaye alimwakilisha mkuu was wilaya hiyo Farida Mgomi walisema mwenyekiti huyo alihusika kugawa maeneo hayo bila kushirikisha wajumbe wa halmashauri ya kijiji na wananchi waliopitisha kutenga eneo hilo tangu miaka ya nyuma. Lingisoni Sikanyika mkazi wa kijiji hicho alisema mwenyekiti huyo alitumia madaraka yake kuwagawia kwa nguvu baadi ya ndugu zake na kushindwa kuwaondoa wananchi wengine waliovamia eneo Hilo  Zaidi ya hekari 20. Sikanyika alisema mwenyekiti wetu atupishe kwenye kiti tumeshindwa kuendelea kufanya naye kazi kwani yeye yupo mbele kuharibu matumizi bora ya mpango aridhi ya kijiji ambayo wananchi walik

MKUU WA POLISI(OCD),OFISA UPELELEZI (OC CID)WASIMAMISHWA KAZI KWA UNYANYASAJI

Image
  Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni amewasimamisha kazi Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) na Ofisa Upelelezi Wilaya ya Kilombero baada ya kulalamikiwa na wananchi kuwa wanawanyanyasa. Kilombero. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni amewasimamisha kazi Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD), SSP Shedrack Kigomanya na Ofisa Upelelezi Wilaya ya Kilombero, SP Daud Mshana baada ya kulalamikiwa na wananchi kuwa wanawanyanyasa.  Masauni amechukua hatua hiyo jana Jumatatu, Februari 20, 2023 akiwa kwenye ziara wilayani Kilosa ambapo pamoja na kukagua baadhi vituo vya polisi na magereza yaliyopo pia alizungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara. Waziri Masauni pia amemwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillus Wambura kuwachunguza na kuwahamisha viongozi hao ili kujenga imani kwa wananchi na pia kuimarisha dhana ya uwajibikaji. Vile vile amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama kuwahamisha askari wote wanaotajwa kunyanyasa wananchi na kuleta askari wapya na k

OFISI SERIKALI ZA MITAA ZAONGOZA KUTOLEWA MALALAMIKO MKOANI SONGWE

Image
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushw (TAKUKURU) Mkoa wa Songwe imefanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo 68 yenye thamani ya shilingi bilioni 11.564 katika Halmashauri zote za Mkoa wa Songwe na kubaini kasoro kadha, ikiwemo fedha za mikopo ya asilimia 10 kwa ajili ya Wanawake, Vijana na Walemavu. Taarifa hiyo ilitolewa jana na Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Songwe, Mohamed Shariff, kwa waandishi wa Habari, wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa ofisi hiyo katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Oktoba hadi Disemba 2022. Alisema katika miradi yote iliyofuatitiliwa  baadhi ya miradi ilibainika  kuwa na upungufu ambapo taasisi hiyo ilichukua hatua mbalimbali kwa wahusika kwa lengo la kuzia vitendo vya rushwa na ubadhirifu. Miongoni mwa miradi iliyobainika kuwa na upungufu ni ile ya sekta ya Afya kwenye ujenzi wa zahanati na vituo vya afya,ujenzi wa vyumba vya madarasa katika sekta ya Elimu, pamoja na Miundombinu ya barabara. Eneo lingine ambalo TAKUKURU ilifanya ufuatiliaji kwa le

MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE ADAIWA KUJINYONGA

Image
  Mwanafunzi wa darasa la nne Shule ya Msingi Kambarage Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Mkoa wa Pwani, Tatu Machemba amepoteza maisha ikielezwa kuwa amejinyonga kwa kutumia kamba chumbani nyumbani kwao Mtaa wa Mkoani mjini Kibaha, Pwani.  Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi leo Jumatatu Februari 20, 2023, Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkoani,  Shabani Rashidi amesema kuwa taarifa za tukio hilo zilimfikia juzi kwa njia ya simu na kabla ya kwenda aliwasiliana na Jeshi la Polisi. "Nilipigiwa simu nikijukishwa tukio hilo juzi na kabla ya kwenda niliwasiliana na Jeshi la Polisi tukaenda eneo la tukio nyumbani kwa familia hiyo," amesema Amesema kuwa baada ya kufika eneo la tukio waliingia na kukuta mwili wa mwanafunzi huyo kichwa chake kimechomekwa kwenye kamba na yeye amepiga magoti," amesema. Mwenyekiti huyo amesema kinacholeta maswali kwa baadhi ya wananchi ni mazingira yaliyokutwa kwani mwili wa marehemu haukuwa unaning'inia bali alikutwa amepiga magoti. "Sasa hali hiyo

POLISI SITA WAFUKUZWA KAZI

Image
 Jeshi la Polisi mkoani Arusha limewafukuza kazi askari wake sita katika kipindi cha miezi sita, kutokana na makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu yasiyoendana na maadili ya jeshi hilo. Arusha. Jeshi la Polisi mkoani Arusha limewafukuza kazi askari wake sita katika kipindi cha miezi sita, kutokana na makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu yasiyoendana na maadili ya jeshi hilo. Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake leo Febuari 20, 2023 bila kuwataja majina ya askari hao, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Justine Masejo amesema kuwa askari hao walifukuzwa kazi katika kipindi hicho baada ya uchunguzi wa kijeshi kukamilika kutokana na makosa yaliyokuwa yakiwakabili. Amesema kuwa utaratibu wa kuchukuliana hatua za kinidhamu ndani ya Jeshi la Polisi ni jambo la kawaida hasa kwa askari wanapokiuka maadili ya jeshi hilo "Katika kipindi cha miezi sita tumewafukuza askari wetu sita, wakikabiliwa na makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu, kama mnavyojua askari wetu wanaoajiriwa wanatoka kwe

WEZI WAVAMIA NYUMBANI KWA KAMANDA WA POLISI WAIBA BUNDUKI

Image
  Wezi katika kaunti ya Busia walivaamia nyumbani kwa kamanda huyo usiku wa manane na kuiba bunduki aina ya Czeska, polisi wameanza upelelezi wa tukio hilo. Kenya. Polisi katika kaunti ya Busia wameanza msako kutafuta bastola aina ya Czeska iliyoibwa kwenye nyumba ya kamanda wa polisi wa kaunti hiyo usiku wa Jumamosi, Februari 18 ambapo wezi mbali na bastola waliiba redio na mtungi wa gesi. Inasadikika wezi hao walinyunyiza dawa ya kulewesha kupitia dirisha la chumba alichokuwa amelala kamanda huyo kabla ya kutekeleza tukio lao kkitu ambacho kilimsababishia maumivu ya kichwa na kupata kiznguzungu alipoamka. Kamanda wa polisi wa kaunti hiyo ya Busia, Bishar Muhumed SSP amethibitisha kutokea kwa tukio hilo usiku wa jana na wezi hao walipora vitu ikiwemo bastola anayomiliki kamanda huyo. Maofisa wa usalama wametembelea eneo la tukio na kikosi cha wapelelezi wakiwa na mbwa wa kundi la K9 kwa ajili ya kuchukua harufu ambapo aliwapeleka barabara inayokwenda Uganda lakini huyo alipoteza dira

MAJAMBAZI YATEKA GARI LA MAITI SONGWE YAPORA SIMU NA FEDHA

Image
  Jeshi la Polisi Mkoani Songwe limethibitisha Majambazi kuteka gari la Serikali lililokuwa limebeba maiti ya mwanafunzi katika Msitu maarufu wa Nyimbili uliopo kata ya Ntungwa tarafa ya Kamsamba Wilayani Momba. Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake kamanda wa polisi Mkoa wa Songwe (ACP)Theopista Mallya amesema siku ya Februari 16,2023 katika misitu wa Nyimbili uliopo barabara ya Mlowo Kamsamba unaounganisha Wilaya za Momba na Mbozi mida ya saa saba na nusu usiku gari la Serikali  SM 14056 likiwa limebeba maiti ya mwanafunzi wa shule ya Msingi Itumbula kwenda Kijiji cha Msanyila Mbozi aliezama katika bwawa wakati anaogelea na kwenye hili gari alikuwemo Afisa Elimu wa kata ya Ivuna ambae jina lake halikutajwa na wenzie watano wakisafirisha mwili wa marehemu lakini walipofika eneo la Msitu wa Nyimbili walikuwa Magogo yamewekwa mbele yao na hapo ndio walipotekwa na Majambazi na kuporwa fedha 216,000 pamoja na simu zao vyote thamani yake ni 1,200,000 zote kwa pamoja. Kamanda Mallya a

MBUNGE MWENISONGOLE,WATUMISHI TANROADS NA WADAU WENGINE WAMWAGA VIFAA KWA WANAFUNZI WALIOANZA SHULE BILA VIFAA

Image
  Wadau mbalimbali mkoani Songwe wameombwa kujitokeza kusaidia michango na vifaa ili kuwawezesha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ambao hawana vifaa na sare katika mkoa huo. Rai hiyo imetolewa leo Jumamosi Februari 18, 2023 na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe (RAS), Happiness Seneda wakati wa mazoezi ya kujenga afya maarufu 'Back to School Songwe Jogging Club' yenye lengo la kuhamasisha wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni kujiunga na masomo. Katika mazoezi hayo ambayo yameongozwa Katibu Tawala huyo wa mkoa  yaliambatana na kukabidhi vifaa baadhi ya wanafunzi ambavyo vimetolewa na wadau mbalimbali. Katibu Tawala huyo amesema kuwa vifaa hivyo vimechangiwa na wadau wakiwemo Tanroads ambao wamechangia vifaa vyenye thamani ya Sh300,000, Mbunge wa Jimbo la Mbozi, George Mwenisongole akichangia vifaa vyenye thamani ya Sh50,000 huku Shirika la Tanzania Communication and Development Centre (TCDC) likichangia madaftari kwa wanafunzi 17 huku akitoa rai kwa wadau wengine kuchangia.

DC MBOZI AKABIDHI PIKIPIKI KWA WATENDAJI KATA 9 ZA MBOZI,DED NANDONDE ATAKA WAZITUNZE

Image
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi (DC), Esther Mahawe amekabidhi pikipiki tisa kwa watendaji wa kata ambazo zitawasaidia katika kutekeleza majukumu yao. Mkuu wa wilaya huyo  amekabidhi pikipiki hizo leo Ijumaa Februari 17, 2023 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi. Akikabidhi pikipiki hizo, mkuu wa wilaya huyo amesema kuwa usafiri huo utawarahisishia watendaji hao wa kata hizo za pembezoni kutimiza majukumu yao kwa wakati. DC Mahawe ametumia nafasi hiyo kuwaagiza watendaji hao kwenda kuwafuatilia watoto ambao bado hawajaripoti shuleni ili waweze kujiunga na wenzao kuendelea na masomo "Naomba sana tuungane kwa pamoja tumsaidie mama Samia (Rais Samia Suluhu Hassan) juhudi kubwa anazofanya katika kuwasaidia wananchi wake" ameagiza DC huyo. Amekumbusha watendaji hao kuwa makini katika matumizi ya vyombo hivyo vya moto Ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi (DED) Abdallah Nandonde amezitaja kata zilizopata pikipiki hizo kuwa ni

RC KINDAMBA " WAKANDARASI WABABAISHAJI KUCHUKULIWA HATUA

Image
    Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Waziri Kindamba ameshuhudia utiaji saini mikataba 10 ya miradi ya maji mkoani humo, akiwaonya makandarasi watakaokiuka mikataba hiyo kuwa watachukuliwa hatua kali. Songwe. Jumla ya mikataba 10 ya miradi ya maji yenye thamani ya zaidi ya Sh14.27 bilioni imesainiwa na kuleta tumaini jipya kwa wananchi la kuondokana na uhaba wa maji. Hafla ya utilianaji mikataba hiyo imefanyika leo Ijumaa February 17, 2023 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Songwe na kushuhudiwa na Mkuu wa mkoa huo, Waziri Kindamba aliyewaonya makandarasi wababaishaji. Kindamba amesema Serikali imetoa fedha nyingi kwenye miradi inayogusa maisha ya kila siku ya watu ili kuona wanaondoka pale walipokuwepo katika shida ya kusaka maji na kuacha kazi ya uzalishaji ili shida hiyo imalizike na watu waendelee kufanya kazi ya Kujenga nchi. "Leo mnaposaini mikataba mnatuonesha sura za upole, lakini mkienda kufanyakazi mnabadilika na kuanza kumsumbua, sasa nawaambia kama kuna mkandarasi aliyefika

WAKUU WA IDARA SIMAMIENI MIRADI-MAJALIWA

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Idara katika halmashauri zote nchini wasimamie kikamilifu miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali kwenye maeneo yao na wahakikishe inakamilika kwa wakati ili itae huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa. “Huduma za jamii ndizo zinazogusa maisha ya kila siku ya wananachi kama elimu, maji, nishati, afya na kilimo, hivyo halmashauri zetu lazima ziongeze nguvu katika maeneo hayo. Wakuu wa Idara tumieni muda mwingi kwenda kwenye maeneo ambayo miradi inatekelezwa badala ya kukaa ofisini tu.” Ameyasema hayo leo (Jumatano, Februari 15, 2023) wakati akizungumza na watumishi wa mkoa wa Songwe akiwa kwenye majumuisho ya ziara ya kikazi mkoani Songwe ya kukagua miradi ya maendeleo na mafanikio ambayo Serikali ya awamu ya sita imeyapata katika kipindi cha miaka miwili. Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Mji Tunduma kwa kujenga baadhi ya miradi kwa kutumia makusanyo ya ndani ukiwemo ujenzi wa madarasa 10 kat

AMCOS MBOZI KUCHUNGUZWA-MAJALIWA

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itafanya uchunguzi kwa vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) wilayani mbozi mkoani Songwe na watakaobainika kuhusika na ubadhirifu wowote watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Mheshimiwa Majaliwa ametoa kauli hiyo baada ya Mbunge wa jimbo la Mbozi, George Mwanisongole kuzilalamikia AMCOS za wilaya hiyo kuwanyonya wakulima wa kahawa na hivyo kuwafanya wauchukie ushirika. Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Februari 14, 2023) wakati akizungumza na wananchi katika eneo la Mlowo wilayani Mbozi akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Songwe ya kukagua miradi ya maendeleo na mafanikio ambayo Serikali ya awamu ya sita imeyapata katika kipindi cha miaka miwili. “Ushirika ni muhimu kwa maendeleo ya wakulima lakini wanahitajika wanaushirika waaminifu, hivyo tutakuja kufanya uchunguzi wa mwenendo wa AMCOS za Mbozi ili kubaini wabadhirifu na kuwachukulia hatua. Pia tutachunguza makato wanayokatwa.” Kwa upande wake, Mbunge wa Mbozi, Mwanisongole

RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI

Image
 

UKUSANYAJI WA MAPATO TUNDUMA WAMKOSHA MAJALIWA AMTAKA DED KUCHAPA KAZI

Image
  Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji   Tunduma  Philimon Magesa kwa ukusanyaji wake Mkubwa wa Mapato ambapo kabla ya mwaka wa fedha kukamilika amekusanya Bilioni 8 huku kukiwa na mategemeo ya kukusanya zaidi. Pia waziri mkuu amemuagiza Mkurugenzi huyo aendelee kubana mianya ya upotevu wa fedha kwani serikali ya Rais Dkt Samia imemuamini aendelee kupiga kazi. Majaliwa alisema anafahamu changamoto anazopitia  Mkurugenzi huyo Halmashauri ya Tunduma hivyo atambue kuwa amewekwa hapo na serikali na achape kazi  eendelee na makusanyo kwani mapato  ndani yanajenga miradi mikubwa ikiwemo shule za Ghorofa huku akiagiza kuleta fedha zaidi ili Tunduma ipae kiuchumi kuendana na msemo wa lango kuu la Sadc. Kwa Upande wa wake Mbunge wa Jimbo la Tunduma David Silinde amemueleza Waziri Mkuu kuwa  Mkurugenzi huyo ni jembe na anawasaidia sana Wilaya Tunduma na  amemshukuru Rais Samia kwa Kuwaletea Mkurugenzi mzuri na ana imani  Tunduma itaendelea kupaa katika Mapato.

WAZIRI MKUU AKOSHWA NA MWEKEZAJI KIJANA KIWANDA CHA KAHAWA SONGWE

Image
WAZIRI Mkuu Kassim Majiliwa amekoshwa na uwekezaji mkubwa wa kiwanda kikubwa Cha kahawa Cha GDM kinachoendeshwa na kijana mzawa Richard Mwangoka mwenye umri wa miaka 22 kinachochakata kahawa iliyonunuliwa kwa wakulima wazawa. Akiwa katika Ziara ya Siku tatu katika mkoa wa Songwe , akitembelea kiwanda na kuongea na wafanyajazi wa kiwanda Cha GDM alisema Serikali ya awamu ya sita chini ya Dokta Samia Suluhu Hassani inafurahishwa na uwekezaji mkubwa unaofanywa na kijana mzawa ambaye anatengeneza ajira , biashara  na uchumi. Alisema zao la kahawa ni miongoni mwa mazao makuu ya kimkakati ndani ya Nchi yetu  ambalo Serikali inatoa kipaumbele kutokana na kukuza uchumi wa Wananchi na Taifa . "Rais wetu Dokta Samia Suluhu Hassan anahamasisha sana wawekezaji wa ndani, Leo hii nimefarajika sana kwa kupata mwekezaji kijana mzawa ambaye anatengeneza ajira, kukuza soko kwa kuliongezea thamani kwa kulichakata zao la kahawa na kukuza uchumi wa Wananchi na Taifa Pamoja na baba yake aliyeanzisha ki

BILIONI 4 ZAPELEKWA MBOZI KUJENGA BARABARA KUPITIA TARURA: SILINDE

Image
Naibu Waziri Ofisi ya Rais -TAMISEMI, Mhe. David Silinde (Mb) amesema Bajeti ya  wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) katika Halmashauri ya wilaya ya Mbozi imeongezeka mara nne hadi kufikia shilingi bilioni 4 katika mwaka wa fedha 2022/23. Amesema hayo leo tarehe 14 Februri 2023 wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Mlowo katikaHalmashauri ya wilaya Mbozi mkoani Songwe. “Wakati Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani alikuta bajeti ya TARURA katika Halmashauri ya Mbozi ilikuwa bilioni 1.7 lakini kwa sasa bajeti imepanga kufikia bilini 4 katika mwaka wa fedha 2022/23” amesema Mhe. Silinde Amesema kupitia mradi wa kujenga barabara katika maeneo ya uzalishaji wa mazao ya kilimo “Agri-connect”, barabara ya Ilolo - Ndolezi yenye kilometa 11 inajengwa kwa Kiwango cha lamikatika katika wilaya ya Mbozi ambayo inaanza kutekelezwa hivi karibuni. Aidha, Mhe. Silinde amesema katika awamu ya pili ya Mradi wa Agri-connect

KANISA LA ANGLIKANA KUTOWAZIKA WASIOHUDHULIA JUMUIYA,IBADA KANISANI

Image
   Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam limeweka msimamo kuhusu utoaji huduma za kiroho kwa waumini wake, ambapo kuanzia sasa watakaohudumiwa ni wale wanaoshiriki ibada za jumuiya na kanisani. Hayo yamebainishwa leo Jumamosi Februari 11, 2023 wakati wa kikao cha Achidikonary ya Kibaha kilichofanyika mjini Kibaha, Mkoa wa Pwani. Huduma hizo ni pamoja na mazishi, ndoa kipaimara, ubatizo na hata maombi mbalimbali yanayoendana na imani ya dhehebu hilo. Wazazi watakiwa kuhamasisha masomo ya sayansi Kitaifa 19 hours ago "Baba Askofu ameshasisitiza kuhusu hilo hivyo kuanzia sasa sisi wachungaji hatutahusika kutoa huduma hizo kwa waumini ambao watakiuka kanuni hizo," amesema Rogers Mshuza. Mshuza ambaye ni Mchungaji kutoka Kanisa la Anglikana, Sofu Kibaha mkoani Pwani amesema kuwa hivi sasa baadhi ya waumini wamekuwa wakiyumba, leo yuko huku kesho yuko kule jambo ambalo linaweza kuleta mvutano hata kwa viongozi wa madhehebu mengine. Kwa upande wake Kasisi kiongozi Kanisa Ang

WAZIRI MKUU MAJALIWA KUANZA ZIARA MKOANI SONGWE JUMATATU

Image
Waziri Mkuu Kasim Majaliwa anatarajia kuanza ziara ya kikazi Mkoani Songwe ya siku 3 kuanzia tarehe Februari 13,2023 na kuhitimisha Februari 15,2023 ambapo atafanya Halmashauri zote sita za Mkoa wa Songwe. Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Songwe Waziri Kindamba amesema Mkoa wa Songwe tunatarajia kumpokea siku ya tarehe 13,2023 na ataanza ziara katika Wilaya ya Songwe ambapo ataweka jiwe la msingi hospitali ya Wilaya iliopo eneo la kaloreni pia ataongea na Wananchi baada ya hapoo Waziri Mkuu ataongea na Watumishi wa Wilaya ya Songwe katika Ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Mwambani. Kindamba amesema siku inayofuatia ya tarehe Februari 14,2023 Waziri Mkuu atatembelea kiwanda cha Mwekezaji Gdm kilichopo Mlowo na kisha ataelekea makao makuu ya Wilaya ya Momba Chitete ambapo atafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kukagua soko la Kimataifa la Kakozi kisha siku hiyo hiyo ataelekea Halmashauri ya Tunduma ambapo Waziri Mkuu ataongea na Wananchi wa Tunduma eneo la kastamu  pia a

MBUNGE MOMBA APENDEKEZA WAHITIMU JKT WALINDE BARABARA

Image
  Mbunge wa Momba, Condester Sichalwe (CCM) amependekeza Serikali kuajiri vijana waliomaliza mafunzo ya mgambo kulinda barabara zisiharibiwe kwa uchafu. Dodoma. Mbunge wa Momba Condester Sichalwe (CCM) amependekeza Serikali kuajiri vijana waliomaliza mafunzo ya mgambo kulinda barabara zisiharibiwe kwa uchafu. Sichalwe ametoa pendekezo hilo leo Ijumaa Februari 10, 2023 ndani ya Bunge alipouliza swali la nyongeza kuhusu utunzaji wa barabara ambazo zinakuwa na uchafu mwingi kutokana na wasafiri kutupa taka. Mbunge huyo amesema wapo vijana waliomaliza Astashahada na Stashada lakini hawana kazi na hasa waliopitia mafunzo ya JKT ili wanaotupa taka watozwe faini ambazo zitatumika kuwalipa. Naibu Waziri wa Ujenzi Godfrey Kasekenya amesema wazo la mbunge ni zuri hivyo Serikali italifanyia kazi. "Hata hivyo niwaombe waheshimiwa wabunge na Watanzania kuwa, kutupa taka wakati unasafiri ni kosa hivyo tujitahidi kulinda na kutunza mazingira yetu kwa pamoja," amesema Kasekenya. Akijibu swal

RC SONGWE KUANZISHA KAMPENI YA KUTOKOMEZA VITAMBI KWA WATUMISHI MKOANI SONGWE

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Songwe Waziri Kindamba amesema anaanzisha kampeni ya kutokomeza vitambi kwa Watumishi wa Mkoa wa Songwe na Wilaya zote Mkoani humu itakayoitwa "kitambi noma" Akiongea katika kikao cha kutathimini mkataba wa nusu mwaka wa lishe kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Nselewa Mbozi Kindamba amesema kampeni hiyo itakwenda sambamba na kuelimishana juu ya lishe bora. Kikao cha hicho kilihudhuliwa na Viongozi ngazi ya Mkoa na Wilaya pamoja na Viongozi wa chama

ASKARI AFARIKI,MTUHUMIWA APONA KWENYE AJALI

Image
  Kati ya watu 12 waliofariki katika ajali iliyotokea Kongwa mkoani Dodoma wapo askari wawili huku mtuhumiwa   aliyekuwa akisafirishwa na mmoja wa askari akinusurika. Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia leo katika Kijiji cha Silwa kata ya Pandambili wilayani Kongwa mkoani Dodoma. Ajali hiyo imetokea majira ya saa saba usiku ikihusisha lori lililokuwa limebeba Cementi lenye namba za usajili T677 DVX na basi la kampuni ya Frester lenye namba za usajili T 415 DPP lilokuwa likitoka Bukoba kwenda Jijini Dar es salaam Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Alhamisi Februari 9,2023,Kamishana wa Operation na Mafunzo Jeshi la Polisi Tanzania, Awadh Haji amesema katika ajali hiyo kulikuwa na mtuhimiwa aliyekuwa akitokea Mwanza na alikuwa akipelekwa Jijini Dar es salaam. Amesema kwa bahati mbaya askari ajulikanaye kwa jina la Coplo Hamis aliyekuwa akimsindikiza amefariki huku mtuhumiwa akipata majeruhi na wanaendelea kumshikilia. “Mtuhumiwa amepona tupo nae yupo chini ya ulinzi, bahati mbaya tum

BABU WA MIAKA 80 ABAKA MJUKUU WAKE

Image
  Shinyanga. Katika hali ya kusikitisha mzee wa miaka 80 mkazi wa Kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga, Luhende Tungwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake anayesoma Shule ya Msingi Old Shinyanga (jina limehifadhiwa) baada ya kutoka shule. Tukio hilo limetokea jana mchana baada ya mwanafunzi huyo kutoka shule na kumkuta babu yake, huku bibi akiwa ameenda shambani, ndipo mtuhumiwa aliamua kutumia fursa hiyo kufanya kitendo hicho dhidi ya mjukuu wake. Kwa upande wake, bibi wa mjukuu aliyefanyiwa ukatili huo, Mariam Kishiwa mkazi wa Kijiji cha Ihapa amesema alikuwa shambani na baada ya kurudi na kumuona mtoto anaumwa, alimhoji na kumjibu kwamba alipoamechomwa na mti sehemu za siri. Hata hivyo baada ya kumwangalia alikuta anatiririka damu, alichukua jukumu la kumpeleka shuleni alimkuta mwalimu mkuu na kumwambia kuwa mtoto ameumia. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Old Shinyanga, Judith Julias baada ya kumwangalia alibaini mtoto huyo amebakwa, ndipo wakampeleka mw

POLISI ATEKWA APORWA SILAHA

Image
  Polisi mjini Narok wanawasaka watu wawili waliokuwa na silaha wanaoripotiwa kumteka nyara Fredrick Shiundu, Mkuu wa Polisi (OCPD) wa Narok ya Kati Jumanne usiku kisha kumtupa karibu na mto. Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Narok Kizito Mutoro amesema watu hao waliokuwa wamejihami na silaha walikuwa wakimvizia Shiundu nje ya nyumba yake na kumvamia alipofungua mlango wa nyumba yake. “Watu hao walimpokonya silaha Shiundu kabla ya kumfunga kwenye gari aina ya Toyota Wish na kuendesha umbali wa kilomita 17 hadi eneo la Tipis ambako walimpora bastola yake aina ya Jericho ikiwa na risasi 14 kisha kumtelekeza afisa mkuu huyo wa polisi," amesema Mutoro.  Kwa mujibu wa kituo cha Televisheni cha NTV Kenya kimeripoti kuwa, Shiundu aliokolewa na maofisa wenzake siku ya Jumatano asubuhi, ambapo walifuatilia simu yake kwa njia ya mtandao baada ya mkewe kutoa taarifa. Kulingana na Muturo, ambaye anasema yeye binafsi alimhoji Shiundu baada ya tukio hilo, washukiwa hao wa

MWANAFUNZI AKUTWA AMEFARIKI CHUMBANI KWAKE

Image
  Mwanafunzi Philipo Simengo (16) wa Shule ya Sekondari Edward Ole Lekaita, iliyopo Kata ya Namelock wilayani Kiteto Mkoa wa Manyara, amekutwa amefariki dunia akiwa chumbani kwake.Mwenyekiti wa Kijiji cha Njiapanda, Lucas Kilusu Memoi  akizungumza na Mwananchi leo, Februari 8, 2023 amesema  mwanafunzi huyo akiwa na wenzake wawili baada ya kupika chakula alikwenda chumbani kwake na jiko la mkaa kutokana na kuhisi baridi.Amesema ilipofika asubuhi wenzake walimwamsha kwenda shule bila mafanikio na ndipo wakatoa taarifa polisi.Hata hivyo polisi walifika kisha kuingia ndani kwake na kukuta akiwa amepoteza maisha huku damu zikiwa zimemtoka puani na mdomoni. Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi zaidi kutokana na na tukio hilo.

RC SENDIGA: MAAFISA TARAFA NA KATA SIMAMIENI UPANDAJI MITI

Image
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga ametoa agizo kwa Maafisa Tarafa na Kata kusimamia na kuhamasisha kampeni ya upandaji miti kwenye maeneo yao ili kutunza mazingira. Mkuu huyo wa Mkoa ametoa kauli hiyo wakati akizindua kampeni ya mkoa kupanda miti kwenye barabara  na makazi ya watu katika maeneo ya Utengule na Nambogo Manispaa ya Sumbawanga leo (Februari 08,2023). Katika kuhakikisha kampeni ya urejeshaji uoto wa asili mkoani Rukwa inafanikwa Sendiga amezitaka  halmashauri za Nkasi, Manispaa ya Sumbawanga, Kalambo na Sumbawanga kuboresha sheria ndogo ili ziweze kuchua hatua kwa waharibifu wa vyanzo vya maji. “Maafisa watendaji wa kata zote  jukumu lenu ni kwenda kusimamia zoezi la upandaji miti kwenye maeneo yenu. Maafisa Tarafa nendeni pia mkasimamie zoezi hili la upandaji miti Rukwa” alisisitiza Sendiga. Sendiga alisema mkoa huo una changamoto ya utapiamlo ,hivyo sasa ni wakati wa wananchi kupanda miti ikiwemo ya matunda ili kuimarisha lishe ya familia. Katika hatua nyingine Sendiga

NYUMBA ZAIDI 30 ZAEZULIWA NA MVUA YENYE UPEPO MKALI

Image
 Licha ya makazi ya watu pia mvua hiyo imeharibu madarasa mawili  na vyoo vya shule Sekondari Kiva. Handeni. Nyumba zaidi ya 30, madarasa mawili na vyoo vimeezuliwa na mvua wilayani Handeni mkoani Tanga katika mvua zilizonyesha zikiambaytana  na upepo Februari saba Wakizungumza kwenye ziara ya kamati ya siasa ya kukagua maeneo ambayo yameathiriwa na mvua hizo ,baadhi ya waathirika wamesema upepo ulikuwa ni mkali kiasi cha watu kutosikilizana. Mkazi wa Mbwagwi Mwanahamisi Ally amesema kuwa baada ya kuona upepo huo ni mkali sana,aliwaambiwa watoto waliopo ndani wasikimbka na kuwakumbatia ambapo nyumba iliezuliwa bati. Aidha Shabani Yusuph ameshauri wadau kujitokeza kwa kusaidiana na serikali kwenda kuwasaidia chakula kwani wengine hata vyakula vimeharibika. "Vyakula ambavyo tulihifadhi kama akiba pia vimeharibika hivyo wadau kwa kushirikiana na serikali walione hili,na kuja kutusaidia huku mkikumbuka wakati huu hali ni mbaya",ameswma Diwani kata ya Kiva Valentino Mbuji amesema

WATUMISHI NA WAZABUNI 672 MIKONONI MWA TAKUKURU

Image
  Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Angela Kairuki amesema watumishi na wazabuni 672 wamefanyiwa uchunguzi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) huku akidai wameanza kuwachukulia hatua waliotajwa na CAG.  Kairuki ameyasema hayo leo Februari 7,2023 wakati akichangia taarifa ya utekezaji wa shughuli za kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC). Amesema kuwa wameshaanza kuchukua hatua kwa watumishi waliotajwa katika ripoti ya CAG kupitia sektarieti za mikoa na Takukuru. Amesema wamepata mrejesho kutoka kwa Mkurugenzi wa Takukuru kuwa watumishi na wazabuni 672 wameshafanyiwa uchunguzi na taasisi hiyo. “Wazabuni na watumishi 46 uchunguzi umeshakamilika kutokana na kutodhibitika kwa tuhuma zao lakini watumishi na wazabuni 53 majalada yao yako kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kuomba kibali wafikishwe mahakamani,”amesema Kairuki. Amesema watumishi na wazabuni 51 mashtaka yao yako mahakamani na kuwa yot

SENEDA AWAONYA WANAOWABEZA WALIMU SONGWE, ILEJE YAWAPONGEZA WAALIMU KWA KUWAFANYIA SHEREHE

Image
  Wakuu wa Idara ya elimu msingi na sekondari katika halmashauri za mkoa wa Songwe wameonywa kujiepusha na tabia ya kutoa kauli zisizofaa Kwa walimu  pindi wanapowasilisha changamoto zinazowakababili bali wajenge daraja litakalosaidia kuoandisha kiwango Cha ufaulu.        ( Katibu Tawala Seneda katikati kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje Farida Mgomi na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe akicheza Muziki pamoja na Waalimu) Hayo yamesemwa na katibu Tawala mkoa wa Songwe Happiness Seneda wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu wa shule zilizofanya vizuri Kwa matokeo ya darasa la Saba 2022 wilayani Ileje ikiambatana na kutoa vyeti vya pongeza ,fedha , na majiko ya gesi Kwa shule zilizopo katika mazingira magumu. Hafla hiyo imefanyika Februari 4, 2023 katika ukumbi wa RM  Itumba ikiandaliwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo kwa lengo la kuendeleza ufaulu ambao umepanda kutoka 56% mpaka 65%          ( Afisa Elimu Mkoa wa Songwe) Happiness amesema mkoa wa Songwe upo katika