Posts

Showing posts from July, 2024

KINDAMBA AWATAKA WAGANGA WAFAWIDHI VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI ILEJE KUKUMBUKA WAJIBU WAO

Image
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Bi. Nuru Waziri Kindamba mapema leo Julai 29,2024 ameongea na Waganga Wafawidhi wa Hospitali, Vituo vya Afya pamoja na Zahanati zilizopo wilayani hapa ambapo ametumia fursa hiyo kuwakumbusha juu ya uwajibikaji pamoja na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Bi. Kindamba ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo maalumu ya mifumo mbalimbali ya utendaji kazi za Serikali kwa Waganga Wafawidhi wa Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati wilayani hapa. Aidha, Mkurugenzi Mtendaji Kindamba amesisitiza juu ya umuhimu wa utunzaji wa vifaa sambamba na kuzingatia maslahi ya watumishi wenza pamoja na wateja (wagonjwa) wanaopatiwa huduma. Mafunzo hayo yanalenga kuwaongezea uwezo Waganga Wafawidhi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kama ilivyo miongozo ya Serikali, miongoni mwa mifumo waliyojifunza ni pamoja na Gothomis na Nest ambayo yote inatumika kutekeleza miradi mbalimbali ya Serikali

MBUNGE SHONZA ATOA MISAADA YA ZAIDI YA MILIONI 3.KWA WAJAWAZITO NA WATOTO AKISIFU KAZI ZA RAIS SAMIA

Image
 ATOA MISAADA YA ZAIDI YA MILIONI 3.KWA WAJAWAZITO NA WATOTO AKISIFU KAZI ZA RAIS SAMIA. Mbunge viti maalum mkoa wa Juliana Shonza (CCM) ametoa wito kwa watumishi idara ya afya mkoani Songwe  kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa Shonza aliyasema hayo jana wakati akigawa vifaa kwa kina mama wajawazito na watoto katika hospitali ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe  psmoja na kukagua ujenzi wa jengo la mama na mtoto ambalo linajengwa kwa  Milioni 900. Alisema siku za nyuma akiwa na uongozi wa chama alifika hospitalini hapo na kukuta kero nyingi ikiwemo lugha za matusi kwa wajawazito wanaofika hapo kujifungua. Alisema mgonjwa anahitaji faraja ili aweze kujifungua salama na hilo alilifikisha kwa waziri wa afya Ummy Mwalimu hali iliopelekea  watumishi wengine kuhamishwa katika hospitali hiyo. "" Nawaomba tuwe na lugha za staa kwa akina mama hawa, na ni marufuku pia kuwatoza fedha akina mama wajawazito na watoto Dkt Samia analeta fedha nyingi ili kuwasaidia Wajawazito hawa kwa kuwajengea m

RAIS ATENGUA WENYEVITI NA WATENDAJI WAKUU TTCL,UCSAF NA POSTA

Image
 

WAZAZI WAMETAHADHALISHWA KUWA KARIBU NA WATOTO WAO

Image
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya ametoa tahadhali kwa wananchi kuhusiana na taarifa zinazozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba watoto wanatekwa kwa kuwaambia wananchi wote kuendelea kuwa karibu na watoto wao na kuhakikisha wanafahamu watoto wao walipo ili kuwafanya kuwa salama wakati wote. Ameyasema hayo Julai 23, 2024 alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisini kwake na kusema alipokea taarifa kutoka kwa Kondakta wa basi la AM Safari linalofanya safari zake kutoka Kigoma kwenda Dodoma hadi Dar es Salaam kwamba kuna mtoto ametelekezwa kwenye basi hili aitwaye Lightness Taifa (3) na jitihada za kuwatafuta wazazi wake zimefanyika kuweza kumkabidhi mtoto huyo. "Mtoto huyo alipotea katika mazingira ambayo mama wa mtoto alienda kumtafutia chips mtoto wake na baada ya kurudi hakumkuta kumbe mtoto huyo alimfuata mama yake bila ya mama yake kujua na ndipo alipopotea hadi alipokuja kupatikana kwenye basi la AM Safari a

UTEUZI,NAPE,MAKAMBA WATENGULIWA,KIKWETE WAZIRI KAMILI,SILAHA APEWA KITI CHA NAPE

Image
 

MIL 900 KUJENGA KITUO KIPYA CHA AFYA, MLOWO,MBOZI

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali itapeleka shilingi Mil 900 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwa ajili ujenzi wa Kituo cha Afya kitakachotoa huduma kama Hospitali ya Wilaya. Waziri Mchengerwa ameyasema hayo alipokua akizungumza na Wananchi wa Mlowo Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe wakati Mhe. Rais aliposimama kuwasalimia wananchi katika Wilaya hiyo. Amesema Mhe. Rais katika Jimbo hili kuna Hospitali ya Wilaya pamoja na vituo vya Afya 5 lakini kutokana na wingi wa watu waliopo hapa umetuelekeza tulete fedha kwa ajili ya Kituo cha Afya kipya na sisi Mhe. Rais tunatekeleza na fedha hiyo itaingia ndani ya mwezi huu. Ujenzi wa Kituo hiki utafanya sasa Idadi ya Vituo vya Afya katika Wilaya hii kufikia 6 na Kituo hiki kitawekewa vifaa Tiba vyote muhimu ambavyo vitawezesha upatikanaji wa huduma bora za Afya’ alisema Mhe. Mchengerwa

POLISI WATAKIWA KUTUNZA AFYA YA AKILI

Image
Naibu Balozi wa Ireland nchini MAGS GAYNOR amewataka askari Polisi kutunza afya ya akili jambo litakalowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Ameyasema hayo leo tarehe 19.07.2024 katika Shule ya Polisi Tanzania -Moshi wakati akifunga mafunzo ya siku tatu awamu ya pili ya kuwajengea uwezo watendaji wa madawati ya jinsia nchini wa namna ya kukabiliana na makosa ya unyanyasaji kingono hasa kwa watoto. Aidha, Naibu Balozi huyo ameeleza kuwa Jeshi la Polisi Tanzania lina jukumu la kuwalinda watoto na kwamba wako tayari kuendeleza ushirikiano baina ya Nchi ya Ireland na Tanzania katika kufanikisha hayo. Naye, Kamishna wa Polisi jamii nchini, FAUSTINE SHILOGILE amewataka wahudhuriaji wa mafunzo hayo kuthamini kwa vitendo mchango wa muda na raslimali uliotolewa na wawezeshaji wa mafunzo hayo kutoka ubalozi wa Ireland kwa kwenda kuyafanyia kazi yote yaliyofundishwa. Pia, amewataka kwenda kutoa elimu kwa watendaji wengine ambao hawakupata nafasi ya kuhudhuria mafunzo hayo ili kuwa na uel

RC DODOMA ASHIRIKI HAFLA FUPI YA MAKABIDHIANO MRADI WA BILIONI 19 BBT CHINANGALI 2

Image
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameshiriki hafla fupi ya Makabidhiano ya Eneo la Mradi wa Chinangali II kwa Mkandarasi STC COMPANY LIMITED akishirikiana na PRO AGRO GLOBAL LIMITED. Mradi huo wenye thamani ya shilingi Bilioni 19 utatekeleza kwa Ujenzi wa Bwana moja, Ufungaji wa Miundombinu ya umwagiliaji kwenye shamba la ukumbwa wa ekari 560, Uchimbaji wa visima 29, ufungaji wa pampu za visima, Ujenzi wa Barabara zilizopo mashamba zenye Jumla ya kilomita 28, ujenzi wa miundombinu ya barabara kilomita 75, Ulazaji wa mabomba ya mfumo wa umwagiliaji yenye kilomita 9.4, Ujenzi wa mifereji ya umwagiliaji katika mashamba pia ununuzi wa gari moja kwa ajili ya usimamizi.

TUME HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA WAMTIA HATIANI MAKONDA,GEKUL NA HALMASHAURI YA MBOZI WASALIMIKA

Image
 DODOMA: TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imebaini ukiukwaji wa sheria na taratibu kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kuhusu amri aliyoitoa kukamatwa mkazi wa mkoa huo hivi karibuni. - Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu ameeleza hayo kwa waandishi wa habari mkoani Dodoma leo wakati akisoma taarifa ua chunguzi mbalimbali zilizofanywa na tume hiyo. - Katika uchunguzi iliyoufanya tume hiyo kuhusu Mkuu huyo wa mkoa iliyohusu tuhuma dhidi yake ya kutoa amri kukamatwa na kuwekwa mahabusu mkazi wa Mkoa wa Arusha kinyume na utaratibu wa kisheria mnamo Juni 2024, tume imebaini kuwa amri iliyotolewa na Mkuu huyo ya kumkamata na kumuweka ndani mkazi huyo haikuwa halali na haikuzingatia aina ya makossa na utaratibu ulioainishwa kisheria wa utekelezaji wa mamlaka hay. - Katika hatua nyingine Tume ilichunguza malalamiko dhidi ya Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul na wenzake kudaiwa kuwafanyia vitendo vya ukatili na udhalilishaji Hashim Ally na Michael Isaria kwa kuw

NOEL MAGARI DALALI MWENYE NDOTO ZA KUWA BILIONEA MKOA SONGWE

Image
  Mkoa wa Songwe ni Mkoa kitinda mimba nchini Tanzania ambao uchumi wake umeonekana kukua kasi  na vijana wa mkoa wa Songwe wamekuwa ni Vijana wakuchakalika usiku na mchana ili kuweza kujikwamua kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja. Katika angaza angaza yetu tunakutana na kijana Noel Mzumbwe anaejulikana hivi sasa kama Noel Magari kutokana na kujikita katika biashara ya kuuza magari iliompa umaarufu mkoani Songwe na mikoa mbali mbali nchi Tanzania. Ukishuka Mji mdogo wa Mlowo ulipo Wilayani Mbozi makao makuu ya mkoa wa Songwe bila shaka ukiuliza tu Noel magari lazima utaonyeshwa aidha ofisini kwake au kijiweni kakaa akiendeleza shughuli zake za udalali wa magari. Akiongea na Mwandishi wetu magari kwanza ameishukuru serikali ya awamu sita chini yake na Daktari Samia Suluhu Hassani kwa kuwajali Vijana na kuwapa mazingira rafiki ya kujitafutia ridhiki zao za halali ili mradi tu ulipe kodi ya serikali "Ndugu mwandishi asingekuwa Samia sijui ningekuwa wapi maana Mazingira haya tulivu ya awamu

WAZIRI JAFFO: TUTAHAKIKISHA TUNATATUA CHANGAMOTO ZA KIBIASHARA MIPAKANI

Image
  Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema kuwa Wizara yake itahakikisha inatatua changamoto za kibiashara katika maeneo ya mipakani ili sekta ya viwanda na biashara iweze kukua  Dkt. Jafo amesema hayo Julai 18, 2024 wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliposimama kuwasalimia wananchi wa mji wa Tunduma Mkoani Songwe alipopita akitoka katika ziara yake Mkoa wa Rukwa Amesema kuwa Wizara hiyo itahakikisha inatakeleza maagizo yaliyotolewa na utekelezaji wa Maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokutana na Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema katika ziara ya Kitaifa nchini humo Oktoba 23 - 25, 2023 yanayohusu utatuzi wa changamoto za biashara katika mpaka wa Tunduma. Aidha, Jafo amebainisha kuwa kati ya changamoto 15 zilizokuwepo katika mpaka huo, changamoto nne (4) tayari zimeshafanyiwa kazi huku akiahidi kuwa changamoto zingine zinaendelea kufanyiwa kazi. Akifafanua zaidi, Dkt. Jafo amesema kuwa changamoto ya

WIZARA YA AFYA YATOA TAMKO AGIZO LA RAIS TUNDUMA JUU YA MTOTO MLEMAVU

Image
 Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema wao kama Wizara wamelipokea agizo la Rais Dkt Samia alilolitoa mapema leo asubuhi tarehe 18.07.2024 akiwa Mkoani Songwe katika Mji wa Tunduma kuhusu mtoto mwenye ulemavu wa miguu mmoja "Tumepokea kwa ajili ya Utekelezaji mara moja Maelekezo ya Mhe Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan kuhusu Mtoto Ebenezer Wile Mwaksyle (8) ambaye ni mlemavu kupatiwa huduma ya kutengenezewa Mguu Bandia, pamoja na huduma bora za afya. Tunamshukuru Mhe Rais kwa upendo wake wa dhati na moyo wa huruma kwa wananchi wake" ameandika Waziri Ummy

MZEE WA MIAKA 63 AUWAWA MBOZI NA KUNYOFOLEWA VIUNGO VYAKE

Image
Watu wasiojulikana wamemuuwa Mzee Kuminya Sambo (63) mkazi wa kijiji cha Nambizo wilayani Mbozi Mkoani Songwe huku viuongo vya mwili wake ikiwepo mguu na mkono vikiwa vimenyofolewa kandokando ya barabara. Baadhi ya ndugu wa marehemu pamoja na majirani wamesema mauaji ya Mzee Sambo ambaye alikuwa akiishi bila mke  yamewashitua huku wakiomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi na kujuwa chanzo cha mauaji hayo. Mwananchi imefika nyumbani kwa marehemu na kuzungumza na mtoto wa marehemu Jose Kuminya Sambo ambaye amesema baba yake alikutwa ameuwawa kandokando ya barabara baada ya kupotea nyumbani kwa takribani siki 3 na wananchi kumtafuta bila mafanikio. Amesema Mzee Sambo alipotea nyumbani nyakati za usiku Julai 9, 2024 hali iliyopelekea wananchi kuungana kumtafuta kwa siku 3 bila mafanikio ambapo Julai 11,2024 walimkuta akiwa ameuwawa kandokando ya barabara huku mguu moj na mkono vikiwa vimenyofolewa. Grace Sambo mtoto wa marehemu amesema baada ya baba yao kupotea walifika nyumbani kwao na k

MAAFISA ARDHI ILEMELA MATATANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani humo kuwakamata Mkuu wa Idara ya Ardhi wa Manispaa ya Ilemela Grace Masawe pamoja na Afisa Mipango Miji Mwajuma Mabula kwa tuhuma za kuomba Rushwa. Mhe. Mtanda ametoa agizo hilo leo tarehe 16 Julai, 2024 Mtaa wa Igoma kwenye Mkutano wa kusikiliza na Kutatua kero za wananchi na ndugu Matiko Migire kuwasilisha kero kwamba watumishi hao wamemuomba rushwa ya Tshs. 2,430,000 ili wafanye upimaji wa viwanja na. 311, 312 na 313 Block A Pasiansi. Mhe. Mtanda amesema kitendo hicho si cha kiungwana na kinawanyima haki wananchi hivyo wakati TAKUKURU wanalichunguza suala hilo Idara ya ardhi amewapa siku saba kukamilisha Upimaji wa viwanja hivyo kwani wamemzungusha kwa muda mrefu mteja huyo anayefuatilia bila mafanikio. Awali, akiwasilisha kero hiyo kwa Mkuu wa Mkoa, Matiko alifafanua kuwa 2019 Halmashauri hiyo iliomba Hati za viwanja hivyo na kuzifuta na kuahidi kufanya upimaji m

KASEKENYA ATOA MIEZI MIWILI UJENZI OSBP KASUMULU UKAMILIKE

Image
Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya ametoa muda wa miezi miwili kwa Mkandarasi M/S China Geo Engineering Corporation, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), na Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Mbeya kuhakikisha ujenzi wa Kituo cha huduma ya pamoja mpakani (OSBP), cha Kasumulu katika mpaka wa Tanzania na Malawi kinakamilika ifikapo Septemba mwaka huu.   Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo Eng. Kasekenya ameelezea kutoridhishwa kwake na kasi ya ujenzi huo na kumtaka Mkandarasi, Msimamizi, TANROADS na TBA kukutana haraka kutafuta ufumbuzi ili kituo hicho kikamilike kwa wakati na hadhi ya kimataifa ili wananchi na wasafirishaji wanufaike kwa huduma za kisasa.   “Fahamuni mko nyuma ya muda, hivyo ongezeni wataalam, wafanyakazi, muda wa kufanya kazi ikiwezekana iwe usiku na mchana na vifaa vinavyostahili vyote viwepo site ili nikija Septemba mnikabidhi kituo kilichokamilika na wananchi na wasafirishaji waanze kunufaika na huduma za kisasa “, amesisitiza Eng.

MKUU WA MKOA WA RUVUMA KANALI AHMED ABBAS AMEIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA NAMTUMBO KWA KUPATA HATI SAFI

Image
Akizungumza wakati wa mkutano maalum wa kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali leo Julai 15, 2024 uliofanyika katika ukumbi wa makao makuu ya halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bi Rehema Madenge amesema ;- “. Nitumie fursa hii kuipongeza Halmashauri hii ya Wilaya ya Namtumbo kwa Kupata Hati safi”. Bi Rehema Madenge amewaelekeza Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji na Waheshimiwa madiwani kuendelea kusimamia na kuhakikisha hakuzalishwi hoja wakati wa ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali – CAG Mwaka 2024/2025. “Nataka wakuu wa idara wote washiriki kikamilifu katika suala zima la kuzuia uwepo wa hoja na kuzijibu hoja za ukaguzi, Endeleeni kusimamia vyema ili Hoja hizo kujirudia" :- Rehema Madenge, Kikao hicho cha kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali – CAG kimefanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

BASI LA NGASSERE LATUMBUKIA MTONI SONGWE WAWILI WAPOTEZA MAISHA

Image
  Basi la Kampuni ya Ngasele lilokuwa likitokea Dodoma kuelekea Tunduma limetumbukia mtoni Mji wa Mlowo kijiji cha Myovizi Wilayani Mbozi Mkoani Songwe na jitihada za uokozi zinaendelea. Kwa mujibu wa Kaimu kamanda msaidizi wa Polisi Mkoa wa Songwe ACP GALLUS HYELA amesema watu wawili wamepoteza maisha na wengine watano wamejeruhiwa vibaya akiwemo dereva wa basi na wamekwisha kimbizwa hospitali. kamanda amesema chanzo cha ajali hilo ni dereva wa basi hilo alikuwa akilikwepa gari linguine ndio alipogonga ukingo wa daraja hilo na kudumbukia mtoni.

WANANCHI WAMETAKIWA KUITUMIA VIZURI MITANDAO YA KIJAMII

Image
  WANANCHI wametakiwa kutumia vizuri mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na kuepuka kuweka taarifa zao za siri ili zisidukuliwe na watu wenye nia ovu na wakazitumia kwenye matukio ya uhalifu. Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Tekonojia ya Habari, Maryprisca Mahundi, alitoa wito huo mwishoni mwa wiki alipozungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mbeya (CUoM) pamoja na wahadhiri. Alisema baadhi ya watu wamekuwa wakidukua taarifa muhimu za watu wengine kwenye mitandao na kuzitumia kukopa fedha kwenye taasisi zinazokopesha kupitia mitandao na kuwaweka wahusika kama wadhamini. Alisema wanaposhindwa kurejesha mikopo hiyo ndipo taasisi hizo zinaibuka na kuanza kutuma jumbe zenye vitisho na hapo ndipo wahusika wanaanza kushtuka na kulalamika bila kujua kwamba walisababisha wao wenyewe kwa kuweka taarifa zao muhimu mitandaoni. “Hivi karibuni Rais Samia alituzindulia taasisi ya kulinda taarifa binafsi, lakini bado kuna watu ni watundu huko kwenye mitandao, wanaweza kuchukua taarif

IMANI ZA KISHIRIKINA NI CHANZO KIKUBWA CHA UKATILI KATIKA JAMII

Image
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya amesema imani za kishirikina zinachangia kwa kiasi kikubwa kuendelea kwa ukatili uliokithiri katika jamii hivyo ameitaka jamii kuepukana na imani hizo kwani zinapelekea migogoro katika jamii pamoja na mauaji. Ameyasema hayo Julai 14, 2024 alipokuwa akiongea na waumini wa Kanisa la Efatha lililopo Kisasa Jijini Dodoma na kuwaeleza kuwa tumtegemee mwenyezi Mungu katika kila kitu na kuachana na tamaa ya Mali inayopelekea kwenda katika imani za kishirikina na matokeo yake ni mauaji. Kamanda Mallya amesema kitu kingine kinachopelekea kuwepo na ukatili uliokithiri ni ulevi uliopitiliza na wivu wa mapenzi ambao hupelekea vipigo na matusi jambo ambalo husababisha ukatili wa kijinsia, ubakaji, kulawiti, kujeruhi pamoja na mauaji. Katika hatua nyingine Mamanda Mallya amewataka wazazi kuwa karibu na watoto wao ili kubaini changamoto za ukatili wanazokumbana nazo ikiwemo ukatili wa kijinsia, ubakaji na

WATAALAMU KUTOKA ZHEJIANG NORMAL UNIVERSITY WAENDESHA MAFUNZO KWA WAKUFUNZI WA ADEM

Image
Timu ya Wataalamu 11 ikujumuisha maprofesa na Madaktari kutoka Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal University cha nchini China wamefika ADEM leo tarehe 9 Julai, 2024 kwa ajili ya ziara maalumu ikiwa ni hatua ya kuanza kwa utekelezaji wa mkataba wa ushirikiano ulioingiwa kati ya ADEM na chuo kikuu cha Zhejiang Normal University mnamo Mwezi Desemba, 2023 uliolenga kubadilishana utaalam, ufadhili wa masomo ya Muda Mfupi na Mrefu, kutembeleana ili kujifunza, kufanya tafiti nk. Wataalamu hao wataendesha mafunzo ya siku tatu kwa Wakufunzi wa ADEM kuhusu Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu hasa eneo la Instructional Leadership na Uthibiti Ubora wa Elimu ili kuwajengea uwezo katika maeneo hayo. Katika ufunguzi wa programu hiyo ya mafunzo, Dean college of Education ZJNU Prof. Huang Xiao ameshukuru Menejimenti ya ADEM kwa kukubali ushirikiano na Chuo Kikuu cha ZJNU ambao utaleta matokeo chanya kama pande zote mbili zilivyokubaliana namna ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kitaaluma zitaka

KATIBU MKUU NISHATI AWATAKA TANESCO KULEGEZA BEI YA UMEME ILI WANANCHI WAPIKIE NISHATI YA UMEME

Image
  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) sanjari na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kulegeza bei ya umeme, ili mwananchi asiogope kupikia umeme badala ya nishati nyingine. Akiwa katika ziara yake kutembelea Banda la Wizara ya Nishati sambamba na mashirika na taasisi zilizo chini yake katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba 2024) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, vilivyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, Mramba amesema ni lazima wananchi wawe na machaguo mengi ya aina ya nishati wanayotaka kupikia ima umeme, gesi ama mkaa. “Umeme ndio nishati safi zaidi kulinganisha na nishati nyingine kama gesi na mkaa, lakini ili mwananchi aweze kutumia umeme ni lazima umeme uwe wa bei nafuu, “Kinachonisumbua ni kwamba mwananchi anakuwa na umeme nyumbani lakini umeme sio chaguo lake la kupikia, hii sio sahihi, Mfano watu wengi wa Dar es Salaam wana umeme, nilitaka wawe na uwezo wa kutumia ume

ADAI KUMNG'OA MENO MKEWE KISA SHILINGI 200

Image
  JESHI la Polisi mkoani Mara linamshikilia mkazi mmoja wa Kijiji cha Nyakatende wilayani Musoma, Musa Abdallah kwa tuhuma za kumn'goa meno matatu mke wake kwa kutumia ‘pliers’ kwa kile kilichoelezwa ni ugomvi wa Sh. 200. Inadaiwa mtuhumiwa huyo ambaye ni mganga wa kienyeji alitenda ukatili huo baada ya mke wake huyo kutumia fedha hizo, zilizotokana na mauzo ya mahindi kununua mahitaji ya mtoto wao mdogo bila idhini yake. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Salum Morcase, alithibitisha tukio hilo akisema mtuhumiwa huyo akisaidiana na mke wake mwingine ambaye bado hajatiwa nguvuni walimkamata mke mdogo wakamlaza chini na kisha mume wake akamn'goa meno matatu. "Mtuhumiwa huyo akisaidiana na mke wake wa pili walimshika mama huyo na kumlaza chini huku wakiwa wamemshikilia ambapo kwa kutumia pliers aliweza kutenda ukatili huo na kumsababishia maumivu makali," alisema. Kamanda Morcase alisema hata hivyo, baada ya kutenda ukatili huo mtuhumiwa huyo ambaye yuko mikononi mwa polis

SAUTI YA SIMBA DAVID SILINDE KUANZA KUUNGURUMA JIMBONI TUNDUMA SIKU SABA KUANZIA LEO

Image
  Mbunge wa Jimbo Tunduma David Silinde ambae pia ni Naibu Waziri wa Kilimo anatarajia kuanza ziara ya siku saba za Jimbo kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali jimboni mwake ikiwa sambamba na kufanya Mikutano ya hadhara lengo likiwa ni kuwaelezea Wanatunduma fedha za miradi mbalimbali walizopewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassani katika Jimbo la Tunduma. Katibu wa Jimbo wa Silinde Zamana Simkwai amesema leo Jumatano 10.07.2024 ndio Mbunge anaanza rasmi ziara yake na ataanzia kata ya majengo ambapo atafanya Mikutano miwili  mmoja ikiwa Soko la kimataifa la mazao ambapo ataongea na wafanyabiashara wa mazao ili kuwasikiliza kero zao kisha jioni siku hiyo hiyo atakuwa soko la majengo pia kusikiliza kero na kuyaelezea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita. Simkwai amewaomba Wananchi wa Jimbo la Tunduma kujitokeza kwa wingi katika Mikutano ya Mbunge na kuja na kero zao mbalimbali ili wazitatue kwa pamoja "Mbunge wetu sauti ya Simba David Silinde amewataka Wananchi wa Jimbo l

WANACHAMA 80 WAIKACHA CHADEMA MOMBA

Image
Wanachama zaidi ya themanini (80) wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kata ya Kamsamba Halmashauri ya Momba mkoani Songwe wamejiunga na CCM kwa madai kuwa wameridhishwa na utedaji kazi wa Serikali ya awamu sita inayo ongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Wakipokelewa mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kata ya Kamsamba na mbele ya Mbunge wa Jimbo la Momba Mhe. Condester Sichalwe baadhi ya wanachama hao wamesema wameona hakuna haja ya kusalia Chadema, kwani CCM ya sasa chini ya viongozi wake wa Serikali wanafanya kazi kubwa ya kuwaletea wananchi maendeleo.  Mmoja wa Wanachama hao ambao wamejiunga na CCM Joseph Simfukwe, ambaye pia amewahi kuwa mwenyekiti wa kijiji cha Muungano kupitia tiketi ya CHADEMA, amesema kwa iyari ya moyo wake bila kushinikizwa na mtu yeyote ameona ni vema kurudi CCM ili kuunga mkono jitihada za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita. “Kwa kazi kubwa zinazofanywa na Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge wetu Condester Sicha

RC NAWANDA APANDISHWA KIZIMBANI,AACHIWA KWA DHAMANA

Image
 Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza imemuachia kwa dhamana aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Nawanda leo July 09,2024 baada ya kupandishwa kizimbani katika Mahakama hiyo na kusomewa shtaka moja la kulawiti. Dkt. Nawanda amepandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Erick Marley na kusomewa shtaka hilo na Waendesha mashtaka wa Serikali, Magreth Mwaseba na Martha Mtiti. Kwa mujibu wa Mwaseba, Mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 154 (1) (a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16. “Mshtakiwa, Yahaya Nawanda, Mkazi wa Nyamata Wilaya Bariadi Mkoani Simiyu unashtakiwa kwa kosa la kumwingilia kinyume na maumbile kumlawiti Tumsime Ngemela, kosa ulilolitenda June 02, 2024 eneo la maegesho ya magari lililoko Rocky City Mall Wilayani llemela Mkoani Mwanza” Mara baada ya kusomewa shtaka hilo, Dkt. Nawanda aliambiwa dhamana ya shtaka lake ipo wazi ambapo amekidhi masharti na kuachiwa kwa dhamana hadi shtaka hilo litakapotajwa t

MWALIMU JELA MIAKA 30 KWA KURUHUSU KULAWITI NA WANAFUNZI MTWARA

Image
  Mwalimu wa Shule ya Sekondari Naputa Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara,Ramadhani Nanyalika amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mtwara, Issa Suleiman amesema mwalimu huyo siku za nyuma alijenga urafiki shuleni na mwanafunzi wa kidato cha nne mwenye umri wa miaka 19 ambaye jina lake limehifadhiwa kwa kuanza kumnunulia vitafunwa shuleni na kumtaka akamtembelee nyumbani. Amesema mwalimu huyo alimtaka mwanafunzi huyo akamtembelee nyumbani na alipoenda alianza kumuonyesha video chafu kupitia simu janja na baadae kumtaka amuingilie kinyume na maumbile. Baada ya mwanafunzi huyo kuambiwa hivyo alikataa na kusema hawezi kufanya kitendo hicho ndipo mwalimu akaanza kumtisha kwa kumwambia asipofanya hivyo atapata adhabu kali mara kwa mara shuleni pamoja na kufukuzwa shule. Baada ya vitisho hivyo mwanafunzi huyo alilazimika kutekeleza kitendo hicho pasipo ridhaa yake. Katika hatua

MBUNGE AMKOSHA KATIBU CCM MOMBA AWAAMBIA WANAMOMBA WASIJARIBU KUKOSEA

Image
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Momba Ndg. Kataba Sukuru amewataka wananchi wa Jimbo la Momba kuendelea kumuamini na kumpa muda mrefu wa kuwatumikia Mbunge wao wa Jimbo la Momba Mhe.Condester Sichalwe (Mundy). Sukuru ametoa shukrani na pongezi hizo leo Julai 7 mwaka 2024 wakati akiwa mgeni mwalikwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kata ya Msangano. Amesema kuwa Momba ni miongoni mwa majimbo hapa nchini ambayo imebahatika kupata Mbungemchapakazi na mwenye mapenzi mema na wananchi wake. “Wananchi wa Momba, sisi chama cha Mapinduzi tunajivunia sana kuwa na Mbunge Condester, maana anawatengea haki wananchi, kwanza anafanya kazi kwa kujituma , pili anawapenda sana wanchi, maana kila Mbunge likiisha lazima afike jimboni na kuwasalimia watu wake, hakika huyu Mbunge mwenye kupigiwa mfano” Kataba

MBUNGE MOMBA KUTOA SHILINGI MILIONI 28 UJENZI WA OFISI ZA CCM KATA 14

Image
 MBUNGE wa Jimbo la Momba Mkoani Songwe Mhe. Condester Sichalwe (Mundy) ametenga kiasi cha shilingi milioni 28 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ofisi za CCM kwenye kata zote 14 za jimbo hilo. Akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye vikao vya Halmashauri Kuu ya CCM kata za Nkangamo na Msangano, Mbunge Sichalwe amesema lengo la kutoa fedha hizo ni kuunga mkono shughuli za maendeleo za kujenga chama hicho. Akiwa mgeni mualikwa kwenye kikao hicho katibu wa CCM wilaya ya Momba Kataba Sukuru, amempongeza na kumshuru Mbunge Condester Schalwe kwa kutoa fedha hizo kwa madai kuwa anajenga chama kwa vitendo. “Tukushuru sana Mheshimiwa Mbunge jambo hili unalofanya nikubwa sana, kutoa milioni mbili kila kata si jambo dogo, inaonyesha ni jinsi gani unavyokipenda chama chetu, hakika wewe ni Mbunge wa mfano sana” Kataba. Kupitia mpango huo tayari Mbunge ametoa milioni Nne kwa kata mbili za Nkangano na Msangano, huku akiendelea na kata zingine, lengo ni kuona kata zote zinafikiwa na fedha hizo.

DED MALINYI AONGOZA TUMU YAKE KUSIKILIZA NA KUJIBU KERO ZA WANANCHI

Image
   Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Bi. Rose Robert Manumba ameongoza timu ya Wataalam kutoka Halmashauri kusikiliza na kujibu Kero za Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Njiwa. Kero mbalimbali zilizoibuliwa na Wakazi wa njiwa ni pamoja na kutaka ufafanuzi wa huduma za afya, Migogoro mbalimbali ya ardhi kati ya vijiji, taasisi na mtu mmoja mmoja,Stakabadhi ghalani, hatma ya vitongoji halali vilivyopo maeneo ya hifadhi,Migogoro ya wakulima na wafugaji. Baadhi ya kero hizo zilipatiwa majibu ya hapo kwa hapo na Mkurugenzi pamoja na Wataalam kutoka Halmashauri na nyingine Mkurugenzi Aliahidi kuwasilana na Tasisi husika na atawarejea Wananchi kwa majibu ndani ya muda mfupi. "Niwahakikishie Wananchi wa Njiwa yale yote niliyoyachukua kwaajili ya utekelezaji nitaenda kuyasimamia ipasavyo,kuna yale ambayo nimeyatolea muda kwaajili ya utekelezaji nitatimiza ahadi yangu, na hata yale ambayo sikuyatolea muda niwahakikishie kwamba naenda kufanya ufuatiliaji wa ki

MSIMAMIZI WA VIKOSI MAALUMU VYA POLISI ATUA SONGWE

Image
  Mkuu wa usimamizi Vikosi Maalum vya Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ferdinand Mtui kutoka Kamisheni ya Operesheni na Mafunzo, Makao Makuu ya Polisi Dodoma leo Julai 06, 2024 amewasili Mkoa wa Songwe na kufanya kikao na Maafisa wa Polisi Songwe. Naibu Kamishna Mtui yupo ziarani mikoa ya nyanda za juu kusini kuangalia na kukagua hali ya ulinzi na usalama wa bomba la mafuta la Tazama Pipeline katika mikoa iliyopitiwa na bomba hilo.

SILINDE AFANYA ZIARA IRINGA YA UKAGUZI

Image
  Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) amekagua kituo cha Seatondale kinachosimamiwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kwenye kituo cha Kifyulilo kilichopo Iringa mjini na kukagua Kampuni ya Chilongola Agro Forest and Livestock Limited iliyopo Mafinga, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa ambalo ni shamba la vijana wanaojihusisha na uzalishaji wa miche bora ya parachichi. Ziara hiyo imefanyika tarehe 6 Julai 2024 ikiwa ni maandalizi ya kumpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) ambaye atatembelea maeneo hayo tarehe 7 Julai 2024. Kituo cha Seatondale ni miongoni mwa vituo vidogo vinavyotumika kufanyia majaribio ya mazao ya kilimo kutoka vituo vingine vya utafiti vya TARI pamoja na wadau wengine wa Sekta ya Kilimo. Kituo cha Seatondale kipo katika ukanda wa futi 5,463 (mita 1,665) toka usawa wa bahari na kinapokea mvua za wastani wa milimita 800 kwa mwaka.   Aidha, Kituo kina jumla ya hekta 11.2 (sawa na ekari 28). Hekt

MKURUGENZI KIBAHA DC ATEKELEZA MAAGIZO YA WAZIRI KWA VITENDO

Image
  MKURUGENZI KIBAHA DC ATEKELEZA MAAGIZO YA  Zaidi ya Wananchi 70 wameendelea kupata huduma ya kliniki ya Ardhi ya Mama Samia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Julai 4 mwaka huu. Bi Regina Bieda ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha amewasikiliza na kutatua migogoro midogo Kwa agizo la Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Aidha, Bieda amesema migogoro mikubwa ataendelea kuwakumbusha viongozi wake wa juu Kwa lengo kupata ufumbuzi kama alivyo ahidi Waziri Ardhi. Pia ameahidi kupitia timu yake ya wataalamu wa Ardhi na wanasheria kupanga utaratibu maalumu wa kutembelea mara Kwa mara maeneo yote yenye migogoro Kwa lengo la kutatua. Naye Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Brown Nziku amesema wataendelea na huduma ya kliniki ya Ardhi ndani ya Ofisi za Halmashauri Kwa utaratibu maalumu hivyo Wananchi wanakaribishwa. Zaidi ya Wananchi 70 wameendelea kupata huduma ya kliniki ya Ardhi ya Mama Samia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Julai 4 mwa